Ole wao wanaonizushia kwamba mimi ni miongoni mwa TeamBazazi…!

Kuna tabia mbaya sana ya kunichafua humu JF ambayo imezuka siku si nyingi. Nimevumilia lakini leo nimefika kikomo naomba nitoe msimamo wangu.

Napenda kuwatahadharisha wale wanaonizushia kwamba mimi ni miongoni mwa #TeamBazazi kwamba uvumilivu wangu umefika kikomo na atakayethubutu kunituhumu kwamba mimi ni miongoni mwa #TeamBazazi nitamfanyia kitu mbaya hata panya hawatabaki kwao......

Hivi mimi kama mwanaume rijali na mwenye siha nzuri mlitarajia niwe mtu wa namna gani, yaani kupenda kwangu kusafisha kiwi cha macho kwa warembo na kuusifu uumbaji wa maulana ndio iwe nongwa!

Kwanza naomba niwaulize, kwani majukumu ya mwanaume kwa mwanamke ni yapi na majukumu ya mwanamke kwa mwanaume ni yapi? Au mngefurahi sana kusikia kwamba mimi si rijali…?

Nasema ole wake atakayenihusisha na #TeamBazazi ………!

Ujumbe huu uwafikie......
watu8, Eiyer, Asprin, Mentor, Mr Rocky, Erickb52, KakaKiiza, Jiwe Linaloishi, Kaizer, Ruttashobolwa, @C6, Excel

Sikuiona hiii.Poleeee best yangu. Kwa hiyo tukuite rijali?????
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom