Ole Sosopi wa BAVICHA ameyasema haya baada ya Adhma na Zuio la Kwenda Dodoma kuzuia Mkutano wa CCM

SeriaJr TW

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
246
224
Awali ya yote nimshukuru Mungu kwa uzima aliotuonekania wote sisi viongozi wa Bavicha na wanachama wote.

Nitumie fursa hii adhimu sana kwa kifupi tu, kuwa shukuru vijana wote nchi nzima kwa support kubwa na hamasa mliyoionyesha tangu Bavicha tutoe tamko la kwenda Dodoma kuzuia mkusanyiko haramu wa CCM kufuatia kauli ya Jeshi la Polisi na Rais Mwema sana.

Tumepitia changamoto mbalimbali ambazo mpaka sasa adhima yetu imefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 99%.

Polisi na serikali wametambua nguvu tuliyonayo, ni kweli kabisa CCM bila polisi niwepesi kuliko tissue paper.
Viongozi wa Bavicha Taifa, mikoa, wilaya na kata tuko imara sana....
Hivi karibu tutawaeleza maamuzi mapya na tutaomba pia vijana wenzetu mtuunge mkono.

Shukrani nyingi sana pia makamanda wote waliotumia muda wao ku-amplify kazi zetu za Bavicha, kupitia Whatsup, FB, JF na Twitter na media zote.
......aluta continua........

*To Be Is To Do*

Ole Sosopi
13 July 2016
 
Back
Top Bottom