Ole Sendeka: Tutampa Magufuli uenyekiti wa CCM ili kuenzi mila ya chama

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968

Msemaji wa CCM christopher Ole Sendeka akiongea ofisi ndongo za CCM Lumumba Dar amesema kwenye mkutano mkuu utakaofanyika Julai 23 mwaka huu wanatarajia kuenzi mila ya chama cha mapinduzi kwa kumpa John Magufuli ambaye ni rais uenyekiti wa chama hicho siku hiyo kutoka kwa mwenyekiti wa sasa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni rais mstaafu
 
hivi kati ya mila ya chama na katiba ya chama kipi muhimu zaidi? huu uongozi wa kupeana utalitesa taifa letu...
 
Polisi vipi hawakuibuka?
 
Ila mkumbuke huyo Dereva alikwishawahi kutamka wazi wazi mbele ya umma " Mimi siyo dereva, sijui kuendesha na wala gari sitaki kuliongoza na leseni sina" Leo hii mnataka kumkabidhi busi lililojaa abiria aendeshe kwa miaka 5/10. litafika salama kweli?
 
Kweli mkuu, hebu tusubiri tuone
 
Okey,,,, kumbe hamna uchaguzi mtampatia kuendeleza mila za chama???? Hii inaleta raha ya demokrasia ndani ya chama chetu pendwa Ccm. Ole wenu mchukue form kubishana na mila za chama chetu.
Ila CUF, na CHADEMA acheni udikteta fuateni katiba kupata viongozi wa vyama vyenu.
 
Ila mkumbuke huyo Dereva alikwishawahi kutamka wazi wazi mbele ya umma " Mimi siyo dereva, sijui kuendesha na wala gari sitaki kuliongoza na leseni sina" Leo hii mnataka kumkabidhi busi lililojaa abiria aendeshe kwa miaka 5/10. litafika salama kweli?
Busi=Bus=Basi
 
Nina imani Magufuli atakirekebisha chama na kitakuwa mfano wa kuigwa duniani. Viva Magufuli....
 
khaaa! ina maana kna wakati walimuweka pending, yani hawakuwa ni imani nae ila kwa sababu tu ya utaratibu ndo mana wanaamua kumpa uenyekiti. inastaajabisha!
 
Hii hatari...tutampa Magufuli uenyekiti...kudumisha mila ndiyo hatari zaidi.

Ila kumbukeni Magu alishasema mapema yeye sio mwanasiasa akianza kulirekebisha gari msianze kulialia.
 
hivi kati ya mila ya chama na katiba ya chama kipi muhimu zaidi? huu uongozi wa kupeana utalitesa taifa letu...
Ni kweli mkuu kama sisi wanachadema tunavyoteseka na Mila ya chama chetu, mbowe hana kabisa mpango wa kufuata kanuni ya chana, ... Siasa za Tanzania ni uozo tu hasa huku kwenye vyama ambavyo wanalilia demokrasia ya nchi wakati ya kwao ndani ya chama inawashinda..
 
Msemaji wa CCM christopher Ole Sendeka akiongea ofisi ndongo za CCM Lumumba Dar amesema kwenye mkutano mkuu utakaofanyika Julai 23 mwaka huu wanatarajia kuenzi mila ya chama cha mapinduzi kwa kumpa John Magufuli ambaye ni rais uenyekiti wa chama hicho siku hiyo kutoka kwa mwenyekiti wa sasa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni rais mstaafu

Nilidhani mikutano imepigwa marufuku (hadi mahafali). Naona nilisahau kwamba CCM si chama cha siasa bali ni serikali. Nilisahau kwamba mkutano wa CCM ni sawa na mkutano wa baraza la mawaziri.
 
Ni kweli mkuu kama sisi wanachadema tunavyoteseka na Mila ya chama chetu, mbowe hana kabisa mpango wa kufuata kanuni ya chana, ... Siasa za Tanzania ni uozo tu hasa huku kwenye vyama ambavyo wanalilia demokrasia ya nchi wakati ya kwao ndani ya chama inawashinda..
haa haa kwa kweli ni shida. chama kimekabidhiwa dola kuongoza bado kinavunja katiba yake. je kweli watalinda katiba ya nchi? kweli ccm iliondoka na nyerere mwenyewe.
 
Back
Top Bottom