Ole Sendeka ahojiwa na timu ya Mangula

Ole Sendeka ahojiwa na timu ya Mangula

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

KITAIFA

Na Mussa Juma, Arusha

Posted Jumatano,Februari27 2013 saa 23:38 PM

KWA UFUPI

Kuhojiwa kwa Sendeka na viongozi wengine wa Simanjiro, kumekuja siku chache baada ya kuhojiwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk Mary

MBUNGE wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka na vigogo kadhaa wa CCM Wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Manyara, wamehojiwa na maofisa wa CCM, kuhusiana na malalamiko ya ukiukwaji wa taratibu katika uchaguzi wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya chama hicho (Nec) wa wilaya hiyo.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa mikakati ya Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Phillip Mangula, ambaye aliahidi kushughulikia malalamiko yote ya chaguzi zilizopita na kuyatolea uamuzi. Mangula ndiye Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Maadili ya CCM.

Kuhojiwa kwa Sendeka na viongozi wengine wa Simanjiro, kumekuja siku chache baada ya kuhojiwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk Mary Nagu ambaye pia ushindi wake wa Nec Wilaya ya Hanang, ulilalamikiwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye akisema kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu na kanuni za uchaguzi wakati wa kinyang'anyiro hicho.

Katika uchaguzi wa Simanjiro, Sendeka alishinda kwa kupata kura 471 dhidi ya Diwani wa CCM Kata ya Mirerani, Justin Nyari ambaye alipata kura 126.

Maofisa hao kutoka Makao Makuu ya CCM, wakiongozwa na Mwanasheria wa CCM, Glorius Luoga waliwahoji Sendeka na Katibu wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Jamillah Mujungu, Nyari na viongozi wengine wa chama hicho.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika wikiendi iliyopita, zimebainisha kuwa Nyari na makada kadhaa wa CCM, wanalalamikia ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi huo, ikiwamo kufanyika kwa kampeni kinyume cha taratibu kama kutawaliwa na ukabila, pia baadhi ya wapigakura kutokuwa halali.

Hata hivyo, Luoga ambaye pia ni Mjumbe wa Nec anayetoka Songea Vijijini, alipotakiwa kuelezea hatma ya malalamiko hayo, hakutaka kufafanua kwa maelezo kuwa yupo Zanzibar.
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Manyara, Ndekubali Ndeng'aso alikiri kufika kwa maofisa wa makao makuu ya chama hicho mkoani hapo na kuhojiana na walalamikaji na walilalamikiwa.

"Nadhani hizi ni taratibu za kawaida tu ndani ya chama, kuna ambao wamelalamika sasa chama kimeona ni busara kuwafuata na kujua malalamiko yao," alisema Ndeng'aso.
Sendeka na Nyari hawakupatikana jana kuelezea kilichojiri katika mahojiano hayo kwani simu zao za mkononi ziliita bila ya kupokewa.

Hata hivyo, Mujungu licha ya kukiri kuhojiwa alisema wenye mamlaka ya kuzungumza ni maofisa hao wa makao makuu... "Hili jambo lipo ngazi za juu nadhani wao ndiyo wana majibu ya maswali yenu."

Rushwa ndio FAGIO la USHINDI CCM; Sasa Tutaona nani atafukuzwa kama kweli wana UBAVU wa kuondosha mtu aliyehonga Madarakani; sababu kama wakifanya hivyo itafungua MILANGO ya WENGINE LOL; Sasa Hapo wale vijana waliokuwa CHADEMA wakakimbilia CCM sababu ya RUSHWA; Wanasema nini?? Au wanafumbia Macho?
 
Wakiondoa wahongaji nadhani chama kitakufa, nani atabaki.
 
MBUNGE wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka na vigogo kadhaa wa CCM Wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Manyara, wamehojiwa na maofisa wa CCM, kuhusiana na malalamiko ya ukiukwaji wa taratibu katika uchaguzi wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya chama hicho (Nec) wa wilaya hiyo.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa mikakati ya Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Phillip Mangula, ambaye aliahidi kushughulikia malalamiko yote ya chaguzi zilizopita na kuyatolea uamuzi. Mangula ndiye Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Maadili ya CCM.

Kuhojiwa kwa Sendeka na viongozi wengine wa Simanjiro, kumekuja siku chache baada ya kuhojiwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk Mary Nagu ambaye pia ushindi wake wa Nec Wilaya ya Hanang, ulilalamikiwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye akisema kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu na kanuni za uchaguzi wakati wa kinyang’anyiro hicho.

Katika uchaguzi wa Simanjiro, Sendeka alishinda kwa kupata kura 471 dhidi ya Diwani wa CCM Kata ya Mirerani, Justin Nyari ambaye alipata kura 126.

Maofisa hao kutoka Makao Makuu ya CCM, wakiongozwa na Mwanasheria wa CCM, Glorius Luoga waliwahoji Sendeka na Katibu wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Jamillah Mujungu, Nyari na viongozi wengine wa chama hicho.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika wikiendi iliyopita, zimebainisha kuwa Nyari na makada kadhaa wa CCM, wanalalamikia ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi huo, ikiwamo kufanyika kwa kampeni kinyume cha taratibu kama kutawaliwa na ukabila, pia baadhi ya wapigakura kutokuwa halali.

Hata hivyo, Luoga ambaye pia ni Mjumbe wa Nec anayetoka Songea Vijijini, alipotakiwa kuelezea hatma ya malalamiko hayo, hakutaka kufafanua kwa maelezo kuwa yupo Zanzibar.
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Manyara, Ndekubali Ndeng’aso alikiri kufika kwa maofisa wa makao makuu ya chama hicho mkoani hapo na kuhojiana na walalamikaji na walilalamikiwa.

“Nadhani hizi ni taratibu za kawaida tu ndani ya chama, kuna ambao wamelalamika sasa chama kimeona ni busara kuwafuata na kujua malalamiko yao,” alisema Ndeng’aso.
Sendeka na Nyari hawakupatikana jana kuelezea kilichojiri katika mahojiano hayo kwani simu zao za mkononi ziliita bila ya kupokewa.

Hata hivyo, Mujungu licha ya kukiri kuhojiwa alisema wenye mamlaka ya kuzungumza ni maofisa hao wa makao makuu... “Hili jambo lipo ngazi za juu nadhani wao ndiyo wana majibu ya maswali yenu.”

source. mwananchi
 
Wacha wafu waziki wafu wao.sendeka anajivunia tanzanite one kumpa mchanga na kudanganyia wajumbe wa wasimanjiro,
 
Chama kubwa linajua kufuata utaratibu sacoos hapo utasikia wamefukuzwa na kuvuliwa uanachama bila hata kuwapa nafasi ya kujieleza
 
Ukweli ni kwamba watalindana tu kwa kuwa ndiyo sera ya CCM.
 
Wanaoweza kufanya hivyo ni CHADEMA TU angalieni madiwani Arusha, Mwanza, Mara na BAVICHA nyie mnaigiza tu hakuna lolote
 
Back
Top Bottom