Ole Sendeka afichua ufisadi wa wabunge!

sokoinei

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
1,832
Reaction score
566
Bunge la Mchana siku ya Jumamosi wakati akihitimisha Hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini mh Prof Muhongo alimuita Sendeka kuwa ni muongo kwa kutaka kumlisha Mh Rais Maneno ambayo hakuyasema.

Hii ni baada ya Mh Sendeka wakati akichangia hotuba hiyo alisema kua Rais hajatimiza Ahadi aliyowahi kutoa kuwa baada ya kuisha kwa Mkataba wa kampuni ya Tanzaniteone serikali itatwaa Mgodi huo na kumilikisha Wachimbaji wadogo wadogo. Migodi hiyo ipo Mererani wilayani Simanjiro mkoaniManyara.

Akimjibu Sendeka Mh Waziri alisema kua siku moja aliwahi kumuuliza swala hilo na yeye waziri alienda kwa Mh Rais na kumuuliza lakini Mh rais alisema kua hayo maneno hakuwahi kuzungumza isipo kua Sendeka anamsingizia.

Mh waziri alionya wale wote wenye tabia ya kuzungumza vitu vya uongo na kumlisha Rais maneno ambayo hakusema. Mh Waziri Muhongo Wakati akikamilisha kujibu hoja za Wabunge ndipo Mh Sendeka akaomba Muongozo lakini Spika alimkatalia.

Je Spika kumnyima Sendeka nafasi ya kuwasilisha Muongozo ni Demokrasia au anabalance mambo ili na wabunge wa Upinzani wakiomba muongozo awanyime kama tulivyoona?

 
huyu mzee amenyimwa kitalu mererani ndio maana anatoa povu,wote wazee wa 10% hakuna msafi ccm
 
Siku hizi ni kawaida ku-balance equation! Ukiifungia Redio Imani, lazima uifungie pia Redio Kwa Neema! Ukisema Makanisa yanachomwa, ni lazima pia usema Msikitiki inachomwa-hata kama haujachomwa hata mmoja! CCM wakianza kuhubiri udini (CUF Waislamu, Chadema Wakatoliki), baadaye watasema waendesha udini ni CUF na Chadema- Hiyo yote ni ku-balance equation!!! This is Bongo!
 
Ha haa! Magamba yamepata moto!
 
Makinda amewekw pale kulinda maslahi ya ccm kwahiyo jambo lolote limaloweza kukiumbua chama au kumuumbua rais hawezi kuliacha lipite
 
JK kakataa kauli yake na Bi Kiroboto kamulinda kwa kutumia uspika wake, fungua hapa...

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...miliki-kampuni-ya-tanzanite-one-14-print.html

Halafu msome waziri wetu wa Nishati na Madini Mr muongo

DailyNews Online Edition - State to acquire 50 pc stake in TanzaniteOne

Kuthibitisha kuwa Sendeka anasema kweli basi soma hapa chini penye red...


Kweli Tanzania kuna wahuni, Mtu anaomba apatiwe kura na akishapata anachukua yeye kile alichowaahidi wapiga kura na kuvaa miwani ya mbao, Nafikiri James Ole Millya hapa ana siri ndefu
 

Ni hakika mkuu kila kitu Serikali yetu "sikivu" inafanya kwa kubalance japokuwa Ndugu Musa Zungu aligoma sijui yeye ndo Msemaji wa Serikali.
 


Hapo kwenye red mkuu nia ya Spika sio Demokrasia wala kubalance mambo kuwaridhisha wapinzani hapa spika anajaribu kuifichia aibu serikali iwapo Ole Sendeka angekomaa kuleta ushahidi ili kudhibitisha kauli yake,ujue madam spika ana kazi mbili moja ni kuwadhibiti wapinzani na pili ni kuilinda serikali ya Dhaifu.
 
ah!!!!! nafuu Sendeka akasirishwe maana kasinzia sana. Na leo Dr. Slaa yupo Simanjiro, anamtafuna kwakwenda mbele.
 
WACHA MOTO UWAKE, :A S-fire1: SERIKALI INAKOPA HELA WORLD BANK NA ADB DOLLA MILLION 500 KULIPIA MADENI YA TANESCO, NI UPUUUZI WA HALI YA JUU, PROFESA BORA AKASHIKE CHAKI
 
Ile hutuba ilikuwa na magumashi kibao! Inaonekana alichokuwa akikiongea wazir hakina fact yeyote kakosea saaana ... Kajichanganya mpaka akasema walishajiloga wakauza nchi(sehemu zote za machimbo) so kama walivo impotence hawana uwezo wa kujisahahisha ili kuwapa wananchi japo kasemu kakuchimba ile hali kila siku utawasikia wakituhadaa kuwa mikataba yote mibovu wanaipitia upya kumbe danganya toto kama hii aliyofanyiwa olesendeka!!
 
Hata akileta ushahidi utafungiwa kabatini tu. bongoo!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Naamini JK ahadi alizo toa wakati wa kampeni anaweza akawa anakumbuka kumi tu.
 
Hapana, Spika alikuwa akimlinda Rais na ahadi yake, maana angemruhusu angethibitisha kuwa hajatendewa haki kuitwa muongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…