Ole Sabaya ataka kesi yake iharakishwe

Ole Sabaya ataka kesi yake iharakishwe

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
18,302
Reaction score
31,559
Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ameieleza Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi kuwa anateseka gerezani kwa kuwa ni mgonjwa na akaomba upande wa mashtaka uharakishe upelelezi wa kesi dhidi yake.

Huku akibubujikwa na machozi, Sabaya alisema gerezani si sehemu ya ‘picknic’.

Sabaya na wenzake wanne wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwemo uhujumu uchumi na kujipatia Sh30 milioni kutoka kwa mfanyabiashara wa Bomang’ombe, Alex Swai aliyedaiwa kukwepa kodi.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Sylvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey.

Kesi hiyo namba 2 ya 2022 yenye inasikilizwa na Hakimu Mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Salome Mshasha. Upande wa Jam huri una mawakili wanne Tumain Kweka, Khalili Nuda, Verediana Mlenza na Suzy Kimaro.

Hata hivyo, wakati wakili Mlenza akiomba kuahirishwa kwa kesi hiyo kutokana na upelelezi wa shauri hilo kutokamilika, Sabaya alinyoosha mkono mahakamani hapo na alipopewa nafasi alitoa ombi lake

Ombi la Sabaya

“Mheshimiwa hakimu, kwa kuwa kesi hii ililetwa hapa Juni mosi mwaka huu na ikaelezwa mbele ya mahakama hii kuwa upelelezi umekamilika na mwendesha mashtaka akaomba tarehe ya karibu kwa ajili ya usikilizwahi wa kesi hii, kinachokwamisha kesi hii ni nini, tunaonewa, tunaomba Ofisi ya DPP ijue kinachofanyika kwenye ofisi yake.”

“Wakati tunaletwa Gereza la Karanga tulichukuliwa mazingira ya usiku na ya kutisha, tunaumia sana tunateseka na mimi ni mgonjwa, tuna imani na ofisi ya DPP ndiyo maana tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aingilie kati kwa sababu tunaonewa,” alieleza Sabaya.

Wakili wa utetezi, Hellen Mahuna aliutaka upande wa mashtaka kuwa makini kwa kuwa ulishasema upelelezi umekamilika nna jana ukasema haujakamilika.

Hakimu anayeisikiliza kesi hiyo, Mshasha alisema hoja ya upande wa utetezi ni za msingi kwa kuwa awali upande wa mashitaka waliieleza mahakama kuwa upelelezi umekamilika.

“Nimesikiliza hoja za pande zote mbili,na hoja za upande wa utetezi ni za msingi na zina mashiko kwa hiyo naahirisha kesi hii mpaka Julai 4 mwaka huu angalau upande wa mashtaka uje na hitimisho,” alisema.

Mwananchi
 
Taarifa za ndani ya gereza la Karanga zinaonyesha , General Sabaya anaishi na simu yake ya mkononi huko Gereza la Karanga na usiku anawasiliana na watu mbali mbali, ikiwemo Ofisi ya DPP.

Je, sabaya anaruhusiwa kukaa ns simu Gerezani?

Kama haruhusiwi mkuu wa Gereza la Karanga unaitafuta serikali maneno.
 
Je sabaya anaruhusiwa kukaa ns simu Gerezani?
Kama haruhusiwi mkuu wa Gereza na Karanga unaitafuta serikali maneno.
Lete ushahidi achana na stori za kuambiwa
 
Ninakuwekea namba za simu ambazo sabaya amekuwa akipiga na kuongea nazo kwa simu yake na TCRA wazipokee . Huku sio Fb mkuu
Toa ushahidi, kilichopo ni kwamba hakuna mfungwa wala mahabusu anaekaa na simu
 
Taarifa za ndani ya gereza la Karanga zinaonyesha , General Sabaya anaishi na simu yake ya mkononi huko Gereza la Karanga na usiku anawasiliana na watu mbali mbali, ikiwemo Ofisi ya DP...
kaka hii nchi ni ngumu, ukitaka kujaribu kila kitu presha itakupanda.
 
Iharakishwe?? Na akitolewa arudishe haraka mali za watu, ikiwa ni kweli alifanya hayo! Otherwise watamuuwa aise
 
Hamna kitu hapa kesi ni ngumu ukiwa gerezani tu, ila ukisha kuwa uraiani ni chap tu
 
Hata akitoka leo naamini hali ya Jiji la Arusha itakuwa shwari,hatutaona ule ubabe wake na misafara yake ikiwa na gari zenye namba za UN za kimagumashi,zile fujo zake zote na kunyenyekewa kwake kote alikokuwa ananyenyekewa sehemu za starehe HAKUTAKUWEPO,kule kunywa bila kulipa Bill HAKUTAKUWEPO tena,hata akiona Kuku au Mbuzi barabarani atakuwa anapiga goti na kutoa Shikamoo,hivi sasa ni saa 9 kasoro,kwa taratibu za Jela Jenerali Sabaya anatakiwa aingie Selo kwake kulala,daaah maisha haya[emoji1787][emoji1787]
 
Taarifa za ndani ya gereza la Karanga zinaonyesha , General Sabaya anaishi na simu yake ya mkononi huko Gereza la Karanga na usiku anawasiliana na watu mbali mbali, ikiwemo Ofisi ya DPP.

Je, sabaya anaruhusiwa kukaa ns simu Gerezani?

Kama haruhusiwi mkuu wa Gereza la Karanga unaitafuta serikali maneno.
Kama ni kweli hii mbaya Sana afunguliwe Kesi ya kumiliki simu ndani ya gereza na ikiisha hii ndo ianze hyo ya simu, nakumbuka kuna mwamba mmoja nae alikua ana simu akiwa jela akawa anampigia bro JK kutokea gerezan kilichotokea ni akapewa Kesi ingine tena. Hebu weka namba nimuulize kama amekula ugali na nini mchana huu na je akitoka atakoma ujinga wake ule au
 
Alikua ni Amatus Liyumba wa BOT.
 
Lete ushahidi achana na stori za kuambiwa
Namba anayowasiliana / wanao Wasiliana/ kupigana au kuongea na Sabaya wahusika Hawa hapa.
1. 0754-980805
2.0764-223300
Nitaendekea ukukuwekea namba kuhitagi ushahidi zaidi.
Ndio sababu tunasema General Sabaya anayo simu gerezani na huwa wana Ongea usiku wa manane.
 
Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ameieleza Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi kuwa anateseka gerezani kwa kuwa ni mgonjwa na akaomba upande wa mashtaka uharakishe upelelezi wa kesi dhidi yake.

Huku akibubujikwa na machozi, Sabaya alisema gerezani si sehemu ya ‘picknic’.

Sabaya na wenzake wanne wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwemo uhujumu uchumi na kujipatia Sh30 milioni kutoka kwa mfanyabiashara wa Bomang’ombe, Alex Swai aliyedaiwa kukwepa kodi.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Sylvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey.

Kesi hiyo namba 2 ya 2022 yenye inasikilizwa na Hakimu Mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Salome Mshasha. Upande wa Jam huri una mawakili wanne Tumain Kweka, Khalili Nuda, Verediana Mlenza na Suzy Kimaro.

Hata hivyo, wakati wakili Mlenza akiomba kuahirishwa kwa kesi hiyo kutokana na upelelezi wa shauri hilo kutokamilika, Sabaya alinyoosha mkono mahakamani hapo na alipopewa nafasi alitoa ombi lake

Ombi la Sabaya

“Mheshimiwa hakimu, kwa kuwa kesi hii ililetwa hapa Juni mosi mwaka huu na ikaelezwa mbele ya mahakama hii kuwa upelelezi umekamilika na mwendesha mashtaka akaomba tarehe ya karibu kwa ajili ya usikilizwahi wa kesi hii, kinachokwamisha kesi hii ni nini, tunaonewa, tunaomba Ofisi ya DPP ijue kinachofanyika kwenye ofisi yake.”

“Wakati tunaletwa Gereza la Karanga tulichukuliwa mazingira ya usiku na ya kutisha, tunaumia sana tunateseka na mimi ni mgonjwa, tuna imani na ofisi ya DPP ndiyo maana tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aingilie kati kwa sababu tunaonewa,” alieleza Sabaya.

Wakili wa utetezi, Hellen Mahuna aliutaka upande wa mashtaka kuwa makini kwa kuwa ulishasema upelelezi umekamilika nna jana ukasema haujakamilika.

Hakimu anayeisikiliza kesi hiyo, Mshasha alisema hoja ya upande wa utetezi ni za msingi kwa kuwa awali upande wa mashitaka waliieleza mahakama kuwa upelelezi umekamilika.

“Nimesikiliza hoja za pande zote mbili,na hoja za upande wa utetezi ni za msingi na zina mashiko kwa hiyo naahirisha kesi hii mpaka Julai 4 mwaka huu angalau upande wa mashtaka uje na hitimisho,” alisema.

Mwananchi
Kiburi cha uzima ukichanganya na madarska ya kuokota ni kibaya sana.
 
Huku akibubujikwa na machozi, Sabaya alisema gerezani si sehemu ya ‘picknic’.

Wakati tunaletwa Gereza la Karanga tulichukuliwa mazingira ya usiku na ya kutisha, tunaumia sana tunateseka na mimi ni mgonjwa, tuna imani na ofisi ya DPP ndiyo maana tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aingilie kati kwa sababu tunaonewa,” alieleza Sabaya.
Justice delayed is justice denied.
 
Back
Top Bottom