Ole Medeye jiandae kuachia jimbo

2010 mgombea wa CDM Ole Kisambu alimpeleka sana Ole Medeye tatizo hakuwa na comitted mawakala ktk maeneo ya Oljoro na Mirongine ambao by saa 7 wengi wao walikuwa washalewa na kama sikosei CDM arumeru Magh ina madiwani 6 means inatawala kata 6 kuanzia kiranyi na tayari CDM ina nguvu huu ukanda wa Nairobi road nguvu ielekezwe upande wa chini wa barabara ya BAbati huko ndo bado ila 2015 hadi Longido CDM inabeba wana hasira na CCM haijawalipa fidia ya mifugo yao ilyokufa ingawa inatangaza imelipa

Kumbukeni Arumeru magh hatutaki Olmekiii tunataka muarusha au Mmasai full stop
 
hoja yako ni nzuri, hao waarusha wenyewe wameanza kubadilika, arumeru magharibi ina miundo mbinu mibovu sana, kuanzia sanawari, ilboru, mianzini, sakina, ngaramtoni n.k. huwez kuamini ni maeneo yaliyo karibu na mjini. na hakika chadema watachukua jimbo hili 2015, wajitahidi sana kulinda kura zao kwani nimejifunza huwa wanachakachuliwa sana. OLE KISAMBU alikuwa na hoja nzuri sana nilishangazwa kabisa na ushindi wa OLE MEDEYE.
 
kipuyo,elisa mollel na sasa ole medey hawajaitendea haki arumeru magharibi.pamoja na kwamba jimbo hili liko mpakani mwa kenya na tanzania na pia kupakana na manispaa ya arusha bado tunaendelea kushuhudia wakazi wake wakiwa maskini na ombaomba mijini.
Wakazi wa jimbo hili hawajui kusoma na kuandika.
Watoto wa ki-arusha wanakufa kwa utapiamlo na magonjwa ya kuambukiza.

Pesa iliyopatikana wakati wa mchakato wa uuzaji wa viwanja vya burka haieleweki imetumika vipi.

Mbunge wake hajawahi kusimama bungeni na kuuliza kwa nini barabara namanga-arusha iliyokuwa ikamilike na kukabidhiwa august mwaka jana haijakamilika mpaka leo.

Ol medey jiandae

Wameshidwa kujenga soko la oldonyosambu lichafu kazi kukusanya ushuru tu na kuwakimbiza mamayeyo na mboga na vitunguu, soko la kisongo hamna hata choo cha uhakika mvua ikinyesha balaa.Kile kidaraja pale ngaramtoni kimechakaa sijui kama wana mpango wakukijenga siku ya soko ndo hapapitiki japo sasa hivi soko limehamishiwa juu lakini bado hapavutii.
 
najiandaa kuchukua jimbo hili mnipe sapoti wakuu. Nimezaliwa Kijiji cha Manyire Kata Mlangarifni nina uwezo na elimu ya degree 2. Matatizo ya Arumeru mgrb ndio profession yangu niliosomea.

Huwezi kusomea matatizo ya Wana Arumeru Magharibi.Kujua matatizo ya ndugu zetu ni lazima uwe umetoka katika mazingira wanayoishi.Mkuu kwa hili sio kweli ila ningeshauri ni vyema kujua matatizo ya wananchi.Hauitaji kwenda Chuo kikuu kusomea ,matatizo ya watu, ila inakusaidia jinsi gani utaweza kujenga hoja ili angalau uweze kuleta mabadiliko na kutatua matatizo ya wananchi kushirikiana na Serikali,Wafadhili,Wananchi wenyewe na Stakeholders wengine..
 
Wameshidwa kujenga soko la oldonyosambu lichafu kazi kukusanya ushuru tu na kuwakimbiza mamayeyo na mboga na vitunguu, soko la kisongo hamna hata choo cha uhakika mvua ikinyesha balaa.Kile kidaraja pale ngaramtoni kimechakaa sijui kama wana mpango wakukijenga siku ya soko ndo hapapitiki japo sasa hivi soko limehamishiwa juu lakini bado hapavutii.

Mkuu soko la oldonyosambu wamejenga sema wamechakachua bati linavuja mbaya kwa ujumla hakukuwa na value for money.bora hata soko jipya la ngaramtoni.hope utakubaliana na mimi.medeye kazi yake kupita kila kata@kusaini visitor book.
 
naona lema anaendelea kuchota wafuasi wa ccm na kuwauzia kadi za chadema kama njugu!
 
Back
Top Bottom