Ole Medeye 'ajitumbua mwenyewe' UDP, Cheyo abaki mpweke

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,883
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha 'The United Democratic Party' (UDP) ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi hiyo kwa madai ya kujipa fursa ya kuitumikia familia yake.




Ole%20Medeye.JPG

John Cheyo (Kushoto) akiwa na Goodluck Ole Medeye

Ole Medeye ambaye alijiunga na UDP akitokea CHADEMA mapema mwaka jana, ametoa kauli hiyo leo katika barua aliyomuandikia Mwenyekiti wa chama hicho Mh. John Cheyo, huku akimshukuru kwa kumuani katika nafasi hiyo kwa kipindi chote.

"Napenda kukujulisha rasmi kwamba ili nipate muda wa kutosha kufanya shughuli za ustawi na maendeleo ya familia na jamii inayonitegemea nimeamua kwa hiari yangu kujiuzulu nafasi hiyo ya Katibu Mkuu kuanzia tarehe ya barua hii".Imesema sehemu ya barua hiyo

Mwanasiasa huyo amewahi kushika nyazifa mbalimbali ikiwemo Ubunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi kupitia CCM katika Bunge la 10 na kupitia nafasi hiyo aliweza pia kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika serikali ya awamu ya nne.

Mara baada ya kushindwa katika kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, aliamua kuhama chama na kujiunga na CHADEMA ambapo hakudumu sana licha ya CHADEMA kumpa nafasi ya kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kisha alihamia UDP kabla ya kupewa nafasi ya Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho.



Ole%20medeye%20barua.JPG
 
Pole medeye ulikuwa hujui ulitendalo. Kutoka naibu Waziri mpk mzururaji was vyama. Ametoka ndiyoooooooo then cdm mpk kafika iliyokuwa ccmb akakosa support. Pole, umestaafu vibaya.
 
Sio siku nyingim atarudi ccm. CCM wameona hawana wa kusimamisha mkoa wote wa Arusha hivyo wesha mtongoza angalau apeperushe tena bendera ya ccm
 
Mtu ulishafikia hatua ya uwaziri kushindwa ubunge tu unaanza kutangatanga ....huyu ndio bye bye kwenye siasa labda abebwe na wenye siasa zao ...
 
Nimependa sana post ya ndotilo nimecheka hatari.kiukweli kawa mzururaji asiyejua aende wapi kama kichaa vile! Huyo imekula kwake kurudi ccm na kupewa fursa akae miaka mitatu, ndo kwishine huyo labda abebwe tu.
 
Back
Top Bottom