Oldupai Gorge ipo Tanzania -TTB

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imeonya kuhusu upotoshaji unaofanywa kupitia mitandao ya kijamii kwamba eneo la Oldupai Gorge lipo nchi jirani ya Kenya na kuitaka dunia kutambua eneo hilo lipo Tanzania.

TTB imesisitiza pia kuwa vivutio vingine, ikiwamo Mlima Kilimanjaro, ulio mrefu kuliko yote barani Afrika, upo Tanzania na si vinginevyo.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na TTB kukanusha taarifa zinazosambazwa katika mitandao hiyo, ikiwamo YouTube, kuhusu eneo la Oldupai Gorge kuwa Kenya na kuonya kuwa eneo hilo lipo Tanzania.

“TTB imekuwa ikifuatilia video iliyotumwa katika YouTube na imekuwa ikisambazwa kupitia njia mbalimbali za habari ikimuonesha mtu mmoja kutoka nchi jirani akisema kuwa Olduvai (Oldupai) Gorge ambayo kimsingi iko Tanzania kwamba iko Kenya.”

Ilisema taarifa hiyo. Eneo hilo la Oldupai Gorge liko katika Bonde la Ufa katikati ya Bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Manyara nchini Tanzania, ilieleza taarifa hiyo.

TTB katika taarifa hiyo ilieleza kupinga upotoshwaji huo uliofanywa na mtu huyo wakati akihutubia mkutano ambao ulikuwa ni wa Vijana wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Marekani Agosti mwaka jana.

Ilifafanua kuwa bodi hiyo inataka dunia ijue kuwa kama ilivyo kwa Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Zanzibar na vivutio vinginevyo, Oldupai Gorge ipo Tanzania.

Ilieleza kuwa eneo hilo ambako kunaaminika ndiko binadamu wa kwanza duniani aliishi na ambako Dk Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la binadamu huyo wa kale anayesadikiwa kuishi miaka takribani milioni mbili na historia, utafiti na jiografia inathibitisha ipo Tanzania na si mahali pengine popote duniani.
 
HA HA HA HAAAAA DAH! IMEBIDI NICHEKE KWA HERUFI KUBWA !!!!! KUMBE SERENGETI IPO MKOANI MANYARA KWELI HII BODI YA UTALII NI TEZI DUME NA SIO JIPU. si ajabu wenzetu wamejua weakness yetu thats why wanatumia hiyo nafasi effectively
 
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imeonya kuhusu upotoshaji unaofanywa kupitia mitandao ya kijamii kwamba eneo la Oldupai Gorge lipo nchi jirani ya Kenya na kuitaka dunia kutambua eneo hilo lipo Tanzania.

TTB imesisitiza pia kuwa vivutio vingine, ikiwamo Mlima Kilimanjaro, ulio mrefu kuliko yote barani Afrika, upo Tanzania na si vinginevyo.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na TTB kukanusha taarifa zinazosambazwa katika mitandao hiyo, ikiwamo YouTube, kuhusu eneo la Oldupai Gorge kuwa Kenya na kuonya kuwa eneo hilo lipo Tanzania.

“TTB imekuwa ikifuatilia video iliyotumwa katika YouTube na imekuwa ikisambazwa kupitia njia mbalimbali za habari ikimuonesha mtu mmoja kutoka nchi jirani akisema kuwa Olduvai (Oldupai) Gorge ambayo kimsingi iko Tanzania kwamba iko Kenya.”

Ilisema taarifa hiyo. Eneo hilo la Oldupai Gorge liko katika Bonde la Ufa katikati ya Bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Manyara nchini Tanzania, ilieleza taarifa hiyo.

TTB katika taarifa hiyo ilieleza kupinga upotoshwaji huo uliofanywa na mtu huyo wakati akihutubia mkutano ambao ulikuwa ni wa Vijana wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Marekani Agosti mwaka jana.

Ilifafanua kuwa bodi hiyo inataka dunia ijue kuwa kama ilivyo kwa Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Zanzibar na vivutio vinginevyo, Oldupai Gorge ipo Tanzania.

Ilieleza kuwa eneo hilo ambako kunaaminika ndiko binadamu wa kwanza duniani aliishi na ambako Dk Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la binadamu huyo wa kale anayesadikiwa kuishi miaka takribani milioni mbili na historia, utafiti na jiografia inathibitisha ipo Tanzania na si mahali pengine popote duniani.

Sasa TTB inamuonya nani??SI ikamuonye aliyetangaza kwenye Mkutano wa Vijana wa UN ,Rosemary Odinga?Wapuuzi kweli hao TTB
 
Back
Top Bottom