nakumbuka sana enzi hizo nilikuwa seminari moja huko sengerema(Mary Queen of the Apostles Sengerema Seminary), barua zikija lazima Rector hazifungue basi tukabuni kwamba zile barua zote ambazo ni hatarishi zitokazo Bukumbi na Nganza tuwe tunazipitishia sengerema secondari. Tukaweka agenti kule barua zote zikawa zinaaandikwa kwa kupitia kwake, alafu siku tukipata free and out jumamosi ya kwanza ya mwezi tunazifuata.....tulifanikiwa kwa kiasi fulani. Room master siku zote kilikuwa cheo cha form one ili awajibike kusafisha chumba mwenyewe kwani wakuojiwa ni yeye kama chumba kitakuwa kichafu. Tukiwa form one tulikataa kuosha madishi tukapigwa mchinjo(kunyimwa chakula) hadi tukaunda kamati ya kusaidiana tukawa tunachanga pesa na kufata matinda mjini tunajificha polini tunakula kwani sheria ilikuwa hairuhusu kwenda na chakula chochote maeneo ya seminarini, nakumbuka ilikuwa mwezi wa tisa ndo yalitukumba hayo hivyo na sisi tukanuwia kuwatesa kwa mateso makali waseminari watakaokuja kuanza form one sisi tukiwa form two. Kweli tulipofungua shule tu na kuitwa form two watu walipania sana kutesa form one hivyo mimi nilifika jioni siku na kukuta tayari form two watatu wameishafukuzwa kwa kuwalazimisha form one kusukuma choo eti gari ya rector imekwama, walikuwa wakisukumwa huku wakipewa kipigo. Pamoja na hayo yote hatukukata tamaa, utesaji uliendelea na ilipofika mwezi wa tisa tulikaa kikao cha kuhimiza kuongeza kiwango cha utesaji ikiwa ni kukumbuka mateso tuloteswa sisi, kikao kilipendekeza kwamba siku ya mwisho ya kufunga mateso yaani tarh 30/9/....lazima usiku kama Rector na Spritual Director hawatakuwepo kichapo kitolewe. Basi siku ya kuhitimisha mateso kweli Rector hakuwepo, form one walikuwa wanasomea katika ukumbi wa kulia chakula, mimi niliwekwa katika kitengo cha kuzima taa, kilikuwepo kitengo cha fimbo kitakachobaki nje ya ukumbi na kuwacharaza form one wote watakaofanikiwa kutoka nje vilevile kilikuwepo kitengo cha wavamizi ambao taa zikizimwa tu, watavamia na kuanza kutembeza kisago. Kweli nilifanikiwa kuingia mle ukumbini na kujifanya nimekwenda kunywa maji ya kunywa, palepale nilizima taa na fujo zikaanza, tulipanga zoezi hili lifanyike kwa muda wa dakika tatu tu. Baada ya dakika tatu wote tulikuwa tuko darasani, viongozi wengi walikuwa form three hivyo walisikia purukushani walipofika hawakukuta watu kwani form one wote walikuwa wamekimblia vichakani usiku huo na sisi tayari tulikuwa darasani kimya tukijisomea. Baadaye walifanikiwa kumwona form one mmoja raia wa musoma, akawapa full stori alikuwa amepasuka kichwani kwani aliingia chini ya meza akafumuliwa buti moja na li-form two moja pia la musoma. Hofu ilitawala kwa wote viongozi na sisi form two kwani tulijua rector angefika na kukuta hali ile ya kutoonekana baadhi ya form one na kuumia kwa huyo jamaa basi form two wote tungeondoshwa vilevile viongozi nao wangefukuzwa. Hivyo hapakuwa na wakumlaumu mwenzake kwani hata hao viongozi enzi zao walitutendea hayo ingawa ni kwa style nyingine. Ilibidi tukubaliane kuanza kuwatafuta form one kule porini, kazi ilikuwa ngumu kwani kila walipotuona walizidi kujificha wakidhani tunaendeleza kichapo, hadi muda wa kulala saa 4 kamili usiku ilifika baadhi yao wakiwa hawajaonekana, vilevile tulishirikiana na viongozi kumshawishi yule aliyeumia kuwa kesho yake achukue daftari la wagonjwa bila rector kumuona aende hospitali alafu akirudi asitoke nje sisi tutamuhudumia kwa kila kitu ikawa ni pamoja na kumpelekea chakula chumbani. Alikaa ndani kwa muda wa siku tatu ndo akaanza kutoka nje tukamwambia rector akimuuliza aseme aliumia mpirani, kweli alishawishika kwani tulimwambia kuwa hata yeye akifika form two atayafanya hayohayo na mtu akifukuzwa kwa ajiri yake basi hata yeye atafukuzwa kwani akifanya kosa dogo tu huwa inaangaliwa alishawahi kumfukuzisha nani, tulimtisha kwamba ukifukuzisha mtu ikitokea ukakamatwa hata unaongea kiswahili lazima uondoke na huu ndo ulikuwa ukweli......yapo mengi ya kukumbuka, lakini all in all nimefanikiwa kuwa Baba Paroko.