OLAMS, mfumo wa HESLB ni aibu tupu!

Underwood

JF-Expert Member
Dec 25, 2020
1,909
3,117
IMG_8443.jpg


Waungwana,

Julai 16, bodi ya mikopo elimu ya juu HESLB walitangaza kufunguliwa rasmi kwa dirisha la maombi ya mikopo huku wakitaka waombaji watumie mfumo wao wa OLAMS kufanya maombi.

Sasa ni takribani wiki ya pili mfumo wa maombi ya mkopo haufanyi kazi inayoeleweka. Kila mtu anayejaribu kufanya maombi anakwama kwa namna yake na wakati wake, wengine hawawezi kutuma taarifa, wengine wameshindwa hata kuanza kwani controll number hazitoki, wengine demographic information wakituma haziendi interface inaonyesha loading hadi kesho na kama utakosea katika hatua yoyote, hakuna option ya ku-edit. Matatizo ni mengi sana.

Bila kupepesa macho, mfumo huu ni mbovu kupitiliza na tatizo sio kuelemewa kwa mtandao kama baadhi wanavyohizi bali ukosefu wa uwezo (incompetence) na uzembe wa developers na wasinamizi wa mfumo wenyewe.

Kwa kuukagua mfumo wenyewe kidogo tu inaonyesha jinsi gani developers hawakufuata kwa usahihi hatua yoyote muhimu wakati wa kuunda mfumo wenyewe hasa testing.

Errors zinazoonekana kwenye inspection ni zile ambazo zilitakiwa kuwa fixed wakati wa development ya mfumo lakini ajabu ni kwamba kwa sasa ndio errors zinazosumbua watumiaji wa kawaida wa mfumo.

Just imagine (kwa wataalam) mfumo uko hosted ukiwa kwenye development mode na sio production mode.

Pamoja na tabu zote hizo, namba za msaada kwa waombaji hazipokelewi au zinatumika muda wote, kwenye kurasa za mitandao ya kijamii malalamiko yamejaa kwenye comment sections lakini hakuna anayejishughulisha.

Ni wazi kwamba, shida hizi ni baada ya kubadilishwa kwa mfumo wa zamani na kuletwa kwa mfumo mpya ambao ni wa hovyo kulinganisha na ule wa zamani. Kulikuwa na haja gani ya kubadili mfumo ilhali kukiwa hakuna mbadala wa uhakika kwa mfumo uliopita? Hii ni downgrade!

Nimeshuuhudia mifumo inayochechemea, OLAMS unatia aibu. Ni aibukwamba huu ndio mfumo unaotegemewa kufanikisha mchakato wa watoto wa masikini kwenda vyuo vikuu.

Rai yangu:
Taasisi zote, za umma na binafsi, zinapaswa kuwa makini na kuhakikisha zinatumia watu sahihi katika shughuli zao ili kuepusha kama sio kupunguza uzembe, hasara na taharuki nyingine zinazoweza kujitokeza, hili la bodi ya mikopo ya elimu ya juu liwe funzo.


IMG_8439.jpg


IMG_8440.jpg


IMG_8441.jpg


IMG_8442.jpg


Ngoja tuone.
 
Mfumo una sehemu kibao za kulogin. Kwanini isiwe moja na mtu awe redirected kutokana role aliyojisajili?

Kulogin kwenye mfumo ni suala la bahati nasibu yaani mfumo mpya hautambui credetials za watumiaji wa mfumo wa zamani.

Tatizo linaanzia kwenye front end mpaka backend.
 
Tanzania ni kichwa cha Mwendawazimu

Kwa Bongo hilo halishangazi

Kila mahali jau
 
Back
Top Bottom