Wewe vepee! Inaniuma kishenzi aisei, hasa kule timu kufungwa na Green Worriers, Azam na kufukuzwa Omog wakati tuna bonge la mchezaji wetu Okwi ambae huenda angesaidia kuepusha yote haya. Utakiona kitakachotokea tena kwa URA na kombe la Mapinduzi!!Wewe inakuhusu nini au lini uliombwa ukatoe msaada simba kwa niaba ya Okwi
Wapo pia Ngoma na Chirwa, ambao wamepokelewa kishujaa na wapo ZanzibarWewe vepee! Inaniuma kishenzi aisei, hasa kule timu kufungwa na Green Worriers, Azam na kufukuzwa Omog wakati tuna bonge la mchezaji wetu Okwi ambae huenda angesaidia kuepusha yote haya.
Ni kweli hawapo pia, lakini sababu ya kutokuwepo inafahamika vema "U-KA-TA" ndani ya club kitu ambacho hakipo Simba.Wapo pia Ngoma na Chirwa, ambao wamepokelewa kishujaa na wapo Zanzibar
Umeongea Mkuu.Wewe vepee! Inaniuma kishenzi aisei, hasa kule timu kufungwa na Green Worriers, Azam na kufukuzwa Omog wakati tuna bonge la mchezaji wetu Okwi ambae huenda angesaidia kuepusha yote haya. Utakiona kitakachotokea tena kwa URA na kombe la Mapinduzi!!
Hiki ndicho nilichookimaanisha mimi kwenye uzi huu, achana na mawazo ya suSzu36Umeongea Mkuu.
Okwi mimi ananikera sana kama mpenzi wa timu ya Simba.
Simba inatatizo la mshambuliaji mfungaji, inaamua kusajiri mshambuliaji wa kimataifa Okwi.
Okwi hana muda wa kuichezea Simba, akicheza mechi moja au mbili anatafuta sababu na kuondoka zake anakokujua yeye.
Timu inakosa mgungaji wake mahili na inaishia kufungwa na timu pinzani.
Sasa Simba kama timu inayohitaji ushindi inamchukuliaje huyu mshambuliaji wake wa kimataifa ambaye mda wake mwingi anautumia kuzurula mitaani ?
Simba inahitaji ushindi au inamuhitaji mtalii Okwi ?
Ningekuwa mdau wa usajiri wa timu ya Simba hakika ningemfukuza Okwi, potelea mbali ningekubali ghalama ya kumlipa ili akuze utalii wake anaoupenda.
Simba tunahitaji mshambuliji MWENYE MUDA WA KUICHEZEA TIMU YETU ILI KULETA MATOKEO CHANYA.
Simba hatuhitaji mshambuliaji anayejiona bora kuliko mafanikio ya timu yetu pendwa.
Okwi anazurula huku timu ya Simba ikidhalilika kwa kufungwa na vitimu vidogo kabisa au timu shindani.
Okwi huko aliko anayafurahia haya matokeo mabaya ya timu ya Simba.
Kama asingefurahia matokeo mabovu ya timu yake angefanya bidii kuichezea timu mara nyingi ili kupata matokeo yanayohitajika.
MO mfukuze Okwi kama ulivyomfukuza Amog.
Wapenzi wa Simba hatuna imani naye tena.
Mfukuze Okwi tutafute mshambuliaji mwenye MUDA wa kuichezea timu yetu na kuleta matokeo mazuri.
Okwi baki hukohuko Uganda utatue matatizo yako yote kwa nafasi.
Hatutaki Utapeli wako.
Sisi wadau wa ukweli wa timu ya Simba tumekuelewa.Hiki ndicho nilichookimaanisha mimi kwenye uzi huu, achana na mawazo ya suSzu36
kabisaWacha ugonjwa üwatafune
Wajanja wachache wanatafuna hela ya ponjoro kiulaini kabisa kisha wanasema kikosì ghalì
MCHEZAJI anaeongoza ligi kwa ufungaji wa magoli anapokuwa nje ya uwanja bila sababu za msingi anaiumiza timu na hafai kuchekewa. Hii ni pamoja na Obrey na Ngoma. Hata kama unaidai timu, lakini haimaanishi kuwa usipochezea timu kunapunguza ukubwa wa deni lako, club itakulipa kwa mujibu wa makubaliano na mkataba wako na club hata kama timu itashuka daraja kwasababu yako.Sisi wadau wa ukweli wa timu ya Simba tumekuelewa.
Anachokifanya mchezaji wa Simba Emanueli Okwi ni Fedheha kwa timu.
Okwi anaidhalilisha timu makusudi kabisa.
Hata sifahamu kwanini viongozi wa Simba wako kimya tu.
Labda kawafanya Misukule kama inavyosemekana.
Mimi sina hamu na hicho kirusi Okwi.
UlitabiriWewe vepee! Inaniuma kishenzi aisei, hasa kule timu kufungwa na Green Worriers, Azam na kufukuzwa Omog wakati tuna bonge la mchezaji wetu Okwi ambae huenda angesaidia kuepusha yote haya. Utakiona kitakachotokea tena kwa URA na kombe la Mapinduzi!!
Hahaha, mkuu nilijuwa thimba atatolewa kamasi jembamba na URA kutokana na trend yao iliyopo kwa sasa. Kocha makini anaposema anamtaka mchezaji fulani (Okwi, Chirwa au Ngoma) kwenye kikosi chake ana maana na amemaanisha hivyo, viongozi lazima wafanye kila linalowezekana kumleta huyo mchezaji na kuhakikisha kuwa anapatiwa mazingira mazuri ya kucheza kama kocha atakavyoona inafaa kwa mechi ile. Kwa mfano, kumfukuza Omog bila kutatua tatizo la Okwi kwanza ili aweze kutumiwa na Omog kwenye mechi ni kosa kubwa na sio sawa kwakuwa Omog kumkosa Okwi kwenye mechi ni sawa na Zidane kumkosa Ronaldo kwenye mechi au Barcelona bila Messi, au Man U bila Pogba kwenye mechi. Hapa unaweza kusema Omog ameponzwa na Okwi.Ulitabiri