Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 19,147
- 43,079
Wakuu !
Chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania kilikuja na kauli mbiu yake ya No Reforms No Election baada ya uongozi mpya wa Chama hicho kuingia madarakani ukiongozwa na Mheshimiwa Tundu Lissu na Makamu wake John Heche.
Chama hicho kilianza kutoa msimamo wake kwa kuanza kuzunguka maeneo mbalimbali ya nchi kikitoa ufafanuzi kuhusu maazimio ambayo yalishakubaliwa ndani ya vikao vya Kamati kuu chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wake aliyemaliza muda wake Mheshimiwa Freeman Mbowe. Mikutano yake iliyofanyika Kanda mbalimbali za uongozi wa Chama hicho ilikuwa na mapokeo mazuri na Wananchi waliwapokea na kuwaunga mkono pamoja na changamoto na misukosuko mingi lakini Wananchi somo wamelielewa.
Ukirudi kwenye Chama Cha Mapinduzi, Chama kinachoongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nacho kuelekea Uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 kimekuja na kauli mbiu inayoitwa Oktoba Tunatiki.
No Reforms No Election na Oktoba Tunatiki ni kauli mbiu za vyama vikuu vya siasa hapa nchini, mapokeo ya kauli mbiu hizi kwa Wapiga Kura yamepokelewa kwa njia mbalimbali na kumekuwa na mabishano na mijadala mbalimbali, kuhusu hizi kauli mbiu. Kauli mbiu ya No Reforms No Election imekuwa na nguvu na imeeleweka sana kwa kila Mtanzania pamoja na ugandamizwaji wa Chama kinachosimamia hiyo kauli mbiu hiyo lakini kwenye vichwa vya Watanzania wengi ime click.
Ukirudi kwenye kauli mbiu ya Oktoba Tunatiki bado imekuwa haina ushawishi mkubwa kwa watu na hata mapokeo yake yamekuwa bado hayaeleweki pamoja na nguvu kubwa inayotumiwa na Viongozi wake kwa kushirikiana na watu mbalimbali wenye ushawishi kwenye jamii ( Wasanii, Mashehe na Wachungaji wa Makanisa ya Kiroho) bado kauli hiyo imekuwa kama bado haieleweki kutokana na kile kinachofanyiwa chama kikuu cha upinzani (CHADEMA) na Serikali kwa kushirikiana na Mahakama na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Hali hii imesababisha kuwa na msuguano mkubwa wa chini chini unaoendelea na hata Jumuiya mbalimbali za kimataifa, Mabalozi wawakilishi wa nchi mbalimbali nao wamekuwa na misimamo mikali kuhusu hali ya kisiasa inayoendelea nchini Tanzania.
Uwepo wa hali hii Imesababisha hata yale maandalizi ya kuelekea Uchaguzi mkuu kukosa muamko mkubwa tofauti na miaka mingine ya Uchaguzi iliyopita hasa tukikumbuka mwaka 2015 na mwaka 2010. Chama cha Mapinduzi kimekuwa kinafanya maandalizi yake kwa kukosa ile nguvu au ari kama ile miaka ya nyuma kwa sababu kinapojaribu Kuja na matukio yanayohusiana na uchaguzi lakini kinakutana na ile kauli mbiu ya No Reforms No Election, kauli hii inafanya kupoozesha ile nguvu ya maandalizi ya kuelekea Uchaguzi mkuu.
Kwa upande wa Serikali inayoongozwa na Chama chaMapinduzi kumetokea baadhi ya matukio ambayo yanazua sintofahamu hasa tukio la Makamu wa Raisi kutamka hadharani kwamba anapumzika siasa na akateuliwa mgombea mwenza mwingine Balozi Dr Emanuel Nchimbi na vile vile tamko la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kusema kwamba hatogombea tena Ubunge nalo limeleta sintofahamu kubwa na kabla ya Mh Kassim Majaliwa kutoa tamko hilo tayari mwaka mmoja nyuma Raisi wa JMT alikuwa ameshamteuwa Dr. Ditto Biteko kuwa Makamu Waziri Mkuu.
Pamoja na hayo yote bado kumekuwa kuna sintofahamu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kushiriki kwenye Uchaguzi mkuu mwaka huu, hali ambayo imewaweka njia panda Wapiga kura njia panda.
Wiki mbili hizi nazo kumekuwa kimya sana, haieleweki Raisi wa Tanzania yuko wapi na anafanya nini, Makamu wa Raisi Dr Mpango naye haonekani akifanya kazi kama Msaidizi wa Raisi. Mh Kassim Majaliwa kama Mtendaji Mkuu wa serikali naye amekuwa kimya tangu atangaze kutogombea Ubunge.
Kinachotengeneza headline sasa ni kesi ya Tundu Lissu nayo tunasikia kila baada ya wiki mbili.
Tupo njia panda Wakuu, sijui ni kwa sababu ya huu msuguano wa hizi kauli mbiu za vyama vya CCM na CHADEMA.
Kuna vyama vya ACT WAZALENDO na CHAUMA vinaendelea na harakati zake lakini harakati hizo zimekuwa kama upepo unaopita tu na hazina muitikio mkubwa kama harakati zinazofanywa na vyama vya CCM na CHADEMA.
Wataalamu wa mambo naomba mtoe uchambuzi wenu au maoni yenu kuhusu hali inayoendelea hasa kwa kipindi hiki cha mwezi July.
Niwatakie Ijumaa Kareem
Nawasilisha