Ofisi za Umoja Party

Dp800

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,755
3,608
Amani ya Mungu ipitayo amani zote iwe nanyi wapendwa,

Naomba kujuzwa zinakopatikana ofisi za chama cha Umoja (Umoja Party)

Ninawiwa kushirikiana nao kusukuma mbele gurudumu la kuzijenga upya siasa za taifa la Tanzania.

Nimetafakari na kujihoji na mwisho nimefikia lengo la kutaka kuingia kwenye siasa za Tanzania. Natambua wako kwenye nyakati ngumu za kuzisihi maalaka kuwapa kibali na usajili wa chama, na kwangu naona ndio nyakati sasa za kushirikiana nao.

Maswali yatakuwa mengi kwanini hayo nayotaka kuyafanya nisifanye kwenye vyama vingine vingi vilivopo sasa hivi.

Jibu langu kwayo ni kwamba vyama vilivyopo kwa sasa vyenye dira ya kuongoza nchi ya Tanzania ni viliwi CCM na CHADEMA. Niwaombe radhi wengine ila matendo na maneno yao hayasadifu dhamira zao hata kama wameandika kwenye ilani na sera zao.

Hivyo kwa vyama hivyo viwili nimefanya tafiti zangu na kubaini ya kwamba kwa aina ya watu walioshika hatamu na misingi ya sera zao wanazohubiri(sio zilizoandikwa). Falsafa zao hazina misingi ya kujitegemea kitu ambacho kwangu ni kigezo kikuu cha ushirika wangu.

Hoja yangu nyingine ni kuwa Umoja Party imejinasibisha kufuata misingi ya Rais wa awamu ya tano Dr.Magufuli. Binafsi yangu JPM atabaki kuwa mwamba imara hivyo kwa kulitambua hilo dhamiri yangu ni kushirikiana na wenzangu kutengeneza taasisi imara itakayoweza kuunda na kusimamia vyema Taifa la Tanzania. Pia ni nafasi ya kuitikia wito wa JPM aliuomba kwa watanzania wote Kupitia kitabu cha Ali Mfuruki Tanzania's Industrialisation journey, 2016-2056 wa kushiriki katika kufanikisha maendeleo jumuishi kwa watanzania wote.

Natambua na kufahamu sio kazi rahisi kufikia hayo ninayoyatazamia, Najua kuna dhoruba na ukinzania mkubwa utakao jitokeza lakini nimechagua upande wa matumaini kwamba nitayashinda hayo, mimi pamoja na wenzangu. hivyo kwa yeyote mwenye taarifa za namna naweza kuwafikia hawa ndugu anijuze. Niweze kuungana nao.

Asanteni sana.
 
Utàjipa kazi bila sababu,uliona wapi upepo unatafutwa!
Nenda bondeni ukachume NGOGWE.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom