Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Wazo hill kwa nini mnawauzia fomu za Dawasco wananchi?

Powder

JF-Expert Member
Jan 6, 2016
4,800
6,294
Dawasco wametoa ofa ya kuunganishiwa maji kwa gharama ndogo ya 50,000 Kama sikosei pamoja na mpira Mita 50, wamesambaza fomu zao kwenye ofisi za Serikali ya mtaa Ili wananchi wazipate kwa urahisi, tena wamesema fomu zitatolewa bure, cha ajabu ofisi ya Serikali wa Mtaa wa Wazo hill-Tegeta jijini Dar es salaam, iliyopo pale Magereji ambapo Kuna Gereji za Mafundi Magari, wanauza hizi fomu kwa Sh. 10,000 kwa nini wauze fomu ambazo Wenyewe Dawasco wametaka zigawiwe bure???????
 
Si heri ya huko, pale mapinga shule bagamoyo ukitaka kuunganishiwa maji, inabidi ukachukue fomu serikali ya mtaa ya kuthibitisha km wewe mkazi wa hapo , basi ili wakupe iyo fomu,mashariti yake uende na karatasi ya mauziano ya kiwanja, Kama ulinunua kiwanja letsay milioni kumi, basi ulipie asilimia kumi kwao 10%, ni ujinga kabisa..
 
Mkuu haya malalamiko umeshayawasilisha panapohusika au ndio zile tabia zetu watanzania kujificha nyuma ya keyboard na kuanza kubweka, maana sidhani kama hapa utapata suluhisho ila kama lengo ni kufurahisha baraza yetu , karibu .
 
Duh! Sio fair kabisa, vitu vidogo Kama hivi vinaweka Chuki kwa Raia.
 
Mkuu haya malalamiko umeshayawasilisha panapohusika au ndio zile tabia zetu watanzania kujificha nyuma ya keyboard na kuanza kubweka, maana sidhani kama hapa utapata suluhisho ila kama lengo ni kufurahisha baraza yetu , karibu .
Jamii forums inatembelewa Na watu wengi mkuu! Na imekua chanzo kikubwa cha habari, hujui kuwa Kuna malalamiko mengi yameshatatuliwa kupitia JF?
 
Mkuu haya malalamiko umeshayawasilisha panapohusika au ndio zile tabia zetu watanzania kujificha nyuma ya keyboard na kuanza kubweka, maana sidhani kama hapa utapata suluhisho ila kama lengo ni kufurahisha baraza yetu , karibu .
hujui maana ya jamii forums.
 
hujui maana ya jamii forums.
unadhani hapa tupo kwa ajili ya kufurahishana? jf is the home of great thinkers where we dare to speak openly. kuna watu wengi wameshaachishwa kazi kwa post za humu....na ukitaka ushahidi ntakupa......hata hili limefika na jumatatu utapata mrejesho.
 
Kwa huu ushujaa wa kujificha nyuma ya keyboard , great thinker ...!!?? Unafahamu maana ya hilo neno ama..?? Yaani usiwaulize hao watendaji wa serikali ya mtaa wako unakuja huku kijiweni, you must be kidding kid
 
Si heri ya huko, pale mapinga shule bagamoyo ukitaka kuunganishiwa maji, inabidi ukachukue fomu serikali ya mtaa ya kuthibitisha km wewe mkazi wa hapo , basi ili wakupe iyo fomu,mashariti yake uende na karatasi ya mauziano ya kiwanja, Kama ulinunua kiwanja letsay milioni kumi, basi ulipie asilimia kumi kwao 10%, ni ujinga kabisa..
Mngejiunga mkatoa taarifa panapohusika.
 
Kwa huu ushujaa wa kujificha nyuma ya keyboard , great thinker ...!!?? Unafahamu maana ya hilo neno ama..?? Yaani usiwaulize hao watendaji wa serikali ya mtaa wako unakuja huku kijiweni, you must be kidding kid
Hao Watendaji utawauliza kitu gani wamekwambia fomu zinauzwa? Acha ubishi mkuu, Naweza kwenda Dawasco nikafika reception na kupeleka malalamiko yangu, na muhusika akapuuzia Tu, (inatokea Mara nyingi hasa kwa taasisi za Serikali) lakini nikiweka bandiko hapa, litaonekana mpaka na Manager mpaka na Waziri, Kuna malalamiko mengi yametatuliwa kupitia hapa JF, unataka kusema hujui? Hujawahi kusikia kiongozi wa Uma akiita Waandishi wa habari kujibu tuhuma zilizowekwa JF? Ubishi na Ujuaji usio na maana ni ujinga saa ingine!
 
Watanzania bwana ,yaani kero za mwatendaji wazembe tunataka zitatuliwe kwa kubweka mitandaoni ,tena ya kishambenga,
Swali la kizushi, tangu uweke bango mpaka sasa kuna utatuzi wowote umepatikana
 
Dawasco wametoa ofa ya kuunganishiwa maji kwa gharama ndogo ya 50,000 Kama sikosei pamoja na mpira Mita 50, wamesambaza fomu zao kwenye ofisi za Serikali ya mtaa Ili wananchi wazipate kwa urahisi, tena wamesema fomu zitatolewa bure, cha ajabu ofisi ya Serikali wa Mtaa wa Wazo hill-Tegeta jijini Dar es salaam, iliyopo pale Magereji ambapo Kuna Gereji za Mafundi Magari, wanauza hizi fomu kwa Sh. 10,000 kwa nini wauze fomu ambazo Wenyewe Dawasco wametaka zigawiwe bure???????
Kwanza kabisa Napenda nikanushe habari ya kuwa fomu za dawasco zinauzwa la hashaa...!!
Fomu za dawasco zinatolewa na dawasco wenyewe pale hamna fomu Bali unapewa barua ya utambulisho kuwa wewe ni mkazi wa mtaa ule..!
Hiyo elfu10 unayolipa ni kwa ajili ya matumizi ya office kama umeme kodi ya fremu n. k.
Kwa sababu SERIKALI YA TANZANIA inatoa sh. Elfu 60 kwa mwezi kwa ajili ya office
MCHANGANUO WA PESA ELFU 60
elfu 30=kwa ajili ya kodi ya chumba
Elfu 30=kwa ajili ya matumizi ya kulipa umeme na vitu vya stationary
Sasa basi fremu pale ni elfu 70 kwa mwezi ambayo ni bei ya chini kabisa hapa mjini tena kwa hisani ya mafundi gari umeme elfu 10
Wale viongozi mwenyekiti analipwa elfu 30 kwa mwezi
Wajumbe ni watano kila mmoja analipwa elfu 5 kwa mwezi na halmashauri
Ofisi Ile kila mda watu wamejaa wanaihitaji huduma mtaa ule ni mkubwa kwa wilaya ya kinondoni ni wapili kwa wingi wa watu. Kiasi kwamba inawalazimu Wajumbe wote wawepo pale ili kusaidia kuliko kumuachia mtendaji pekee yake na hadi wameomba mabinti wawili toka chuo cha ustawi wa jamii pale bamaga waje wasaidie.
Huduma zoooote unapata bure isipokuwa hiyo ya maji unachangia kidogo na hiyo ilifanyika kwa makubaliano na wananchi pale uwanja wa panga mwezi wa 5 wewe hukuhudhuria na isitoshe kama huna huwa unapewa Huduma hiyo bure sasa kama unakuja kulalamikia huku unashangaza sana kwa sababu hata pale huwa unaelimishwa kabla ya kutoa hiyo pesa.

SULUHISHO
serikali iharakishe kuukata huo mtaa ili iwepo mitaa miwili au mitatu
Pili iongeze pesa kwa ajili ya ofisi zake za mitaa hasa huku mjini sababu huku kodi ya vyumba ni bei juu. Au ijenge kabisa...!!
 
Back
Top Bottom