Ofisi ya Rais ichukue jukumu la kutoa vibali vya kufanya kazi nchini kwa Wageni wote

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Salaam
Wana jamvi

Kutokana na kutolewa vibali holela vya kufanya kazi nchini kwa wageni hata wale wasiokua na sifa husika katika taasisi husika, Hali hii imepelekea wazawa kukosa fursa ya kufanya kazi stahiki, Wizara ya kazi ndio yenye jukumu hilo lakini naona imeshindwa kubaini sifa za kutoa vibali hivyo aitha kwa kujua ama kwa makusudi kwa wageni nchini, Aidha, utakuta mgeni/mzungu anakibali cha kufanya kazi fulani lakini hafanyi kazi stahili mfano Migodini mfano Buzwagi, Bulyankhulu, Handeni, Mgeni au Mzungu anakibali cha kazi kama Mineral engineer lakini kazi anayofanya ni Ulinzi katika mageti ya kuingia na kutokea, Vilevile utakuta mgeni ana kibali cha kazi kama mshauri lakini kazi anayofanya ni ya management zaidi na uzalishaji.Hivyo basi kutokana na Wizara hiyo kutokua makini hata kukagua vyeti vya taaluma vya wageni hao, hali hiyo ndio inayopelekea hata wananchi wa nchi za Afrika kusini, Msumbiji na nyingine kuweka chuki dhidi ya wageni katika nchi zao baada ya kubaini wingi wa wageni kufanya kazi zinazoweza kufanywa na wananchi wenyewe, ninaomba ofisi ya Rais utawala bora wafanye wachukue mamlaka ya kusimamia, kuhakiki vyeti vya taaluma vya wageni, wawekezaji na kutoa vibali vya kufanya kazi nchini kwa wageni kama watakua na sifa stahili kwa wawekezaji wote ili kujua kama wana sifa za kupewa vibali vya kufanya kazi nchini
 
Nakuunga mkono +100%
Watanzania wengi wamesoma vizuri alafu wanasota mtaani kisa wageni wanapewa fursa kwa kuzingatia rangi zao..

Na makampuni mengi yenye tabia za kuajiri mijitu ya kizungu hayapendi kuajiri ma HR wenye sifa.. Bali wanaokota okota vilaza wa kuburuzwa buruzwa na kugeuzwa geuzwa kama chapati..

Ifike mahali serikali itambue kuwa sekta binafsi ni mwajiri namba moja kwa wazawa wa nchi hii.. Inahitaji kuangaliwa kama mboni ya jicho!
 
Tunazungukwa sana na hawa wageni kwa kutojua haki zetu na wapi pa kusimamia. Au tunaweka mwanya wa kesho nipate pa kumuweka ndugu yangu bila kuangalia maslahi ya wengi.
Mambo kama haya yanasababisha watanzania wengi kukosa nafasi za ajira pale inapogitajika na nafasi hizo kujazwa na wageni kinyume na taratibu za ajira
 
Naunga mkono wazo lako, vibali vya kazi vitolewe na ofisi ya rais utumishi wakishirikiana na wizara ya elimu, kimsingi taaluma zao ndio zinawapa sifa ya kufanyakazi nchini na wizara ya elimu na ufundi ndio wenye taaluma ya kubaini vyeti stahiki.

Kwa wenye degree vyeti vyao lazima vihakikiwe na tcu na wenye diploma vihakikiwe nacte.

Utakuta mzungu ana diploma ya wiki mbili kama production manager wakati mzawa anaambiwa lazima awe na masters na uzoefu usiopungua miaka kumi.
 
Back
Top Bottom