Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Longido yakanusha taarifa ya wananchi kubadilisha ng'ombe kwa mahindi

Kisu Cha Ngariba

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
22,135
48,821
Taarifa: Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Longido yakanusha taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la Mwananchi kuhusu uwepo wa njaa wilayani humo.
e102d6ff49d3cc702b83eacdb91ba6bc.jpg
efcf78feacef44f9ca8f6f416e5c6046.jpg
 
Yulsq mwingine alisema wauze ng'ombe kwa debe la maize
 
Katika sehemu ambayo ina ukame wa muda mrefu ni Longido.

Nimepita mara kadhaa mwaka jana na mwaka huu,hali ya Longido ni mbaya.

Mifugo ukiitazama mpaka inakatisha tamaa..

Anyway wenyewe wameshasema HAKUNA NJAA.
 
Taarifa: Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Longido yakanusha taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la Mwananchi kuhusu uwepo wa njaa wilayani humo.
e102d6ff49d3cc702b83eacdb91ba6bc.jpg
efcf78feacef44f9ca8f6f416e5c6046.jpg


Ni afadhali kukaa kimya kama unaogopa kupinganana wakubwa zako kuliko fedheha ya kukanusha halafu baadaye inakuja kuwa ni kweli.

I hope haiko namna hii.
 
mwananchi wanaanza kujisogeza wenyewe kwenye kisu.... kikiwakata wataanza kulia,,,
 
Ni vyema kwani ameipunguzia Serikali mzigo wa kutoa chakula either kwa msaada au kiuzwe kwa bei nafuu kwa wananchi wa Longido.

Hongera sana Chongolo kwa kutoa ufafanuzi mzuri lakini isije kuwagharimu wananchi wa longido baadaye kwani mkipeleka ombi la msaada kuhusu chakula mkikataliwa msije laumu Serikali kuwa haiwatendei haki.

Kwa mkoa kama DSM ni kweli hauna mashamba na ukiona mazao ni vibustani tu mtu kalima mahindi ya kuchoma yeye na familiya yake. Huku wananchi tunaishi kwa kutegemea Soko la Tandale na pesa yako tu, lakini mikoani asilimia kubwa wanaishi zaidi kutegemea kilimo.

Na kutokana na ukame inabidi tukubali kuwa hata hao ng'ombe hawauziki kutokana na afya zao. ni nani mwenye kununua ng'ombe anayehesabika mifupa?????


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!
 
Huyu ni Daniel Chongolo,kabla ya kuwa DC wa Longido alikuwa pale Lumumba kama Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano.Huyu anajua vizuri ile mashine ya Bulgaria ya kuchapisha magazeti ya Uhuru ilivyouzwa kama chuma chakavu.

Nasikitika Chongolo anasema Longido 95% watu wananunua chakula,kwa hiyo sio ajabu.Lakini hataki kujua kuwa sbb ya ukame hata hao wakulima wanaowauzia wafugaji hawatakuwa na chakula sbb ya ukame hivyo watabadilishana tu na mifugo.

Huyu DC mbona anashindwa kuweka logic!!Sasa kama huko Njombe wakulima hununua nyama kwa wafugaji,kama hiyo mifugo ikifa kwa ukame na nyama kuwa adimu maanake si itabdi mkulima mpenda nyama awe anabasilishana mahindi na nyama?Na hapo ndio inatokea Longido ila hawataki kusema tu
 
Taarifa: Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Longido yakanusha taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la Mwananchi kuhusu uwepo wa njaa wilayani humo.
e102d6ff49d3cc702b83eacdb91ba6bc.jpg
efcf78feacef44f9ca8f6f416e5c6046.jpg
Hao wanaodaiwa kubadilisha ndio pekee wanaoweza kulikubali ama kulikataa na siyo mkuu wa wilaya. Kama walibadili itaendelea kuwa kweli tu hata kama mkuu wa wilaya atajitoa ufahamu namna hiyo.
 
Wakuu wa wilaya wanatetea matumbo yao badala ya wananchi wanawaowaongoza!!
 
Unajua kukataa ukweli ambao wananchi wanaujua na wanaona hali waliyo nayo ni dhambi ya kujitakia kwa viongozi wetu
 
Wahenga walisema "Mficha maradhi mwisho kifo humuumbua" hawakukosea kwa falsafa hii.
Wakuu waamejifunza kuimba wimbo wa mwenye nyumba wanaitikia koras vema kabisa hivo watadumu kama wapangaji chezea mwenye nyumba wewe!
 
Mimi sidhani mkuu wa wilaya katumia busara kwenye maelezo ya njaa Longido. Hata km muda mwingi kuna ukame lkn inapotokea maeneo mengi ya nchi yanaukame n mahindi sio mengi lzm wananchi hawa watapata shida kubwa. Mahindi itabidi wayapate kwa bei kubwa. Wakati huo huo ukame huo ng'ombe wao wanakosa nyasi n kupelekea kufa n kupata bei ya chini. Hivi sass bei ya gunia moja Arusha n moshi ni 120000 n upatikane wake wa shida. Je, gunia hilo likifika longido litakuwa n bei gani? Hela ya kununua watapata wp n mifugo imedhoofika? Nilimsikia mkuu wa kaya akisema uzeni ng'ombe. Hivi hili soko la ng'ombe hawa waliokonda liko wapi la kuuza? Karibu mikoa yote kuna ukame n mufugo imeathirika. Wananchi wenyewe uchumi mbaya , nyama kwenye mabucha zinalala. Mabucha mengi yamefungwa. Hebu viongozi wetu wafikiri kwa kichwa n kwakina. Hili ni janga kubwa
 
Back
Top Bottom