dm2000inter
Member
- Oct 27, 2010
- 29
- 10
Mwaka 2012 ofisi ya DPP ili enter nolle prosequi katika kesi ya mauaji inayowakabili matajiri wanne wa Jijini Mwanza wakiongozwa na John Joseph Kisoka maarufu kwa jina la "Magazeti" baada ya kesi hiyo kukosa nguvu kwa vile matajiri hao ambao ndio key suspect walikuwa hawajakamatwa.
Baada ya kesi matajiri hao wakarejea nchini na kuendelea na biashara zao kama kawaida. Ndugu wa marehemu wakalalamika ofisi mbalimbali za umma wakitaka polisi wawakamate watuhumiwa hao bila mafanikio. Badala yake, original file la uchunguzi likiwa na maelezo ya mashahidi likaibwa kimafya katika ofisi ya RCO Kilimanjaro ili kesi hiyo isifufuliwe.
Mwaka jana Ndugu wa marehemu baada ya kuhangaika sqna wakamwandikia barua Rais Kikwete aingilie kati lakini hadi anaondoka madarakani hata kuwajibu ndugu wa marehemu hakuwajibu. Ndugu wakamwandikia barua Rais JPM mara tu alipoingia madarakani. Haikupita wiki DCI Diwani Athman akaunda kikosi kazi kikiongozwa na ACP Charles Kenyela akisaidiwa na SSP Ralph Meela kuanzisha uchunguzi wa suala hilo upya.
Kikosi hicho kilifanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kupata ushahidi mzito dhidi ya matajiri hao. Kikubwa, walifanikiwa kupata original report ya postmoterm baada ya ile iliyokuwepo awali katika jalada lililoibwa kuwa imegushiwa. DCI akapeleka jalada hilo kwa DPP tangu Januari 20 mwaka huu hadi leo hajatoa maamuzi ya watuhumiwa kufikishwa kortini. Badala yake anaibua visingizio kibao akihoji mbona eti baadhi ya mashahidi ni wapya.
DPP anasahau kuwa ni ofisi hiyo hiyo iliyoiondoa kesi hiyo kwa Nolle Prosequi mwaka 2012 leo wanaletewa ushahidi wanaanza kushikwa na kigugumizi. Kigugumizi hiki kimeibua maswali mengi hasa baada ya kuwepo kwa minong'ono ya kutengwa sh100,000,000 ili kesi hiyo imalizikie ofisi ya DPP.
Kwa yanayoendelea, hata kama rupia haijawapitia baadhi ya wasaidizi wake lakini kigugumizi hiki kinaweza kuifanya jamii iamini kuna agenda ya siri na jalada hilo.
DPP anapaswa kusoma alama za nyakati baada ya kauli ile ya Rais JPM wakati wa Law Day alipoinyooshea kidole ofisi hiyo. Kauli ya Rais inaashiria kuna jambo katika utendaji wa ofisi hiyo. Chombo pekee cha utoaji haki ni mahakama, ofisi hiyo isigeuke kuwa kikwazo cha wananchi kuheshimu utawala wa sheria.
Rais JPM na Waziri Mwakyembe wanatakiwa wachukue hatua kurejesha imani ya watanza katika utendaji wa ofisi hii ya umma.