Ofisi ya Auditor General hoi

Ofisi ya Auditor General hoi

Gor

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
2,791
Reaction score
850
Serikali imeaza kuichezea ofisi ya audit general kwa kutoa fedha kiduchu kwa mradi wa kazi ya ukaguzi wa ofisi hii muhimu kuliko ofisi yoyote katika nchi hii.

Katika kipindi cha mwaka 2014 - 2015 ofisi hii imepata 60% tu ya budget yake.Tabia hii inatokea baada ya aliyekuwa Auditor General kustaafu ndg.Utouh.

Wafuatiliaji wanasema hii ni hatari sana kwani inaonekana AG ananyimwa fedha ili asiende field kwani ofisi hii ipo kwa mujibu wa sheria na ni hatari kwa usalama wa nchi endapo ofisi hii ambayo ndio macho ya bunge letu kutokuwa na fedha.

Serikali hii ya CCM wanatumia kila njia kunyamazisha vyombo vinakuza uwajibikaji na uwazi kwenye nchi maana kwao TUNU hizo ni gonjwa hatari la ebola.
 
Ni ofisi ipi katika serikali yetu iliwahi kupata 100% ya initial budget? Labda ofisi ya raisi pekee, the rest ni 10-60% kutegemeana na umuhimu wake.
 
Ofisi hiyo imejidhalilisha yenyewe kwa kuacha kusimamia ukweli. Unakumbuka yule acting CAG wakati wa escrow aliishia wapi? Huyu aliyeingia, nadhani kwa woga wake, akaamua kiogopa serikali. Si aliambiwa aendelee kuchunguza escrow? ripoti yake ya mwisho iko wapi? (au ndiyo iliwasafisha akina muhongo). Hata ukisoma ripoti ya CAG iliyopelekwa bungeni utaona iko shallow sana ukilinganisha na za nyuma.
 
Kuiweka ofice ya cag ndani ya serikali kuu ndio tatizo, ilitakiwa iwe huru ijitenge kama mashirika ya umma.

Ndio maana wakaguzi ni wezi sana maana hawalipwi mshahara mzuri,hawana marupu rupu kama watumishi wa mashirika ya serikali.
 
jamani watz hii ofisi tukiitelekeza hawa mafisi wa ccm wakaikalia basi tugawane mbao tu.
 
Ni ofisi ipi katika serikali yetu iliwahi kupata 100% ya initial budget? Labda ofisi ya raisi pekee, the rest ni 10-60% kutegemeana na umuhimu wake.
Well said! Ofisi yetu, nijapofanya kazi mimi mpaka mwaka wa fedha unaisha, tulikuwa tumetumia asilimia 34.5% ya bajeti ya ofisi ambayo ilikuwa Tzs.42 Million hivi.
Serikalo ya CCM imechoka kikweli kweli mpaka aibu, fedha zipo mikononi mwa mafisadi kama akina Change na wenzao.
 
Gor

Mie mbona niko ofisi ya CAG siyaoni haya uliyo sema? bajeti yetu tunapewa kwa ukamilifu.
 
Last edited by a moderator:
well said! Ofisi yetu, nijapofanya kazi mimi mpaka mwaka wa fedha unaisha, tulikuwa tumetumia asilimia 34.5% ya bajeti ya ofisi ambayo ilikuwa tzs.42 million hivi.
Serikalo ya ccm imechoka kikweli kweli mpaka aibu, fedha zipo mikononi mwa mafisadi kama akina change na wenzao.
umeona wanakiri wenyewe.....tuna pata habari za ndani penda msipende....hii nchi sio ya mkwere tu.
 
Serikali imeaza kuichezea ofisi ya audit general kwa kutoa fedha kiduchu kwa mradi wa kazi ya ukaguzi wa ofisi hii muhimu kuliko ofisi yoyote katika nchi hii.

Katika kipindi cha mwaka 2014 - 2015 ofisi hii imepata 60% tu ya budget yake.Tabia hii inatokea baada ya aliyekuwa Auditor General kustaafu ndg.Utouh.

Wafuatiliaji wanasema hii ni hatari sana kwani inaonekana AG ananyimwa fedha ili asiende field kwani ofisi hii ipo kwa mujibu wa sheria na ni hatari kwa usalama wa nchi endapo ofisi hii ambayo ndio macho ya bunge letu kutokuwa na fedha.

Serikali hii ya CCM wanatumia kila njia kunyamazisha vyombo vinakuza uwajibikaji na uwazi kwenye nchi maana kwao TUNU hizo ni gonjwa hatari la ebola.
naona kinyesi tu hapo nilipo weka red. hivi kama sio Kikwete na ccm yake huo uwazi wa CAG ungeufahamu?
 
naona kinyesi tu hapo nilipo weka red. Hivi kama sio kikwete na ccm yake huo uwazi wa cag ungeufahamu?
...kinyesi sawa but ukweli mchungu kwani hii serikali ya mama yako au baba yako au ya ukoo wenu? Sema si ya ccm?.
 
Napata wasiwasi ofisi gani iyo ambayo imepokea mil 42 mwaka mzima,kwa maana iyo approved budget yenu haizidi mil 150,hii ni buget ya ofisi au ?mmmh sasa mkuu hii ni recurrent au dev?
Well said! Ofisi yetu, nijapofanya kazi mimi mpaka mwaka wa fedha unaisha, tulikuwa tumetumia asilimia 34.5% ya bajeti ya ofisi ambayo ilikuwa Tzs.42 Million hivi.
Serikalo ya CCM imechoka kikweli kweli mpaka aibu, fedha zipo mikononi mwa mafisadi kama akina Change na wenzao.
 
Katika ofisi ambazo zinakusanya pesa nyingi kutoka kwa wateja wake hii ni mojawapo. KUna taasisi ndogo tu ya serikali ninayoijua na wakienda kukagua mahesabua ambayo huwachukua takribani wiki 3 na idadi yao huwa watu kama 4 huwalipisha milioni 20 na zaidi. Sasa huko kwingine kwenye maofisi makubwa ya serikali wana-charge kiasi gani? Hawa watu wana mahela mengi sana tu. labda kama hizo pesa huwa zinaingia kwenye kapu la serikali kuu ndo wagawiwe, lakini kama wanaingiza kwenye kapu lao hawa watu ni matajiri sana tu. Ila wanamatumizi ya kufuru. Kwa mfano unakuta tu stationeries budget ya mkurungezi mmoja inafikia hadi milioni 200 kwa mwaka totally unrealistic.
 
Ni ofisi ipi katika serikali yetu iliwahi kupata 100% ya initial budget? Labda ofisi ya raisi pekee, the rest ni 10-60% kutegemeana na umuhimu wake.
Unajiuliza mwenyewe kisha unajijibu mwenyewe.
 
Napata wasiwasi ofisi gani iyo ambayo imepokea mil 42 mwaka mzima,kwa maana iyo approved budget yenu haizidi mil 150,hii ni buget ya ofisi au ?mmmh sasa mkuu hii ni recurrent au dev?
Recurrent mkuu, ofisi yetu inapewa budget ya Recurrent tu.
Na huo ndiyo ukweli. Ofisi za serikali zipo vibaya kuliko watu wanavyozitazama huko nje.
Mwaka huu Approve budget ya ofisi ni takribani 100M. Sijui tunakoelekea. Wizara ya fedha inaelekea iko hoi mbaya.
 
Back
Top Bottom