kALEnga kidamali
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 542
- 735
Serikali imetangaza kuanzia June 2 hadi 4, 2017 Watanzania wataingia bure katika Mbuga na Hifadhi za Wanyama nchini kote ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Tanzania ambayo yatafanyika kitaifa Butiama mkoani Mara.
Waziri wa Mazingira na Muungano January Makamba amesema tayari utaratibu umeshafuatwa ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na TANAPA kuwa katika siku hizo tatu Watanzania wataingia bure katika Mbuga na Hifadhi za Wanyama.
Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani kitaifa yanatarajiwa kufanyika June 5 mwaka huu Butiama Mkoani Mara huku kukitarajiwa kuwa na mijadala mbalimbali itakayojadiliwa kuhusu utunzaji wa mazingira.
Akizungumza na wanahabari jana, waziri wa wizara hiyo, January Makamba alisema lengo la kupeleka maadhimisho hayo Butiama ni kumuenzi Nyerere ambaye alikuwa mwanamazingira namba moja nchini sanjari na kukumbuka mchango wake katika masuala ya uhifadhi wa mazingira nchini.
Kwa mujibu wa Makamba ambaye ni Mbunge wa Bumbuli Mkoani Tanga, kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu nchini ni utunzaji wa mazingira na maendeleo ya viwanda.
======================
Kalenga kidamali