Sexer
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 8,504
- 8,253
Mbunge wa Nyamagana bw. Ezekiel Wenje akishirikiana na wabunge wa chama cha ODM nchini Kenya wamechangia mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuvisaidia vikundi vya wafanyabiashara wadogo, vikiwemo vya akina mama na wamachinga.
Harambee hiyo pia ilichangiwa na waziri mkuu mstaafu wa Kenya ambaye pia ni kiongozi wa ODM Bw. Raila Odinga ambaye alitoa shilingi milioni 2 katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye mkutano wa hadhara viwanja vya shule ya msingi Mbugani jijini Mwanza ambapo zaidi ya shilingi milioni 21 zilichangwa.
Katika mkutano huo bwana Wenje alichangia shilingi milioni 7, mbunge wa Narienda nchini Kenya bw. Nicholaus Gumbo alichangia milioni 3, mbunge wa Homabay nchini Kenya bw. Peter Kaluma alitoa milioni 2, huku michango ya wananchi wengine ikifika milioni 3, huku milioni 4 zikiahidiwa.
Wabunge wa Kenya walisema serikali ya Tanzania inapaswa kufuata misingi na uwajibikaji aliokuwa nao baba wa Taifa, marehemu Mwalimu Nyerere ili iweze kuwanusuru wananchi na umasikini.
"Sisi wakenya tunashangaa nchi hii ya nyerere kuwa na wanachi masikini wakati mna kila kitu, kiongozi mzuri lazima ajali wananchi wake, Hongera sana kamanda wenje na wananchi tunawaomba muendelee kumchagua huyu wenje" alisema bw. Kaluma.