Obama atembelea Makumbusho ya Bob Marley

Ambiente Guru

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Posts
2,623
Reaction score
1,096
Rais Obama yupo Jamaica na ametembelea jumba aliloishi mwanamuziki wa Reggae - Bob Marley.

Ameseme alikuwa mshabiki wa nguli huyo wa mziki na amehifadhi albam zake zote.

Rais wa mwisho kutembelea nchi hiyo ni Renald Regan 1982.

Chanzo: BBC
 
NAJUA NI MSHIRIKA MWENZETU
WA ILE SAKRAMENTI
:mvutaji:
 
Kumbe hakutania aliposema alishawahi kupata jani aka kijiji! Naona kenda kumbushia enzi kenda pasha kiporo
 
Kichaa hata baada ya kupona akiona jalala lazima atamani kukumbushia.
 
Bob Marley ni legend na mpaka sasa mziki wake unapigwa na unasikilizwa,
Na utaendelea kuwepo na kuwepo
 
Bob alikuwa ni mwanamapinduzi kimziki. ( Musical Revolutionary). Wanamapinduzi walikuwa na wataendelea kuwa wafuasi wake. Ndiyo maana alikuwa kati wa watu waliokaribishwa kwenye sherehe za uhuru wa Zimbabwe. Pia alitunikiwa nishani ya Amani na umoja wa Mataifa.

Hivyo unapo muongelea Bob unatakiwa ufikilie ''nje ya boksi'' ndo utauona mchango wake. Hivyo Oboma kilichompeleka hapo ni mchamgo wa Bob kama mwanamapinduzi.
 
Mzee wa magogoni chemka wahi nenda katembelee kabla hela ya bure hsijaditishwa October.
 
Watu wamechukulia kimzaha na sehemu ndogo ya kutumia bange,na kusahau mchango mkubwa wa Bob katika harakati za kumkomboa mtu mweusi katika bara la mabepari na wanyonyaji.mf."Buffalo soldier" na "Babylon must fall" etc etc
Sina hakika na theme ambayo wachangiaji wengi wame major kama inakidhi haja kwa GT wa jf
 
Mpwa =mshana jr Kumbe hakutania aliposema alishawahi kupata jani aka kijiji! Naona kenda kumbushia enzi kenda pasha kiporo


Kijiti asikudanganye mtu kua ameacha kataa mpwa hakiachiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…