Obama, Arusha ni Salama Kabisa

Obama, Arusha ni Salama Kabisa

Filipo Lubua

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2011
Posts
339
Reaction score
579
Wadau,

Nimeshangazwa sana na habari kuwa Rais Obama amefuta ziara zake katika mbuga za Serengeti na Mikumi, eti kwa sababu za kiusalama. Nikizungumzia zaidi safari za Serengeti, pamoja na mikutano mikubwa ya kimataifa ambayo ingefanyika Jijini Arusha, ni wazi kwamba jiji hilo limekosa mapato mengi sana.

Kinachoniumiza zaidi, kama mkazi wa jiji la Arusha, ni ukweli kwamba hali ya usalama jijini Arusha, ambayo leo inatwayo tete na serikali yetu, imesababishwa na serikali hiyo hiyo. Jiji la Arusha ni jiji lenye usalama wa hali ya juu, kuliko hata Dar es Salaam. Jiji hili limekuwa mwenyeji wa mikutano mingi sana ya kimataifa. Kwa Tanzania yetu, hili ni jiji ambalo lina hadhi ya 'an International City' na hilo lina maana zaidi kutokana na jina lake la "Geneva of Africa". Jiji hili ni makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na ni jiji lenye mahakama ya kimataifa ishughulikiayo kesi za mauaji ya kimbari ya Rwanda, pamoja na mengine yafananayo na hayo.

Hali tete ya usalama jijini humo, imesababishwa na serikali yenyewe. Ni wazi kuwa katika fujo zote zilizowahi kutokea jijini humo, hakuna mtu hata mmoja ambaye alikufa kwa kupigwa mapanga na wananchi. Hata Kiongozi wa Chadema kule Usa River, aliyekufa kwa kuchinjwa siku chache baada ya uchaguzi mdogo wa Arumeru, imeshathibitika kuwa alichinjwa na watu waliotumwa na viongozi wa CCM, akiwepo mwenyekiti wa Kijiji. Zaidi sana ni Jeshi la Polisi lililohusika katika mauaji ya Arusha na maeneo mengine nchini, ikiwepo Morogoro na Iringa. Mauaji ya Januari 2011 yote yalisababishwa na Jeshi la Polisi. Mlipuko wa bomu katika mkutano wa Chadema wiki chache zilizopita ulifanywa na jeshi la polisi (kulingana na mashuhuda wa tukio hilo, ambao walijeruhiwa). Fujo nyingi za kisiasa zitokeazo jijini Arusha zimekuwa zikisababishwa na serikali kupitia Jeshi la Polisi.

Obama anatakiwa ajue kuwa, jiji hili ni salama kabisa ikiwa serikali inayoongozwa na mwenyeji wake, Kikwete, haitapiga mabomu tena. Wasiwasi wote wa kiusalama hapa jijini Arusha ni wasiwasi wa maofisa usalama wa Marekani dhidi ya hujuma za serikali mwenyeji. Wananchi wa Arusha ni wastaarabu, ni wapole, wapenda amani na wenye mshikamano.

Obama, nenda Serengeti ukajionee uzuri wa Tanzania. Arusha iko salama kabisa, kama Rais Kikwete atawaambia askari wake wasilipue mabomu na kupiga risasi. Japokuwa tunajua kuwa hamu yako kubwa ni kupata nafasi ya kupora madini na gesi yetu, ni lazima ujue kuwa ziara yako Tanzania haitafana kama hutakwenda kuiona Ngorongoro Crater, mojawapo ya maajabu ya dunia; kama hutakwenda kuiona Serengeti. Ziara yako haitafana ikiwa hutakwenda huko Kaskazini na kuuona Mlima Kilimanjaro pamoja na Mlima Meru. Ukirudi Marekani utawasimulia nini wananchi wako ikiwa hutakuwa umeuona Mlima mrefu kuliko yote Afrika?
 
Obama ulinzi wake ni mkubwa kuliko sema kuna maeneo ame target kufika hao kk wanamalengo marefu

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Obama hajui kuwa Serengeti ni nchi nyingine ndani ya Tanzania?
Ile ni Nchi ya Falme za Kiarabu ina bendera zake na vyombo vya mawasiliano
 

[TD="bgcolor: #ffffff"]MADHARA ya vurugu za kisiasa mkoani Arusha zinazodaiwa kusababishwa na polisi kukabiliana na wafuasi wa vyama vya upinzani, zimesababisha pigo kubwa kiuchumi katika ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama, Tanzania Daima Jumapili limebaini.
Pigo hilo ambalo limesababisha serikali na mahoteli ya kitalii mkoani humo kukosa mabilioni ya fedha, limetokana na hatua ya rais huyo na ujumbe wake kufuta ziara yake kwenye mbunga za wanyama za Serengeti na Mikumi.
Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni pigo kwa serikali ambayo ilitarajia kuingiza mabilioni ya fedha baada ya rais huyo maarufu duniani na ujumbe wake wa watu 700, kuzuru kwenye hifadhi hizo za taifa.
Rais Obama ambaye alianza ziara yake barani Afrika nchini Senegal, alipata fursa ya kutembelea sehemu za utalii na hata alipokuwa nchini Afrika Kusini, alitembelea sehemu ya utalii, hususan gereza alilopata kufungwa Rais wa kwanza mweusi wa nchi hiyo, mzee Nelson Mandela, ambaye kwa sasa yu mahututi.
Habari kutoka ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa zilisema Rais Obama ambaye anatarajiwa kuwasili kesho nchini, akitokea nchini Afrika Kusini, amefuta ziara hizo kwa sababu za kiusalama, hususan hali tete iliyoko mkoani Arusha.
Kwa mujibu wa habari hizo, hali tete ya Arusha, imesababisha mikutano mingine mikubwa ya kimataifa kufanyika jijini Dar es Salaam.
Jiji la Dar es Salaam linatarajiwa kuwa na wageni 2,700, wakiwamo wajumbe 800 kutoka nchi mbalimbali duniani, wanaohudhuria mkutano wa Majadiliano ya Kimataifa kwa Manufaa ya Wote (ISPD), 2013. Mkutano huo unafanyika katika ukumbi mpya wa kisasa wa Mwalimu Nyerere. Umewahusisha marais tisa, marais wastaafu watano na wakuu wa serikali.
Mbali ya ujio wa Rais Obama na ujumbe wake wa watu 700, serikali pia inatarajia kupokea wajumbe wengine wa mkutano wa wake za marais barani Afrika. Mikutano yote hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maofisa wa wizara hiyo ambao waliomba majina yao yahifadhiwe, waliliambia gazeti hili kuwa, katika hali ya kawaida mikutano hiyo ingefanyika mjini Arusha ambako kuna hali ya hewa ya baridi inayofanana sana na maeneo waliyotoka wageni wengi.
Wameeleza kuwa mandhari na ufinyu wa Jiji la Dar es Salaam kumeifanya serikali mara nyingi kufanya mikutano mikubwa ya kimataifa jijini Arusha ambako pia kuna hifadhi za utalii.
“Haya ni madhara ya kucheza na amani, hatutaki kunyoshea kidole mtu yeyote, lakini sote tunahusika katika hali hiyo. Tunaweza kuilaumu serikali, polisi na vyama vya siasa, lakini ni sote,” alisema mmoja wa viongozi wa wizara hiyo.
Akizungumzia kufutwa kwa ziara ya Rais Obama kwenye hifadhi za taifa, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, alisema Rais Obama hakuwa na mpango wa kwenda Serengeti bali alitaka kwenda Mikumi.
“Ni kweli amefuta ziara ya kwenda Mikumi, lakini hakuwa na mpango wa kwenda Serengeti na si kwa sababu za kiusalama,” alisema Waziri Kagasheki.
Matukio makubwa ya milipuko ya mabomu iliyotokea hivi karibuni mkoani Arusha, moja katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasikiti na jingine kwenye mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), huku polisi ikishindwa kuwanasa watuhumiwa, yameitia doa serikali ya Rais Jakaya Kikwete.
Katika mlipuko wa bomu la hivi karibuni katika mkutano wa hadhara wa CHADEMA, zaidi ya watu wanne wamepoteza maisha huku mawaziri wa serikali wakionekana dhahiri kuinyoshea kidole CHADEMA, huku CHADEMA wakiinyoshea kidole serikali na Chama chake Cha Mapinduzi (CCM) kwamba wanahusika.
Kishindo cha ujio wake kesho
Ukiachia kasoro hiyo, maandalizi ya ujio wa rais huyo yamekamilika.
Rais Obama, anatarajiwa kutua kesho saa 8:40 mchana, huku maofisa wa Marekani wakilazimika kushika majukumu yote katika uwanja huo, ikiwamo kuongoza ndege, ukaguzi wa abiria na mizigo.
Kazi ya kuongoza ndege ambayo kwa kawaida hufanywa na Mamlaka ya Anga Tanzania (TAA), kesho kazi hiyo itasimamiwa na Wamarekani wenyewe.
Hata idadi ya maofisa wa Tanzania wakiwamo viongozi watakaompokea Rais Obama siku hiyo pia itapangwa na Wamarekani wenyewe.
Wakati huduma ya zimamoto ikiwa inahitajika zaidi wakati ndege inapotua au kupaa, maofisa wa usalama wa Marekani wamekataa kutumia zimamoto wa Tanzania.
Tayari magari 150 ya msafara wa ziara yake yamewasili nchini, huku serikali kwa kushirikiana na makachero wa Marekani wakifanya mchujo wa majina machache ya mawaziri watakaoruhusiwa kumpokea kiongozi huyo maarufu zaidi duniani.
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Moses Malaki, aliliambia gazeti hili jana kuwa matayarisho ya ujio wa rais huyo hayajapata kutokea nchini.
Tanzania Daima Jumapili ambayo jana ilikuwa ikipita katika maeneo mbalimbali ambayo Rais huyo atapita, imeshuhudia kuwapo kwa ukaguzi wa hali ya juu ukifanywa na makachero wa Marekani katika kuimarisha ulinzi.
Wamarekani wameamua kufanya kila kitu wenyewe, kwa kuwa hawamwamini mtu yeyote, wakiwamo maofisa usalama wa Tanzania.
“Mazoezi haya yatatoa picha rasmi ya jinsi rais huyo atakavyotua, wapi bendi ikae, wapi maofisa wasimame, wapokeaji na msafara wake mzima,” alisema.
Kinachoendelea ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere ni mazoezi ya kumpokea Rais Obama, hususan jinsi watu wanavyotakiwa kujipanga.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema wakati huu wa ujio wa Obama ulinzi ni mkali na wa kutisha kwa wahalifu.
Alisema mtandao mkubwa wa askari umeshawekwa tayari barabarani kuhakikisha kila kitu kinakwenda kama ilivyopangwa hadi siku ya tukio lenyewe ambayo ni kesho.
Mitaani ni Obama, Obama
Kila mtaa au kundi la watu unalokutana nalo jijini Dar es Salaam, mazungumzo ni Rais Obama na ujio wake, hususan maandalizi yanayofanywa.
Wafanyabiashara ndogondogo ndio waathirika wakubwa wa ziara hiyo ambao wengi waliozungumza na gazeti hili wamesema pasipo kumng’unya maneno kwamba wamekerwa na ziara hiyo.
Wapo wananchi hasa waliojiajiri ambao wamepanga kutofika katikati ya jiji kesho kuendelea na shughuli zao kwa hofu ya kuwapo vurugu hasa za msongamano wa magari kwani baadhi ya barabara zitafungwa kabisa.
Mandela afunika ziara ya Obama
Kutoka nchini Afrika Kusini, inaelezwa kuwa ziara ya Rais Obama imefunikwa na hali mbaya ya afya ya Rais mstaafu wa nchi hiyo, Nelson Mandela.
Maelfu ya wananchi wa taifa hilo wameendelea kufurika katika hospitali anakoendelea kupata matibabu mjini Pretoria na kuweka kando ujio wa Rais Obama


[TD="bgcolor: #ffffff"]
Afuta ziara kwenye mbunga za wanyama za Mikumi, Serengeti

na Martin Malera


[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #ffffff"][/TD]
[/TD]
source: tz. daima
 
Kusingizia? Ahh wapi mnataka kumteka Obama? Janja yenu imejulikana magaidi wakubwa nyie....CDM nyie majanga

Huyu sio mtanzania kama mtz basi pandikizi huwezi kuwa na maoni ya namna hii kama una nia njema na Tanzania kwa ujumla yakiwemo maeneo ambayo ccm inakubalika kuliko cdm.
 

[TD="bgcolor: #ffffff"]MADHARA ya vurugu za kisiasa mkoani Arusha zinazodaiwa kusababishwa na polisi kukabiliana na wafuasi wa vyama vya upinzani, zimesababisha pigo kubwa kiuchumi katika ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama, Tanzania Daima Jumapili limebaini.
Pigo hilo ambalo limesababisha serikali na mahoteli ya kitalii mkoani humo kukosa mabilioni ya fedha, limetokana na hatua ya rais huyo na ujumbe wake kufuta ziara yake kwenye mbunga za wanyama za Serengeti na Mikumi.
Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni pigo kwa serikali ambayo ilitarajia kuingiza mabilioni ya fedha baada ya rais huyo maarufu duniani na ujumbe wake wa watu 700, kuzuru kwenye hifadhi hizo za taifa.
Rais Obama ambaye alianza ziara yake barani Afrika nchini Senegal, alipata fursa ya kutembelea sehemu za utalii na hata alipokuwa nchini Afrika Kusini, alitembelea sehemu ya utalii, hususan gereza alilopata kufungwa Rais wa kwanza mweusi wa nchi hiyo, mzee Nelson Mandela, ambaye kwa sasa yu mahututi.
Habari kutoka ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa zilisema Rais Obama ambaye anatarajiwa kuwasili kesho nchini, akitokea nchini Afrika Kusini, amefuta ziara hizo kwa sababu za kiusalama, hususan hali tete iliyoko mkoani Arusha.
Kwa mujibu wa habari hizo, hali tete ya Arusha, imesababisha mikutano mingine mikubwa ya kimataifa kufanyika jijini Dar es Salaam.
Jiji la Dar es Salaam linatarajiwa kuwa na wageni 2,700, wakiwamo wajumbe 800 kutoka nchi mbalimbali duniani, wanaohudhuria mkutano wa Majadiliano ya Kimataifa kwa Manufaa ya Wote (ISPD), 2013. Mkutano huo unafanyika katika ukumbi mpya wa kisasa wa Mwalimu Nyerere. Umewahusisha marais tisa, marais wastaafu watano na wakuu wa serikali.
Mbali ya ujio wa Rais Obama na ujumbe wake wa watu 700, serikali pia inatarajia kupokea wajumbe wengine wa mkutano wa wake za marais barani Afrika. Mikutano yote hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maofisa wa wizara hiyo ambao waliomba majina yao yahifadhiwe, waliliambia gazeti hili kuwa, katika hali ya kawaida mikutano hiyo ingefanyika mjini Arusha ambako kuna hali ya hewa ya baridi inayofanana sana na maeneo waliyotoka wageni wengi.
Wameeleza kuwa mandhari na ufinyu wa Jiji la Dar es Salaam kumeifanya serikali mara nyingi kufanya mikutano mikubwa ya kimataifa jijini Arusha ambako pia kuna hifadhi za utalii.
"Haya ni madhara ya kucheza na amani, hatutaki kunyoshea kidole mtu yeyote, lakini sote tunahusika katika hali hiyo. Tunaweza kuilaumu serikali, polisi na vyama vya siasa, lakini ni sote," alisema mmoja wa viongozi wa wizara hiyo.
Akizungumzia kufutwa kwa ziara ya Rais Obama kwenye hifadhi za taifa, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, alisema Rais Obama hakuwa na mpango wa kwenda Serengeti bali alitaka kwenda Mikumi.
"Ni kweli amefuta ziara ya kwenda Mikumi, lakini hakuwa na mpango wa kwenda Serengeti na si kwa sababu za kiusalama," alisema Waziri Kagasheki.
Matukio makubwa ya milipuko ya mabomu iliyotokea hivi karibuni mkoani Arusha, moja katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasikiti na jingine kwenye mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), huku polisi ikishindwa kuwanasa watuhumiwa, yameitia doa serikali ya Rais Jakaya Kikwete.
Katika mlipuko wa bomu la hivi karibuni katika mkutano wa hadhara wa CHADEMA, zaidi ya watu wanne wamepoteza maisha huku mawaziri wa serikali wakionekana dhahiri kuinyoshea kidole CHADEMA, huku CHADEMA wakiinyoshea kidole serikali na Chama chake Cha Mapinduzi (CCM) kwamba wanahusika.
Kishindo cha ujio wake kesho
Ukiachia kasoro hiyo, maandalizi ya ujio wa rais huyo yamekamilika.
Rais Obama, anatarajiwa kutua kesho saa 8:40 mchana, huku maofisa wa Marekani wakilazimika kushika majukumu yote katika uwanja huo, ikiwamo kuongoza ndege, ukaguzi wa abiria na mizigo.
Kazi ya kuongoza ndege ambayo kwa kawaida hufanywa na Mamlaka ya Anga Tanzania (TAA), kesho kazi hiyo itasimamiwa na Wamarekani wenyewe.
Hata idadi ya maofisa wa Tanzania wakiwamo viongozi watakaompokea Rais Obama siku hiyo pia itapangwa na Wamarekani wenyewe.
Wakati huduma ya zimamoto ikiwa inahitajika zaidi wakati ndege inapotua au kupaa, maofisa wa usalama wa Marekani wamekataa kutumia zimamoto wa Tanzania.
Tayari magari 150 ya msafara wa ziara yake yamewasili nchini, huku serikali kwa kushirikiana na makachero wa Marekani wakifanya mchujo wa majina machache ya mawaziri watakaoruhusiwa kumpokea kiongozi huyo maarufu zaidi duniani.
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Moses Malaki, aliliambia gazeti hili jana kuwa matayarisho ya ujio wa rais huyo hayajapata kutokea nchini.
Tanzania Daima Jumapili ambayo jana ilikuwa ikipita katika maeneo mbalimbali ambayo Rais huyo atapita, imeshuhudia kuwapo kwa ukaguzi wa hali ya juu ukifanywa na makachero wa Marekani katika kuimarisha ulinzi.
Wamarekani wameamua kufanya kila kitu wenyewe, kwa kuwa hawamwamini mtu yeyote, wakiwamo maofisa usalama wa Tanzania.
"Mazoezi haya yatatoa picha rasmi ya jinsi rais huyo atakavyotua, wapi bendi ikae, wapi maofisa wasimame, wapokeaji na msafara wake mzima," alisema.
Kinachoendelea ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere ni mazoezi ya kumpokea Rais Obama, hususan jinsi watu wanavyotakiwa kujipanga.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema wakati huu wa ujio wa Obama ulinzi ni mkali na wa kutisha kwa wahalifu.
Alisema mtandao mkubwa wa askari umeshawekwa tayari barabarani kuhakikisha kila kitu kinakwenda kama ilivyopangwa hadi siku ya tukio lenyewe ambayo ni kesho.
Mitaani ni Obama, Obama
Kila mtaa au kundi la watu unalokutana nalo jijini Dar es Salaam, mazungumzo ni Rais Obama na ujio wake, hususan maandalizi yanayofanywa.
Wafanyabiashara ndogondogo ndio waathirika wakubwa wa ziara hiyo ambao wengi waliozungumza na gazeti hili wamesema pasipo kumng'unya maneno kwamba wamekerwa na ziara hiyo.
Wapo wananchi hasa waliojiajiri ambao wamepanga kutofika katikati ya jiji kesho kuendelea na shughuli zao kwa hofu ya kuwapo vurugu hasa za msongamano wa magari kwani baadhi ya barabara zitafungwa kabisa.
Mandela afunika ziara ya Obama
Kutoka nchini Afrika Kusini, inaelezwa kuwa ziara ya Rais Obama imefunikwa na hali mbaya ya afya ya Rais mstaafu wa nchi hiyo, Nelson Mandela.
Maelfu ya wananchi wa taifa hilo wameendelea kufurika katika hospitali anakoendelea kupata matibabu mjini Pretoria na kuweka kando ujio wa Rais Obama

[TD="bgcolor: #ffffff"]
Afuta ziara kwenye mbunga za wanyama za Mikumi, Serengeti

na Martin Malera

[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #ffffff"][/TD]
[/TD]
source: tz. daima

Kwa hiyo hata na zimamoto nazo zimeletwa toka USA?
 
Back
Top Bottom