Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,679
- 40,931
Rais wa Marekani Barak Hussein Obama, anatarajia kuzuru kenya mnamo mwezi july mwaka huu.
Ziara yake inakuja mara baada ya kusubiri Muda mrefu sana, kutokana na pingamizi mbali mbali za ndani na nje ya nchi yake.
Mapingamizi hayo yanatokana na uwepo wa mashtaka ya kijinai katika mahakama ya kimataifa ya kijinai kwa viongozi wakuu wawili wa Kenya.
Mashtaka hayo ni matokeo ya makubaliano Baina ya Rais Mwai Kibaki na Raila Odinga , kuunda tume itakayofanya uchunguzi wa kuvumbua wahusika wakuu wa vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi mnamo mwaka 2007-2008.
Baada ya makubaliano hayo Jaji Waki alitoa ripoti yenye list ya majina ya watu waliohusika katika vurugu hizo, lakini mpaka sasa waliofikishwa mahakamani ni sita tu, ikiwemo viongozi hao wakuu wa nchi. Kumekua na maombi mbali mbali yakitaka serikali ya kenya kutoa majina yote ya wahusika yaliyomo kwenye ripoti ya waki jambo ambali halikufanyika mpaka sasa.
Baada ya wahusika kufikishwa mahakamani, Rais Obama alikua na haya ya kusema, nanukuu;

I urge all of Kenya's leaders, and the people whom they serve, to cooperate fully with the ICC investigation and remain focused on implementation of the reform agenda and the future of your nation. Those found responsible will be held accountable for their crimes as individuals. No community should be singled out for shame or held collectively responsible. Let the accused carry their own burdens and let us keep in mind that under the ICC process they are innocent until proven guilty. As you move forward, Kenyans can count on the United States as a friend and partner.
Barack Hussein Obama.
ingawa wahusika wakuu waliofikishwa mahakamani wamefutiwa mashtaka yao, lakini bado kuna kumbukumbu mbichi kwa wahanga wa vurugu hizo zilizosababisha watu zaidi ya 1,200 kupoteza maisha na wengine 500,000 kuyakimbia makazi yao.
Ziara ya Kiongozi mkuu wa Taifa lenye sifa ya kipekee ya kidemokrasia kwa taifa ambalo bado linaongozwa na waliokua wakituhumiwa katika vurugu zilizosababisha upotevu wa mali na maisha ni kama dharau kwa wale waliofikwa na majanga hayo.
Naona kama vile Rais Obama anataka kuweka historia binafsi zaidi ya kusimamia misingi iliyolijenga Taifa la Marekani na kulifanya kuwa kuu, kwa kuheshimu utu na uhai wa binadamu.
Kama Rais Obama anataka kubakiza heshima yake na ya taifa lake, basi ni wakati mzuri kwake kusitisha ziara yake hiyo na kusubiri mpaka atoke ikulu, na kwenda kuzuru Nchi ya Baba Yake. Hata kama akifanya hivyo bado katika historia iatabaki kua Marekani ilishawahi kupata kiongozi mwenye asili ya Kenya.
OBAMA LINDA HESHIMA YAKO NA YA TAIFA LAKO KWA KUSITISHA ZIARA YAKO KENYA.