Nyumbani tuna amani

roservelt

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
1,418
1,510
Nyumbani tuna amani. Tuna furaha isiyo kifani kwa sababu yule mbwa mbwekaji aliyekata usingizi wetu tumemuua! Hatutaki kelele. Wezi waje au wasije- hilo halituhusu.

Raha ya familia ni pana kweli kweli. Kile kioo cha ukutani walichotumia watoto kujitazama kamasi zao kimeondolewa. Mama ambaye kwa sura yake mbaya hakupenda kujitazama na kujikiri alivyoumbwa, anashukuru kioo hakipo! Anajipa matumaini kuanzia sasa atakuwa mzuri kwa kuwa hajitazami kwenye kioo!

Anajidanganya! Alimradi hatuna mbwa wabwekaji waliotuamsha nyakati za hatari, na wala hatuna kioo kilichotusuta taswira zetu, basi ni raha tu. Tunajidanganya. Tukiibiwa tutawakumbuka mbwa wetu. Tukichekwa kwa sababu ya kamasi na uchafu katika nyuso zetu tutakikumbuka kioo cha ukutani. Kuvipata hivyo kwataka tutubu.
 
Walimu wa arts hawawezi kupata ajira kwa mtindo huu.

Mnae maneno mengi ya kufumbafumba.
 
CCM Ilikuwa ndio tatizo kubwa la nchi CCM imekufa AMEBAKI JIWE JIWE AKIFA NCHI ITAPONA.

E MUNGU SIKIA MAOMBI YETU WATANZANIA.
 
Back
Top Bottom