doullar
Member
- Dec 29, 2016
- 31
- 13
NAKUKUMBUKA
Hazinipiti dakika,saa yendapo kulia
mzigo ulonitwika,sina wa kunipokea
nyumbani umeondoka,sijachoka kungojea
kubwa lililoniuma,kule kukuhudumia
kikwona washika tama,karibuyo nasogea
mbona moyo ukahama,nyumbani ukakimbia
uzuri wa mbalamwezi,nakumbuka sura yako
usoni macho ya wizi,yalininogesha kwako
zimebaki simulizi,ni wapi uko uliko
si jambo la kupendeza,hukua mpenzi mwema
na viungo kupooza,ni kazi yake hashima
ndicho kilichokuponza,ukauvunja mtima
Hazinipiti dakika,saa yendapo kulia
mzigo ulonitwika,sina wa kunipokea
nyumbani umeondoka,sijachoka kungojea
kubwa lililoniuma,kule kukuhudumia
kikwona washika tama,karibuyo nasogea
mbona moyo ukahama,nyumbani ukakimbia
uzuri wa mbalamwezi,nakumbuka sura yako
usoni macho ya wizi,yalininogesha kwako
zimebaki simulizi,ni wapi uko uliko
si jambo la kupendeza,hukua mpenzi mwema
na viungo kupooza,ni kazi yake hashima
ndicho kilichokuponza,ukauvunja mtima