VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Serikali ya awamu ya kwanza chini ya Hayati Mwalimu Nyerere ilitenga maeneo maalum ya kiserikali. Humo yalijengwa majengo mbalimbali ya kiserikali kama nyumba za kuishi, masoko na kadhalika.
Nyumba za kuishi ziliwalenga hasa watumishi wa Serikali walio kazini. Lengo lilikuwa kuwaweka pamoja na kuwarahisishia ulinzi wa pamoja na urahisi wa kufika kazini. Watumishi wa umma walio kazini waliwekwa kwenye nyumba za serikali ili waishi humo.
Nyumba za serikali zilipigwa bei/kuuzwa wakati wa Serikali ya awamu ya tatu. Ikasemwa na kuandikwa kuwa nyumba hizi za serikali ziliuzwa kwa bei ya kutupa na bila kufuata utaratibu uliopaswa kufuatwa. Wakauziwa wasiostahili; waliostahili wakazikosa.
Sasa, viongozi wa kiserikali kama Mawaziri, Majaji na wengineo wanaishi walipobarikiwa kupata makazi. Huyu anaishi hapa, huyu pale; na huyu kule. Mambo ni shaghalabaghala. Hata ulinzi na upatikanaji wa watumishi hawa unakuwa wa mashaka.
Hili ni jipu. Kimchakato. Anasubiriwa mtumbuaji alitumbue!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam