Nyumba za Diwani CCM zachomwa moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba za Diwani CCM zachomwa moto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Jul 30, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  DIWANI wa Kata ya Idetemya wilayani Geita, Juma Nyembe Machibya (49) wa CCM amepata hasara ya zaidi ya Sh milioni 51 baada ya wananchi wa kijiji cha Nyabulanda kumvamia na kuteketeza kwa moto nyumba zake nne za bati na mali nyingine kufuatia mgogoro wa eneo la kujenga makao makuu ya kata.

  Mali nyingine zilizoteketezwa na wananchi hayo ni pamoja na baiskeli tano, mahindi, mpunga, pikipiki, kuku 21, kondoo mmoja na pesa taslimu, sh milioni 1.6.

  Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Mugeta Jandwa alisema , tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 4.54 asubuhi katika kijiji cha Nyabulanda wilayani Geita.

  Alisema, sababu ya kuteketezwa kwa mali za Diwani huyo ni wananchi wa kijiji cha Idetemya na Nyabulanda kugombea makao makuu ya ya kata yajengwe katika kijiji cha Nyabulanda.

  Jandwa alisema, jeshi la polisi linawasaka wananchi waliohusika na tukio hilo ambapo upelelezi ukikamilika watafikishwa kwenye mikono ya sheria kwa hatua zaidi.

  Aidha, Jandwa alisema siku hiyo ya tukio majira ya saa 9 mchana wananchi wa kijiji cha Nyabulanda walimjeruhi kwa mawe kichwani Mkuu wa kituo cha polisi NyangwÂ’ale E. 2534 Koplo Masunga (43) baada ya kutega mawe barabarani.

  Mkuu huyo wa kituo alikutwa na zahma hiyo akiwa na Inspekta Barige wakati wakitoka kuwakamata watuhumiwa wa kosa la kutishia kuua kwa maneno katika kijiji hicho ambapo walitega mawe barabarani na waliposimama ndio wananchi walipoanza kumrushia mawe na kumpata kichwani.

  Jandwa aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kwa tuhuma za kumtishia kumuua Diwani huyo kuwa ni pamoja na Medai Fungame (28), Masumbuko Pius (37) na Stephano Malimi (61).

  Hata hivyo alisema hali ya Masunga inaendelea vizuri na kwamba polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio ili hatua zaidia za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa waliohusika.
   
 2. franksarry

  franksarry JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2011
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 1,107
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Nawapa Pole sana Mh Diwani na Afande kwa masahibu yaliyowapata...
  Haya yote ni kutokana na Ugonjwa wa Uongozi legelege, ugonjwa huo upo mpk ngazi za chini!

  Waathirika wa hilo tukio ni imani yangu wakipitisha kikapu cha msaada Mjengoni kwa Walipukaji watawasaidia kutoka ktk posho zao, kama alivyowahi kunukuliwa Kiongozi Mkuu wa walipukaji mjengoni, alipo comment khs Posho!
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  DUh akina Mura mnatishaaaaa
   
 4. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mura geita mkuu?
   
 5. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wananchi wanazidi kugain confidence taratibu kwa sababu ya viongozi wasiojua wajibu wao.Ipo siku watampopoa kiongozi mkubwa zaidi hawa wadogowadogo kama mambo yataendelea hivihivi.
   
 6. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Well said!! Lkn umesahau JK alipopolewa Chunya??
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Pole pole tunaelekea gymkhana square!
   
 8. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #8
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Poleni sana waathirika. Lakini si walisema TZ kuna amani?
   
 9. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Poleni, bora sio wa CDM maana tungesikia mengi.
   
 10. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  nikweli jamani hadi ngombe wamechomapole uongozi ni dhamana diwani
   
 11. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />

  Mkuu ushasahu wananchi waliwahi kumpopoa kwa mawe Vasco da Gama kule Mbeya?

  Sema ipo siku wananchi wataipopoa Magogoni
   
 12. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  jamani wana geita hasira hiyo wangekuwa nayo siku za nyuma huenda madini yao yangekuwa na maana kwao, kuliko ilivyo sasa ambavyo wanaachiwa mashimo na umasikini wa kupindukia
   
Loading...