Hanzu Runi
Member
- Dec 28, 2014
- 49
- 34
Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, kwa baraka za Mkurugenzi wamemgawia nyumba ya serikali ukanda wa Pwani, Ghuba ya Mkoma, kwa mmliki wa taasisi ya kigeni inayojitegemea (NGO) iitwayo Uzikwasa.
Mwenye taasisi hiyo, Vera Pieroth, miaka ya karibu amekuwa akiwaghilibu uongozi wa wilaya kwa vimisaada-misaada kwa hospitali ya Pangani na ukarabati-karabati wa maghofu kwa pesa za serikali za nje.
Kulipa fadhila binafsi, halmashauri bila kupitisha tenda, wala kupata baraka za kikao cha madiwani, imeamua kumzawadia huyo mama wa nyumba iliyokuwa ya Mganga wa Wilaya, kwa "malipo" ya Shiling 79, 000 (elfu sabini na tisa). Nyumba ya serikali pwani amemilikishwa huyo mama wa kigeni.
Mbali ya kutoa mgao huo, mmliki huyo pia amemilikishwa maaneo mawili ya pwani ya Stahabu, njia kuelekea Saadani.
Shamba moja la ekari 25 na shamba jingine la ekari 12.5 katika maeneo ya Choba, njia ya Tanga.
Taarifa hizi zimliwakilishwa ka uongozi wa Wilaya, Kamati za Ulinzi na Usalama, na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa bila hatua zozote kuchukuliwa. Jipu sugu!