Hapana mimi hapo napata kitu kidogo sana. Hili eneo viwanja vinauzwa bei ghari. Ungekua na muda ningekutembeza uone viwanja maeneo hayo vinauzwaje.kina ukumbwa wa sqm 900. Eneo lina uzio.
Pia hiyo nyumba ambayo haijakamilika imejengwa kwa tofari zilichanganywa mchanga, sementi na kokoto. Kawaida tofari moja la namna hiyo huuzwa sh 2000. Msingi,uzio na ukuta vimekula tofari 7000 hapo unazungumzia sh 14mil.
Tofari zimelazwa hazijasimamishwa zimalazwa. Zege na nondo vinakadliwa kufikia 20mil. Sasa hiyo 34 plus gharama za ufundi plus bei ya kiwanja kwa nini isiwe juu? Nadhani naongea na watu wanaojua gharama za ujenzi na thamani ya ardhi.