Nyumba inapangishwa Magomeni Kanisani

Nyumba inapangishwa Magomeni Kanisani

Mwanafalsafa

Platinum Member
Joined
Jun 24, 2007
Posts
682
Reaction score
873
Ina Vyumba viwili, jiko, bafu, stoo, sebule kwa Tshs. 350,000/- kwa mwezi (ambayo inajumlisha na umeme).

Iko katika hali nzuri sana, bado mpya. Sakafu ndani ni ya vigae, na uwanja wa nje umesakafiwa kwa sementi. Bati halivuji, ceiling board bado mpya. Haihitaji matengenezo yoyote.

Ina ukuta na geti. Iko eneo zuri tulivu la wastaarabu, ambako nyumba nyingi zina mageti. Usalama ni wa kutosha unaweza kulala mlango wazi, dirisha wazi.

Gari linafika mpaka ndani, na nafasi ya kuegesha gari moja ndogo ndani ya geti.

Ina umeme wa akiba wa inverter endapo wa TANESCO utakatika.

Nyumba hii inafaa sana kwa watu wanaofanya kazi au biashara katikati ya jiji (Posta/Kariakoo/Muhimbili), au hata ukanda wa mpaka Sinza/Mwenge/Ubungo/Kawe wasiopenda kupoteza muda kwenye foleni, au kudamka asubuhi sana.

Eneo hili ukiondoka nyumbani saa moja asubuhi unawahi kazini bila matatizo.

Kwa mawasiliano piga simu namba 0755027764 (au ukikuta haipatikani tuma msg nitakupigia)

Muhimu:

1. Kodi inaweza kulipwa kwa mwaka, au kwa miezi sita sita.

2. Mnaweza kushea wawili mkalipa nusu kodi.

3. Madalali mnakaribishwa. Ila kama wewe ni dalali naomba ukitaka kuja uje na mteja kabisa.

Picha:

1. Sebule

2426c0w.jpg


2. Choo/Bafu

othsno.jpg


3. Jikoni

dfkglk.jpg


4. Vyumba

2naip2c.jpg


1iif7c.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom