Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
David Kafulila, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR- Mageuzi) na ambaye amefungua shauri mahakamani kupinga kutangazwa kwa Husna Mwilima, kuwa mbunge wa jimbo hilo, ameanza kupata ushindi katika shauri lake,anaandika Pendo Omary.
Ni baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora chini ya Jaji Ferinand Wambali leo kuridhia maombi yake ya kuwasilishwa mahakamani hapo, fomu halisi za matokeo ya uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Kafulila alikuwa ameiomba mahakama kuamrisha NEC kuwasilisha fomu hizo mahakamani ili ziweze kupitiwa kwa kulinganishwa na fomu alizowasilisha Kafulila.
“Hiki kilikuwa kizingiti kigumu sana. Lakini tunamshukuru Mungu tumekivuka. Uamuzi wa mahakama wa kuiagiza NEC iwasilishe fomu halisi za matokeo, imerahisisha kazi yetu ya kudai haki,” ameeleza mmoja wa wafuasi wa Kafulila, nje ya mahakama mjini Kigoma.
Katika shauri hilo, Kafulila anatetewa na wakili mashuhuri nchini, Prof. Abdallah Safari.
Awali wakili wa mshitakiwa wa pili, mbunge wa jimbo hilo, Husna Mwilima, pamoja na wakili wa serikali walipinga maombi ya Kafulila.
Katika uchaguzi mkuu uliofanyika 25 Oktoba, inadaiwa kuwa Kafulila ndiye aliyeibuka kidedea. Lakini msimamizi wa uchaguzi alimtangaza mgombea huyo wa CCM, badala ya Kafulila.
Chanzo: Mwanahalisi online