Nyota Nyekundu Special Thread

Kwa heshima na taadhima, naienzi hii timu ya kijiweni Mtaa wa Congo ambayo ilishiriki ligi kuu Tanzania Bara na kuwa tishio kwa kupiga mpira na buti.
Rosta Ndunguru na wenzako, tunawakumbukeni sana kwa kuleta na kucheza soka tamu la ushindani nchini mwetu Tanzania
Hebu nipe line up ya Red Star
 
Steven Names, Morris Nyuki, Mbaraka Mohamed, Mohamed Nyauba, Pazi Ally, Faustine Kibingwa, Steven Chibichi, Hamis Dilunga, Ayubu Mzee, John Manyama na Rosta Ndunguru
Kuna sub wao Haruna?Mahundi au somebody Mahundu,naye alikuwa mzuri.Thanks bro for the first 11.Umeipatia mno
 
Nalikumbuka chama langu. ...enzi hizo golini unamkuta Steven nemes, pembeni anasimama musa Kihwelu (r.i.p) na mapunda (jina la mwanzo limenitoka ),mabeki wa kati wanasimama abas kuka na frank kassanga bwalya ,dimba dogo anakamata muhidin pazi na Steven chibichi,mawinga wanasimama rosta ndunguru na. .. washambuliaji ni mohammed mgalike na John mgazija .....kwenye bench kuna golikipa omar pazi, zonte'dj',.....chini ya kocha king kibadeni
 
Nalikumbuka chama langu. ...enzi hizo golini unamkuta Steven nemes, pembeni anasimama musa Kihwelu (r.i.p) na mapunda (jina la mwanzo limenitoka ),mabeki wa kati wanasimama abas kuka na frank kassanga bwalya ,dimba dogo anakamata muhidin pazi na Steven chibichi,mawinga wanasimama rosta ndunguru na. .. washambuliaji ni mohammed mgalike na John mgazija .....kwenye bench kuna golikipa omar pazi, zonte'dj',.....chini ya kocha king kibadeni
 
Nyota Nyekundu Sports Club
John Bosco, Morris Nyuchi, Mohamed Nyauba Pazi Ali, ,
Frank Kasanga (Bwalya), Mohamed Mgalike, Roster Ndunguru.

Vv
 
Steven Names, Morris Nyuki, Mbaraka Mohamed, Mohamed Nyauba, Pazi Ally, Faustine Kibingwa, Steven Chibichi, Hamis Dilunga, Ayubu Mzee, John Manyama na Rosta Ndunguru
Marhaba hapo sawa kabisa ila pana mtu aliitwa frank kasanga "bwalya "hao watu utakuta bango lao wameandika "kumkoma Nyani giladi"waqt umekwenda sana pia John bosco ambae baadae alikwenda yanga mweupe kwa wajihi alikuwa beki mshahara kweli alipita hapo.
 
Mimi nilikuwa mpenzi wa TKY Stars, huu ni wasifu mfupi wa timu yangu iliyochukua ubingwa mwaka 1986.


Suleiman Mathew
KWANZA kabisa nawashukuru wote
waliopiga simu na kutuma ujumbe mfupi
kuwa, ingekuwa vipi kama MECCO na Tukuyu
zingekutana, ipi ingeibuka kidedea?
Baada ya kuandika hoja hii, wengi walitoa
maoni yao kuhusu ingekuwaje kama
Tukuyu Stars ya mwaka 1986 na Mecco ya
mwaka 1988, zingekutana katika Uwanja
wa Sokoine Mbeya.
Kati ya waliotoa maoni yao, 38 wameipa
nafasi Tukuyu Stars kuwa ingeshinda huku
27 wakiipa nafasi Mecco kuwa, ingeshinda.
Kwa idadi ya maoni yote, Tukuyu Stars
imeizidi Mecco kwa kura 11.
Binafasi nasema asanteni nyote kwani
imeonyesha kweli watu wamekuwa
wakizifuatilia timu hizo mbili na kubwa
zaidi, wakiridhika kuwa zilikuwa ni timu
zilizokuwa zikicheza soka ya uhakika.
Baada ya kusema hayo, naomba leo
niwaletee kwa ufupi wasifu kila mchezaji
wa timu hizi ambao niliwataja kwa timu
zote mbili ili kumfanya msomaji upate
ufahamu kwa kiasi fulani kuwa wachezaji
hawa walikuwaje, nikianza na Tukuyu Stars:
Mbwana Makata: Ni kipa wa aina yake
aliyekuwa anajua kusoma mchezo na kutoa
maelekezo kwa mabeki wake na alikuwa
mkali kwa mabeki wazembe wenye kufanya
makosa ya kijinga.
Langoni, alikuwa na uwezo sana wa
kucheza krosi, licha ya kuwa na kimo cha
kawaida, hivyo msimu wa mwaka 1986,
alikuwa kati ya wachezaji waliochangia kwa
kiasi kikubwa mafanikio ya Tukuyu Stars.
Ally Kimwaga: Huyu alikuwa beki wa kulia,
aliyekuwa na uwezo wa kupanda mbele
mara kwa mara kwa dakika zote 90.
Alikuwa na mbio sana baadhi ya mabao
iliyokuwa akifunga Tukuyu Stars, yalitokana
na beki huyu.
Hakuwa mchezaji mwenye makeke, lakini ni
mwajibikaji, sikumbuki kama aliwahi hata
kupata kadi yoyote uwanjani. Aidha, alikuwa
beki asiyekubali kupitwa au kwa maneno
mengine beki king'ang'anizi.
Daniel Chundu: Beki wa kushoto asiyekubali
kupitwa kirahisi huku akipanda mbele na
burudani ilikuwa pale napo anapokumbana
na mabeki wa upande wa pili, ilikuwa ni
shughuli kubwa ya beki dhidi ya mabeki.
Uchezaji wake ulikuwa ukiwapa wakati
mgumu mawingi wa kulia na kwa vile
hakuwa akitumia mguu wa kushoto,
alikuwa anawasubiri mawingi katikati ya
uwanja na kweli alifanya kazi yake vizuri.
Godwin Aswile: Alikuwa ni beki wa aina
yake asiyetaka masihara hata chembe.
Alikuwa kisiki kwa mipira ya aina yoyote ya
juu na chini na ilikuwa vigumu sana
kumpiga chenga za ovyo huku akiwa tayari
kucheza soka ya kistaarabu hata ya kihuni.
Waulize wachezaji machachari wa Red Stars,
jinsi Aswile ambavyo alimfanyia rafu mbaya
Roster Ndunguru, kisa ni kutokana na
ngebe ya Ndunguru uwanjani. Kwa hakika,
alikuwa ni beki wa aina yake dimbani.
Suleiman Mathew: Akiwa beki wa mwisho,
alikuwa hana makeke mengi zaidi ya
kutumia akili katika kukabiliana na
washambuliaji, alitumia nguvu ilipobidi na
alikuwa anajua jinsi ya kujipanga ili kuzuia
mashambulizi.
Alicheza nafasi ya ulinzi wa kati ilivyostahili
hadi mwaka huo kuchaguliwa timu ya taifa.
Aston Pardon: Huyu alikuwa kiungo wa
nyuma alikuwa mahiri katika kukaba na
kupanda mbele kuongeza mashambulizi.
Alikuwa na uwezo wa kucheza soka ya aina
yoyote alipoona timu inaelemewa yeye ndiye
alikuwa mtulizaji wa timu alikuwa anapenda
sana kila mpira upitie kwake kwa kweli
alikuwa na uwezo wa hali ya juu.
Yusuph Kamba 'Sharif': Kiasili, ni mchezaji
wa kiungo namba 8, lakini Kocha Athumani
Juma ambaye kwa sasa ni marehemu,
alikuwa akimtumia sana kama wingi wa
kulia.
Ni mchezaji aliyekuwa na kipaji cha soka,
akili na alikuwa anajua jinsi ya kutoa pasi za
uhakika Yanga wanamkumbuka kwa jinsi
alivyowasumbua Uwanja wa Taifa, kisha
kutoa krosi iliyomkuta Richard Lumumba
aliyefunga bao la ushindi licha ya yeye kuwa
Yanga damu, kwani kitu alichokuwa amejali
ni wajibu wake.
Katika mechi zote, nakumbuka bao lake la
mita 30 alilowafunga Coastal Union pale
Tanga.
Peter Mwakibibi: Kiungo wa kati, aliyekuwa
na nguvu, mashuti na uwajibikaji uwanjani,
aliimudu vema nafasi yake katika
kusambaza mipira kwa washambuliaji na
alikuwa na uwezo wa kupambana na yeyote
wa kiungo, wengi walimheshimu.
Richard Lumumba: Hakuna ubishi kwa
mshambuliaji huyu alikuwa hatari sana kwa
mipira ya juu na alifunga mabao mengi kwa
kichwa, ingawa alikuwa na uwezo wa
kufunga hata kwa mguu.
Alikuwa kipande cha mtu asiyeogopa
chochote, hivyo kuchangia kwa kiasi
kikubwa ubingwa kwa Tukuyu Stars mwaka
1986.
Alimudu sana nafasi yake akiona mambo ni
magumu alikuwa akicheza kibabe.
Kelvin Haule 'Super': Nyota nyingine ya
ushambuliaji ya Tukuyu Stars, alikuwa na
akili ya ziada na uwezo wa kufunga mabao
kutoka pembe yoyote ya uwanja.
Aidha, kasi yake uwanjani ilikuwa ya ajabu
hata kuwa kivutio uwanjani, alifunga bao
aina yake kule Shinyanga dhidi ya Mwadui,
ambalo litabaki kukumbukwa ambalo
lilitosha kuipa Tukuyu Stars ushindi wa bao
1-0.
Karabi Mrisho 'Nnunduma': Nyota
iliyopotea ghafla katika soka ya Tanzania.
Alikuwa wingi ya kushoto hatari sana.
Aidha, naamini kama angeendelea kucheza
soka, Celestine Sikinde Mbunga na Edibily
Lunyamila, wangekutana na upinzani
mkubwa kwani alikuwa na kasi kubwa.
Alikuwa na uwezo wa kupiga chenga kwa
kumfuata adui na krosi za uhakika. Hata
hivyo, aliumia goti katikati ya ligi
inahuzunisha kwamba hakupata nafasi ya
kuonyesha kipaji chake na hilo jina la
Nnunduma alipewa na wapenzi wa soka wa
Mbeya wakimlinganisha na mshambuliaji wa
Zimbabwe.
Kocha wa Tukuyu Stars alikuwa ni Athumani
Juma Kalomba ambaye kwa sasa ni
marehemu.
Wachezaji wa akiba ni: Seleman Mwankenja
(kipa), Hussein Zitto, John Alex Lwena,
Abdallah Shaibu, Dickson Makwaya, Taisi
Mwaliyoga, Danford Ngessy na Mohamed
Salehe.
Hawa wote walishiriki kikamilifu katika
kuchangia ubingwa wa Tukuyu Stars
mwaka 1986. Walikuwa wachezaji wazuri,
isipokuwa tatizo lilikuwa ni kukosa nafasi
na walipopata walitumia vizuri.
Angalia wachezaji kama John Alex na
Danford Ngessy walivyowika miaka
iliyofuata.
Maelezo haya mafupi ya wasifu wa nyota
waliokuwa wakiunda kikosi cha Mecco cha
mwaka 1988, yataendelea Jumatatu ijayo.
Mathew ni mchezaji wa zamani aliyewahi
kung'ara na klabu mbalimbali, ikiwemo
Yanga na timu ya soka ya Tanzania, Taifa
Stars, ambaye kwa sasa anamiliki kituo cha
michezo cha Tanzania Sports Catalyst
kilichopo Kwembe, Kigamboni jijini Dar es
Salaam.

Umenikumbusha mbali Mkuu.Huyo Peter Mwakibibi alikuwa hatari kweli.
 
Kwa heshima na taadhima, naienzi hii timu ya kijiweni Mtaa wa Congo ambayo ilishiriki ligi kuu Tanzania Bara na kuwa tishio kwa kupiga mpira na buti.
Rosta Ndunguru na wenzako, tunawakumbukeni sana kwa kuleta na kucheza soka tamu la ushindani nchini mwetu Tanzania
Ilizaliww baada na watu waliotoka Simba kama ambavyo Pan Africa ilianzishwa na watu waliotoka Yanga
 
Back
Top Bottom