Nyoosha kidole Adela; Prof. Sospeter's Muhongo fuata nyayo

MWANAWAVITTO

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
228
250
Katika wimbo wake wa Adela msanii Mrisho Mpoto anamtaka ADELA KUNYOOSHA KIDOLE ILI AKUMBUSHWE JAMBO KAMA SIYO KUFUNDISHWA JAPO YEYE AMEPITA DARASANI. leo hii pia napenda kumwomba Prof, Sospeter's Muhongo waziri wa NISHATI NA MADINI naye kunyoosha kidole ili nimkumbushe jambo japo yeye ana elimu kubwa kunizidi.

1-PROF, MUHONGO, KENYA WAMEWEZA. Kutokana na kukua kwa mahitaji ya nishati ya umeme pamoja na kupungua kwa vina vya maji sehemu mbalimbali duniani hususani kusini mwa jangwa la sahara umeme unaozalishwa kwa njia ya maji[Hydro electric power] umejikuta haukidhi haja hivyo kusababisha upungufu katika uzalishaji na hivyo kupelekea mgao wa mara kwa mara. kutokana changamoto hizo wanadamu na wadau mbalimbali wa sekta ya nishati ya umeme wamekuwa wakihaha huku na kule kutafuta njia mbadala. wakitumia sayansi na utafiti wa hali juu wamegundua kuwa njia ya kutumia mikondo ya chemchem za maji moto [ hot streams ] ndiyo njia mbadala. hivyo wataalam wa JIOLOJIA wameanza kutumika kwa kasi kubwa. baadhi ya nchi ambazo zimepiga hatua kubwa katika miradi hiyo ni pamoja KENYA.

[a]MIKAKATI YA KENYA. nieleze kwa ufupi, Kenya wameingia mkataba na kampuni mbili kufanya utafiti na kuwekeza katika maeneo ya bonde la ufa kule NAKURU na NAIVASHA. .OLKARIA STREAMS-NAIVASHA kampuni ya KENGEN imepewa zabuni ya kutafiti na kuzalisha kiasi cha 280MW hadi 380MW mradi utakapokamilika kwa dau la USD $ 140 milioni. .MENENGAI POWER PLANT-NAKURU Kampuni ya Geothermal developing company imepewa zabuni ya kutafiti na kuzalisha kiasi cha 1600 MW hadi 2000 MW mradi utakapokamilika kwa zabuni ya US $ 145 milioni. katika miradi yote hii inategemewa kuwa kiasi cha 10000 MW kinatarajiwa kuzalishwa ifikapo mwaka 2023 hivyo kumaliza kabisa tatizo la upungufu wa umeme.

2-. TANZANIA TUMELOGWA? Wakati hayo yakiendelea TANZANIA tumeanzisha utafiti katika maeneo ya MBEYA na RUFIJI huko Mbaka na Living stone ILI KUZALISHA KIASI CHA 10 MW kwa kila kituo. nafarijikika kwa kuwa PROF MUHONGO umeitembelea miradi hiyo ambapo lengo kubwa na nguvu kubwa imeelekezwa katika VOLKANO ya NGOZI ili kuzalisha kiasi cha 100 MW ifikapo mwaka 2014.

[a] MBWA KAYARUDIA MATAPISHI YAKE MWENYEWE. L icha ya ukweli usiyopingika kuwa miradi ya umeme WA MAJI ndiyo iliyotufikisha hapa kutokana na kukauka kwa vyanzo mbalimbali vya maji kunakotoka na uharibifu wa mazingira. nimeshtushwa na kushagazwa na ZABUNI hii kwa ZARS. .ZARS ni kampuni ya KIRUSI iliyopewa zabuni ya US $ 700 milioni ili kuzalisha umeme wa maji huko RUMAKALI-IRINGA unaofikia kiasi cha 222 MW hadi 464 MW mradi utakapokamilika ambao ni asilimia 25% YA UMEME UTAKAOZALISHWA NCHINI , kampuni hii hii imewekeza UGANDA na inazalisha kiasi cha 750 MW katika eneo la KARUMA . haya yote yanajitokeza wakati ambapo wataalam wa masuala ya MAZINGIRA wanaonya kuwa kiwango cha maji yaliyo nchi kavu kinaendelea kupungua siku hadi siku, jambo la kushangaza ni kuwa 'licha matatizo ya umeme yaliyopo kuwa yamesababishwa na upungufu wa kina cha maji kutokana ukame wa muda mrefu, tumerudi na kuwekeza tena katika miradi ya UMEME WA MAJI ambayo kina chake kinapungua siku hadi siku' Mhe prof Muhongo "je maji yatakapopungua kule RUMAKALI utafanya nini? au huo ni mpango wa kuzalisha RICHMOND mpya katika siku zijazo?PROF, MUHONGO nyoosha kidole.
 

Fpam

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
290
0
Hivi ule mradi wa umeme wa upepo kule makambako na singida kama sikosei imeishia wapi?

maana nchi hii ina miradi ya umeme mingi na yote huwa haiishi

O.M.G nchi nan katuroga?
 

Azipa

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
1,071
1,225
Miradi ya umeme ni mirija ya mafisadi. Mimi naona upo sahihi. Hawana nia ya dhati ya kutatua tatizo la umeme

Maendeleo yapo kwenye umeme. Ukiwepo umeme wawekezaji watajazana Tanzania. Ajira zitakuwa za kumwagwa. Hakutakuwa na waganga njaa.

Tukiwa na pesa ubwabwa, Tshirt na kofia za CCM nani atazitaka

N.B Durban wanataka kuzalisha umeme toka baharini. Sijui huo mradi umefikia wapi. Hiyo hiyo bahari ya Hindi
 
Top Bottom