Nyongeza ya mishahara hakuna, najenga Nchi

Nyongeza ya mishahara hakuna, najenga Nchi

kamtesh

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Posts
1,395
Reaction score
514
Kauli ya hovyo ilishawahi tolewa na rais. Alikuwa anajua ni Haki ya Kikatiba ya watumishi, lakini kwa jeuri akajibu hivyo. Alisahau kuna Uchaguzi tena after 5 years.

Leo akiulizwa hana jibu tena anaahidi tena kuongeza kama vile alivyoahidi maisha bora ya watumishi 2015 akiingia madarakani. Akatupilia mbali hiyo ahadi, na kuwanyanyasa watumishi, na kuleta tumbua tumbua ya hovyo nchi mzima, yaani kuwafedhehesha watumishi na kuwanyima Haki zao.

Leo hana jibu ndo maana amepwaya sana. Alifikiri kununua ndege, kujenga fly over ya Ubungo, Bwawa la Nyerere na reli watu watampaisha na kumuongezea mitano tena. Kaona imeshindika vibaya mno. Alisahau maisha ya watu akapenda vitu kutaka Tanzania iwe kama Ulaya ndani ya miaka mitano. Icho kitu hakiwezekani, ulaya na Marekani vimechukua miaka mingi kufikia hali walionayo.

Leo Marekani kampeni ni kuhusu AJIRA kwa wananchi, maisha ya watu, Bima ya afya, yaani kiufupi ni swala la maendelo ya watu, ila ndani ya hayo maendeleo ya watu, kuna maendeleo ya vitu.

Kama ni rushwa, watu awamu hii wamepiga hela kweli kweli kuli EPA, RICHMOND, IPTL sijui nini! Matrilion yamepotea kusiko julikana kimia kimia, huku maslahi ya watumishi na wanyonge wengi yako taabani.

Tujiuluize kwa mini Mkaguzi Prosefa Assad alitolewa na kukaliwa ku-renew mkataba, nahisi alionekana mwiba, ndo maana alisema binge ni dhaifu, Ndugai akaja huu, maana wanashirikiana. CCM bado wanataka wabunge wakendelee kupitisha matumizi haramu huku maisha ya watu yakizidi kudidimia.

Wakataeni wabunge wa CCM, hawana msaada kwa taifa hili, wanajinufaisha wao tuu, huku maisha ya wanyonge hana zaidi kuwa mabaya.

VIVA WAPINZANI, SAFARI HII NI KUJENGA AU KUBOMOA. WANANCHI MUKIKOSEA IMEKULA KWENU
 
Itashangaza sana kwenye uchaguzi huu kama kuna mtumishi anaipa CCM kura. Tumeshamuona huyu mtu jinsi alivyotutesa na kutuhadaa. Ana majibu ya hovyo kwa watumishi sana. Kura yako mwaka huu ni ya thamani sana. Watumishi acheni mazoea ya kupiga kura kwa CCM.
 
Huyu akaangwe kwa maneno yake ya kifedhuli tarehe 28/10/2020.
 
sasa ndugu yangu hayo maendeleo mengine yangetokea wapi bila bajeti nyingine kupunguzwa. Rais wetu Magufuli ameweza kufanya wafanyakazi kupata mishahara yao kwa wakati sio kama kipindi kile
 
Yeye Sera ni mabarabara tu na fly overseas kana kwamba wembe utakua uleule wakuchezea maisha yetu.
 
Itashangaza sana kwenye uchaguzi huu kama kuna mtumishi anaipa CCM kura. Tumeshamuona huyu mtu jinsi alivyotutesa na kutuhadaa. Ana majibu ya hovyo kwa watumishi sana. Kura yako mwaka huu ni ya thamani sana. Watumishi acheni mazoea ya kupiga kura kwa CCM.
Hawategemei kura za watumishi,wanakura za kutosha mabegi yanajaa.
 
Back
Top Bottom