Nyoka wa ajabu

Yaani mkuu nimecheka mpaka basi
 
Hakuna nyoka wa ajabu wala sungura au kunguru,hizo ni njozi.UNUSUAL DREAMS mara nyingi huwapata watu wanaotumia aina fulani ya madawa.Watu wanaotumia dawa za kupunguza makali (ARV) Hasa dawa ya EFAVIRENZ huwaletea njozi mbaya za kutisha.Huenda mtoa mada yuko kwenye dose za ARV au dawa zingine.Kwa wale wanaotumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu mara nyingi hua wanapatwa na tatizo la HALLUCINATION.Mwathirika ataanza kuona vitu au viumbe mbele yake wakati ninyi wazima hamuoni chochote.Madereva walioathirika huweza kumwona mtu,mnyama,nyoka nk wakikatisha k atikati ya barabara na anapojaribu kukwepa anapinduka.Akinusurika kufa yeye hudai eneo la mahali pale kuna wachawi.
 
Duu hii sasa kiboko
 
sawa mkuu, sitarudia tena kulala mchana kabla sijala
Jimena, kwani husomi nilichokueleza hapo juu? Sababu sio kulala mchana bila kula mimi ni daktari zingatia sababu nilizokutajia.Hakuna sababu zingine labda ziwe za kienyeji.
 
Jimena, kwani husomi nilichokueleza hapo juu? Sababu sio kulala mchana bila kula mimi ni daktari zingatia sababu nilizokutajia.Hakuna sababu zingine labda ziwe za kienyeji.
Sasa mi situmii ARV wala drugs ndio maana sikufatilia ushauri wako.
 
Basi ni mambo ya kienyeji na SUPERSTITIONS ambako sayansi haifungamani nayo,fuata ushauri wa kula kabla ya kulala itakusaidia!!!.
 
Basi ni mambo ya kienyeji na SUPERSTITIONS ambako sayansi haifungamani nayo,fuata ushauri wa kula kabla ya kulala itakusaidia!!!.
Mambo ya kienyeji nayo ni myth tu
 
Mkuu, tiba sahihi ya kushiba kabla ya kulala nadhani umeshapata unataka watu wakwambie nini tena?
 
mmmmh. ....
 

Wewe ni Mtanzania. Kupitia post mbalimbali ni maisha. Kusinzia ni kupoteza umakini.

Njiwa wawili walio juu ya mti wa Krismasi ni uongozi mzuri wa chama na serikali kuongoza nchi.

Wewe kutaka kuwala njiwa wale wawili ni wananchi kutaka uongozi mzuri wa chama na serikali uwasaidie kutatua matatizo yao, ikiwamo njaa na mengine.

Nyoka kugundua kwamba wale waliodhaniwa ni njiwa juu ya mti wa Krismasi si njiwa ni kunguru, ni wananchi kugundua kwamba uongozi wa chama na serikali si mzuri, ni mbaya na haufai. Wamehadaa wananchi kwa ahadi za uongo wakaonekana wazuri, walivyofika kwenye uongozi wanaonekana tofauti.

Sungura waliopita chini ya ule mti ni vyama vya upinzani.

Hii ndiyo tafsiri ya ndoto yako.
 
Dah pole sana kaka iyo ni ishara mbaya sana kwako,unatakiwa ujitafakali mwenendo wako sio mzuri kuna mapepo au mashetani au unaroho ya uasi,maana yake shetani anakutumia kwa kukutamanisha ni iv ww ni nyoka ni mambo yako ya kishetan tena shetani kakuvaa sanaa na ananutumia kwa nguvu nyingi sana anakutamanisha na unatamani unafata matamanio yako lkn upate unachokitamani,na ukikata shauri unatamanishwa zaidi
 
Asante sana Kiranga
Nimekuelewa vizuri na nakubaliana na tafsiri yako kwani imegusa kabisa maisha ya kila siku na sio vitu vya kusadikika
 
Ila huyu shetani kama angekuwepo kweli siku moja angewajibu mana kila kitu anabebeshwa yeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…