Nyerere: Tunamtaka Rais, si mkabila na si Kaburu

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,865
2,439
Tangu kuzaliwa kwa Taifa hili ni Mara ya kwanza ambapo Watanzania wanashuhudia viongozi wa nchi Yao wakiwabagua wazi wazi, kwa misingi ya ukabila au ya kichama.

Jambo hili ni lazima likemewe na kila mwananchi wa Nchi hii mwenye mapenzi mema kwa nguvu zote.

Mimi sina la kusema zaidi ila watu wa Huku Mbeya hii ndiyo habari ya mitaani, ikiwa wewe ni wa Mbeya hata Kama Huna chama, basi ww unaonekana ni wa Ukawa. Iringa, Arusha na Kilimanjaro ndiyo usiseme.

Mimi najiuliza Kwani vyama vya siasa si vipo kwa Mujibu wa katiba?. Na Kama ndivyo, kwanini watu Tuanze kubaguana kwa mambo tuliyokubaliana?.

Najuta kuzaliwa Africa ila sijuti kuwa Mwafrica

Hakuna binadamu yeyote alizaliwa kwa ajili ya kutawala wenzake, but ikitokea ukapewa hiyo nafasi, ni lazima kwanza Umwogope Mungu sana. Na yeyote anayemwogopa Mungu hawezi kuwa Mbaguzi wa Aina yoyote. Vinginevyo basi Jua cheo chako hakitoki kwa Mungu.

Je Kama Mwalimu Julius Kambarage Nyerere angeamua Kutubagua, Leo tungekuwa Nchi ya namna gani. Tu jiulize, Je tunakwenda Mbele au Tunarudi nyuma?. Binafsi, simpendi Mbaguzi yoyote, awe Mama yangu awe Baba yangu Dada, Kaka Mjomba Shangazi awe yeyote, I hate..
 
Major pole,kuna mtu alisema CHADEMA siyo watanzania.Hivyo sitoshangaa
 
Back
Top Bottom