Nyerere na ujinga

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2010
Posts
2,182
Reaction score
309
Nyerere aliwahi kusema hivi "mtu akiwa anajua kuwa una akili timamu, akakwambia kitu cha kipumbavu na akajua unajua ni cha kipumbavu na ukakubari, atakudharau"

Leo hii tunapojiandaa na uchaguzi mkuu watakuja watu wanatuambia kuwa Jakaya Mrisho Kikwete ni mtu anayefaa kupewa ridhaa ya miaka mingine mitano, huku watu hao wanajua kuwa hawezi na kwa hiyo hapaswi kupewa ridhaa, na sisi tunajua kuwa hafai, na tukakubali tukampa hiyo ridhaa kwa ushindi wa kimbunga, basi watu hao watatudharau sana.
 
Haya Uyasemayo ni ya kweli na mbaya zaidi yanaumiza unapofahamu ukweli ilihali huna pa kuurekebishia.

Tuambie basi ridhaa hiyo tumpe nani safari hii? Tupe alternative
 
Haya Uyasemayo ni ya kweli na mbaya zaidi yanaumiza unapofahamu ukweli ilihali huna pa kuurekebishia.

Tuambie basi ridhaa hiyo tumpe nani safari hii? Tupe alternative

Swali zuri na mwafaka.
Sio lazima yeye ajibu, mdau yeyote mwenye jibu atupatie tafadhali.
 
Haya Uyasemayo ni ya kweli na mbaya zaidi yanaumiza unapofahamu ukweli ilihali huna pa kuurekebishia.

Tuambie basi ridhaa hiyo tumpe nani safari hii? Tupe alternative

Wala hata usiwe na wasi wasi, wakati mwafaka ukifika watajitokeza tena wengi tu na tutaweza kuwapima kwa matendo na maneno yao. Kwa nini hawajitokezi kwa sasa ni swali linaloeleweka kwani hii ni Tanzania nchi inayodaiwa ya amani na utulivu - bahati mbaya hivyo vitu viwili haviliwi na kwa maana hiyo havitulizi njaa. Tuna watu milioni zadi ya arobaini, tutakosaje wa kumpa hiyo ridhaa ? Wapo kede kede !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…