NYERERE:MWALIMU WA UZALENDO

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,685
1,111
Kwanza Mwalimu alifikiri Tanzania kuapata Uhuru
Alifanya makubwa sana kwa Watanzaniaaa.....
Wanjiwaaa wanjiwaaaa aaaaaaah....x2
Tanzania oyeeeeee
Alikwenda mpaka UNO na siasa yote akaimwaga
Alifanya makubwa sana kwa Watanzaniaaa..

Huu ni wimbo wa ukombozi baada ya Uhuru ukiashiria harakati za Watanzania kujikomboa toka kwenye mikono ya wakoloni. Kwa kuzingatia juhudi za Mwalimu,tulijengeka kuipenda nchi yetu,kwa kuwa harakati za Mwalimu hazikulenga ubinafsi bali mapenzi kwa taifa na nchi yake.

Kutokana na falsafa hii ya kudai Uhuru kwa njia ya hoja bila kugombana na kupelekea wakoloni kuelewa umuhimu wa hoja zetu na umuhimu wetu wa kujiongoza wenyewe, tarehe 9 December 1961 hatimaye juhudi za Mwalimu na wapigania Uhuru wenzake zilifanikiwa na Tanganyika kupata Uhuru wake.

Haikuwa kazi rahisi kujenga nchi kwa misingi yenye kuleta umoja wa kitaifa kwa nchi yenye makabila zaidi ya mia moja,lakini hatimaye Tanzania ikawa nchi yenye kuheshimu misingi ya haki na usawa wa binadamu kwa kubali changamoto zilizolifikisha taifa hapo.

Mwalimu alimaliza awamu yake kwa mazuri yake na kuomba msamaha kwa mabaya aliyoyafanya,aliishi kwa hofu ya Mungu ndiyo maana alikubali kujikosoa,kukosolewa na kukosoa pia,msingi uliomjenga rais wa awamu ya nne.

Kwa kutambua nguvu ya vijana kutokana na umri aliotumika katika mapambano ya uhuru ,Mwalimu aliweza kuamini katika umoja wao kwa kuwajengea misingi imara ya uzalendo ambayo ikitumika ipasavyo tutalijenga taifa lenye kuheshimika sana duniani. Ndiyo maana akataka kuona vijana wanakuwa waasi wa utawala unaokandamiza misingi ya haki na kukumbatia rushwa.

Watanzania hatukujengwa katika uoga,iweje leo tupandikiziwe uoga kwa kuwa tunatekwa na kutwezwa utu ili kutufumba midomo tusihasi mifumo kandamizi yenye malengo ya kutugawa ili watutawale watakavyo.

Siamini katika mabavu lakini si muumini wa uoga,wakati tunasoma tulifundishwa wimbo wa kiharakati ambao ulitutoa uoga na kutujenga kiimani kuwa wazalendo kwa taifa letu,lakini pia ilinijengea taswira ya kuamini kuwa kilicho na nia njema hakikosi misusuko,kupitia misusuko hiyo tija ya harakati hizo hupatikana na kufaidi matunda yake.

Wasijidanganye kuzungumza umoja na mshikamano wa kitaifa kwa kutupandikizia uoga,Watanzania watakuwa wamoja ikiwa watungumza lugha itokanayo na kutokutishwa kwa mawazo yao kuheshimiwa kama changamoto za ujenzi wa taifa.

Kutuziba midomo kwa kututeka au kutufungulia kesi hakuuwi spirit ya kukemea maovu,mkipunguza mmoja mwetu wataibuka waasi mia moja zaidi wenye kupinga mifumo ya tawala kandamizi zenye mwendelezo wa kutozingatia utawala wa sheria.

Tanzania ni yetu sote,tuna kila sababu ya kusimamia uzalendo kwa vitendo kwa kuhoji kwa kiwango cha juu na kuilazimisha serikali kufuata katiba ya Jamhuri ya Muungano na kusimamia utawala wa sheria.
 
Back
Top Bottom