Nyerere baba" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere baba"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Swahilian, Oct 28, 2009.

 1. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  NYERERE BABA
  Nisaidieni leso, machozi nijifutie.
  Alotabiri ya kesho, hatunaye nikwambie.
  Mwalimu wetu kumbusho, habarize uzijue.
  Nyerere namlilia, natamani anisikie.

  Alimtoa mkoloni, bendera yetu angani.
  Umoja nayo amani,katutoa ujingani.
  Kabila kwetu utani, tukasifika barani.
  Nyerere katupa lugha, nalonga bara na pwani.

  Uongoziwe nchini, tawala bora nadhifu.
  Nahodha huyu makini, mpingaji uhalifu.
  Alojali masikini, kila kona wamsifu.
  Nyerere Baba U wapi, itika nikusikie.

  Ujamaa ulileta, azimio la Arusha.
  Wote tujitegemee, mali wote kututosha.
  Kwa pamoja twendelee, hakuna wa kukatisha.
  Nyerere nifungulie, yapo mengi nikwambie.

  Nimeona niandike,barua hii ifike.
  Maisha yangu upweke. Nchi yote ni ya kwake.
  Nakula yalo mapeke, nyama nzima ala peke.
  Nyerere baba mwambie, wewe ndo akusikie.

  Misingi ulotufunza, wachache wamegeuza.
  Kunguni wanatufyonza, vitini wamejibanza.
  Nchi yazidi kuoza, yatoka nayo mafunza.
  Baba ulo taa yetu, nuru ya wanyonge wote.

  Nyumbayo sasa kificho,wala bila wasiwasi.
  Wajichana pochopocho, wapatiana nafasi.
  Watuzika hali macho, kupunguza zetu gasi.
  Nyerere Baba wa kweli, hukutenga waso mali.

  Tamati yangu sikia, ni mengi ya kwongeya.
  Kwanza msitari pigia, majibuyo nangojeya.
  Suluhu pa kuanzia, kwani nazidi umiya.
  Nyerere kwa nguvu zako, Taifa tukawa sawa.
   
 2. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2009
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Picha ya ajali ya hice daladala ya mwenge tegeta iliyotokea leo majira
  ya saa Tano na nusu leo Maeneo Lugalo na kusababisha Watu kadhaa
  kujeruhiwa wengi wakiwa wanafunzi wa makongo.

  Mmoja wa wa aliyepata majeraha ni mwanafunzi wa makongo ambaye jina
  lake halikuweza kupatikana mapema

  Daladala hiyo iliyokuwa ikitokea mwenge kuelekea lugalo ilitaka
  kuovateki lori lililokuwa linatoka Mwenge liliibana dalada
  hivyokupelekea dereva wa daladala kuiangusha daladala kwenye mtaro.

  Katika jitihada za kuokoa waliyonaswa ndani ya daladala hiyo wanachi
  waliita winchii ilikukuondoa wale waliyomondani lakini kutokana na
  uchakavu daladala hiyo ilimeguka sehemu ya juu ingawa majeruhi waliopo
  ndani walifanikiwa kutoka.
   

  Attached Files:

 3. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Poleni sana wote mliopatwa na ajali hiyo mola awape ahueni, na afya ili tuendeleze mapambano.tuko pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu

  angalizo: Madereva ,abiriria, serikali tuwe waangalifu ili tuepuke haya.
   
Loading...