Elimu 2.0 na Elimu 3.0 vinatupatia mwangaza na ufunguo kwa 'Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania'... Katika hili, ni uono na ufikirifu mifumo tunapata kubaini 'Ujamaa ni Ushirikia' katika jamii yenye kujua ilivyobora na kuongozwa na namna za rohoni na si tu mifumo ya kibinadamu. Chama cha Mapinduzi, ni chama cha kusudi la ajabu kama si kipekee juu ya muktadha wa mapinduzi ilivyo ni 'Liberiti, Kazi na Maendeleo'.... Chama hiki ni chenye kusudi sawa kabisa na ujumbe
'Inuka Uangaze, Nuru yako Ishakuja'... Na hali katika kipindi cha Tumani hichi kimetupa 'somo fasaha' kuhusiana na Elimu 1.0; kujua isivyobora... Binadamu kuishi akitegemea 'mwanadamu mwenzake', iwe mtu ama mfumo mfu ni jambo hatarishi kwa hatma za ustawi na maendeleo... Wanajamii wanaponasibika kuwa ni wenye kujua ilivyo bora, hili litaakisika katika miktadha ya 'machaguo ya kitaasisi, 'matukio', 'jamii' na 'wakati'. Tanzania ni chimbuko la ustawi--ustawi wa kinchi na pia kimanyota... Na basi, siku za mbele, programu zetu na 'kwenda manyotani'--kwenda gizani na kutobozea 'maji ya juu', Ujamhuri wetu wenye kutaamulika utabeba ujumbe wa 'Liberiti Yunivasali', na hali Chama cha Mapinduzi ni shughuli ya kuandaa umma na stawi kwa 'Liberiti Afrika'... Ndiyo, Kwanzania ni jina la nasibu yetu kama taifa ndani ya taifa lingine kubwa tunapomaliza na kuvuka kipindi hichi cha 'Tumaini' kuu. Afrika ni Bara Kisiwa, bara kisiwa kubwa kuliko lolote duniani lililo na elementi zote za kukadirisha mwanzo mkuu kutoka kwenye kutokuwa kitu, lenye ardhi, maji, hali ya hewa na tropiki zote tatu.... Hili kutukumbusha, Muungano wa Tanzania bara na visiwani ni jambo la kutunzwa ili lisijekuwa kitovu cha 'fanusi ibilisi ya utengano' kwa jamii pana ya Afrika... Zanzibar, tayari inayofungua za '
mapinduzi ya Ujamaa'.... linalobaki ni moja: 'kuwa' au 'kutokuwa' hilo ndilo swali.…
'UCHUMI MAMA' na 'Jiometria ya Utendekavyo Maamuzi Jamii' ni
'Ki-Fimbo-tambi-tatu na ki-Bakora' vya mtu wa
KUTOKA, Musa--mtu wa uaminifu katika kuongozea ustawi wa jamii mpya ya watu wa Afrika. Elimu 2.0: Uono na Ufikirifu Mifumo ni 'Ujuzi wa kutegua Vitendawili'; na hivi kitendawili cha Mapinduzi kwa Mifumo na Stawi, 2023 na kusonga, kinasubiri kutenguliwa na Chama cha Mapinduzi. Afrika yote inapojinasibu na 'Tumaini' kwa uono na ufikirifu Mifumo, tuiite ndoto Afrika:
'Ndoto Mama Afrika' -- ilivyo ni "Afrika ya Fedha". Kutoka kwetu kwenye mifumo Babiloni, kuelekea fanaka na ustawi wa 'Ahadi' iliyovyo pia ni
agano la usoshalisti wa Kiafrika, ni kukadirisha 'Sura, Utukufu na Uzima' ilivyo ni 'Liberiti Afrika'; Tutafika 'Afrika Mpya' ilivyo ni '
Atlantisi Mpya' kwa "Liberiti na Harambee". Kwa Elimu 1.0, tulinasibisha bara la Afrika na 'rangi nyeusi' kusema ni rangi ya 'sisi wenyewe'; Elimu 2.0 na Elimu 3.0 vitatupatia mwangaza kubaini ni namna gani 'Afrika Mpya' ni kwa wale wote 'wenye moyo' na 'wenye nia na kustawi ilivyobora'; na basi 'Afrika ya Fedha' ni fahari ya mtu kutoka kokote duniani na hata kupita--atakayependa kwa hiari yake, na wito, kuja kuishi na kustawi ndani ya Bara la Afrika na kudhihiri 'Ukuu wa Roho' dhidi ya 'vina vya tafsiri' vya watu na mionekano yao ya nje... Afrika ya fedha, ni ya 'mtu mweusi' kadri sawa na 'mtu mweupe', ni ya mtu wa njano, mwekundu, kijani ama vyovyote vile ili mradi huyo anajitambua na anatambua 'Mkuki wa Imani ya Utaifa' ilivyo ni Liberiti na Harambee...
SASA, maendeleo ni kujichagulia kupitia fanusi ya mwangaza bora katika UTU.
Mwalimu Kambarage Nyerere na Washirika walitengeneza njia kwa ajili shauri la ‘Mtu na Maendeleo’ kwa ule mwanzo wa Siasa za Ujamaa na Kujitegemea. Kwa kuwa Mwalimu, alikuwa ni mtu wa ‘Tumaini’; msaada wa nje na ndani, alikuwa nao kiroho na akili.
Ni muktadha wa Elimu 1.0, Elimu 2.0 na Elimu 3.0 ndiyo unaweza kutukadirishia vina sahihi vya tafsiri kwa misingi ya jitihada zake—dhamira, azma na maono. Kwa hivyo, ipo namna tunaweza kubaini hata yale ambayo watu, kwa muktadha wa Elimu 1.0 wanaweza kudhani ‘alikosea’--kuhusiana imani na misingi ya siasa za chama kimoja, ‘Azimio la Arusha’ na ‘Sera za siasa ya Ujamaa na kujitegemea’, Je, Mwalimu alikosea kwa hayo?
++++
View: https://www.youtube.com/watch?v=8IYbv0bW43w&list=LL&index=29&t=522s&pp=gAQBiAQB
++++
Tabasuri ya Elimu 2.0 inatupatia topografu za kutangamanisha mashauri kwa hata topolojia ufikirifu kuwa: labda Mwalimu Nyerere hakukosea hasa juu misingi ya tawala ya dola ya chama kimoja, na tena Azimio la Arusha lilipopelekea sera za Ujamaa na Kujitegemea na baadaye Katiba ya mwaka 1977; ila ilikuwa ni mgongano wa ‘kiufahamu, akili, upeo, utayari, mifumo’ kwenye nasibu ya kukadirisha ‘ushawishi’ katika akili ya umma—umma uliokatika mapambano kati ya ‘nuru’ na ‘giza’ vyenye kudhihiri kwa sura fundamentali ya ‘Ujinga, Umaskini na Maradhi’; sura ambayo pia ni inaweza kudumishwa kwa namna moja ama ingine na mifumo mibovu ya ‘ukoloni wa ndani’ ama/na ‘ukoloni mamboleo’ katika nchi-dola, ndani ya utamaduni globali.
Kwa muktadha wa Elimu 2.0, ipo topografu moja ya ubayanifu -- topolojia ufikirifu 2.0 kadiri kana kubaini kuwa: hata kukiri kwake kidhamira kuhusu ‘makosa’ ndiko kunaleta/kulileta fasaha ya yeye kupambanua na kujipambanua na adha ya haya yote ilivyo ni ‘Nia thabiti’ kwa fasaha ya ‘Vitendo/Matendo’ na ‘Jiometria ya utendekavyo maamuzi jamii’. Kwa kuwa kupitia jiometria ya utendekavyo maamuzi jamii, rizayati juu ya ‘utashi na maendeleo’ ndiyo hukadirika sura—ukirifu wake Mwalimu kwa kusema maendeleo si majengo na kazi za utumwa; unaweza kumpelekea punda penye maji, lakini hauwezi kumlazimisha yeye kunywa. Kiufundi, migongano ya kijamii inaweza kusuluhishwa kwa ‘fanusi’ ya ‘alama za umoja’, ambavyo hata Elimu 1.0 hubayanisha kuhusu jamii na mashauri yenye kuchanganua habari za fanusi-jamii, nadharia migongano na muingiliano wa alama oanifu.
Utashi na Maendeleo ni shauri la Wananchi wenyewe, ikiwa wanalo jukwaa sahihi kwa ajili ya kuwakilisha matamanio yao na uzalendo wao kwa nchi-dola na mustakabali wake. Mwalimu Kambarage alipozungumza ya Maendeleo kuja kwa misingi ya ‘Elimu’ na ‘Ufanyaji-Maamuzi’ alikuwa analeta ‘shauri-mbegu’ kwa jiometria ya utendekavyo maamuzi jamii. Topolojia ya haya ndiyo inatutaka tusawiri dhana za ‘matamanio’ , ‘uzalendo’, ‘Utashi’ na ‘Maendeleo’ kulingana na wanajamii/wananchi na muktadha wa tawala na ustawi.
MATAMANIO-UZALENDO-UTASHI-MAENDELEO
Kwa zana ya fremu-kazi ya Uono na Ufikirifu Mifumo, Elimu 2.0 inatupatia topografu na topolojia kwa tabasuri ya ‘matamanio’; kwamba ni kitu tunachoweza kukikadirisha kwa ‘vekta ya
Kujisikia’ na ‘vekta ya
Ushawishi’. Jamii ya watu ni mjumuisho ya watu wenye ‘mawazo’, ‘hisia’ na ‘kiu/hamu’ viwezavyo kukadirisha ‘Vekta
Muundo’. Namna hii, kwa mfano, ndiyo tunaweza kupata dhana na tafsiri ya ‘Taifa’ ilivyo ni ‘Taasisi’; muktadha wa wanajamii katika taifa hukadirika topografu ya ‘Nchi-dola’ kama ‘Muundo-tawala dunia’ kwa wakati. Kwa topografu ya nchi ya Tanzania, namna hii yawa basi ndiyo msingi wa fasili zilizopo katika
Utangulizi-- ‘Sehemu ya Kwanza’ ya >
Katiba< kuhusu ‘Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.’
1. Kutangaza Jamhuri ya Muungano.
2. Eneo la Jamhuri ya Muungano.
3. Tangazo la nchi yenye mfumo wa Vyama Vingi.
4. Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi.
5. Haki ya kupiga kura
Kwa zana ya fremu-kazi ya Uono na Ufikirifu Mifumo, Katiba ni chombo kinachokadirisha ‘vekta ya
Mwongozo’. Kwa kuwa kwake hivi, ni ‘vekta
Nia’ na ‘Vekta
Vitendo’ hukadirisha ‘
Sura na Mienendo wa jamii ilivyo ni Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania; ambavyo ‘Nia’ na ‘Vitendo’ katika kuukadirisha sura na Mienendo ya JMT ndiyo hutajwa katika
Utangulizi--‘Sehemu ya Pili’ ya Katiba yetu:
6. Ufafanuzi.
7. Matumizi ya Masharti ya Sehemu ya Pili.
8. Serikali na Watu.
9. Ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea.
10. [Imefutwa na Sheri Na. ......... ibara ya ........].
11. Haki ya kufanya kazi, kupata elimu, na nyinginezo.
Kwa zana ya fremu-kazi ya Uono na Ufikirifu Mifumo, katiba ni chombo kinachotupatia fremu-kazi ya ‘vekta
Mfumo’--mifumo Nchi-dola; na kuwa kwake hivi ndiyo tunapata mwongozo kwa ‘vekta
Ushawishi’ na ‘Vekta
Nia’. Kwamba viwili hivi ndivyo vinakadirisha ‘mipaka ya kiutendaji’ na ‘Wajibu wa mtu/chombo’ katika sura ya tawala na stawi ya nchi-dola.
Ushawishi hukadirisha ‘mahusiano ya kinguvu/uweza’ ambavyo adili ama kusudi la mtu/chombo litajipambanua ndani ya
muundo-jamii, katika ustawi wa wanajamii pasipo ‘kukera’ ama ‘shurti’, fanusi ya ‘
Kujisikia’ katika wanajamii. Na basi ‘
Nia’ ya mtu/chombo ni fanusi ya ‘
Mwongozo’ katika wajibu na
vitendo—jinsi ambavyo mtu ama chombo, kifuatishavyo taratibu zinazokubalika na kurasimishwa na jamii nzima kama taifa lenye serikali na vyombo vya sheria.
Haya, kimsingi, ndiyo hufanya na kukadirisha shauri la ‘Ukuu wa Katiba’ ilivyo ni Utaasisi wa Nchi-dola kwa dhana za Mihimili Mitatu ya Dola—mihimili ilivyo ni vyombo vya kiustawi, maendeleo na utendaji; >
‘Ukuu wa Katiba’ambavyo huweza kuwapa wananchi mamlaka ya kufukuzia mbali ‘serikali’ ikiwa haitendi ipasavyo na ‘matamanio’ ya umma kwa misingi ya ‘haki na usawa’ ambayo wamejiamulia ama kuridhia wenyewe<… Kwenye katiba yetu haya hukadirishwa na tamko lililo ni msingi wa Katiba, katika ‘Utangulizi’, na kisha hubayanishwa sehemu ya muktadha wake kwenye
Utangulizi-- ‘Sehemu ya Tatu’ ilivyo ni maelekezo/mashauri ya mastahikio haki wakati wowote na mazingira yote:-
UTANGULIZI
MISINGI YA KATIBA
KWA KUWA SISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani:
NA KWA KUWA misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na
kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu:
KWA HIYO, BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE MAALUM LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.
HAKI NA WAJIBU MUHIMU
Haki ya Usawa
12. Usawa wa Binadamu.
13. Usawa mbele ya sheria.
Haki ya Kuishi
14. Haki ya kuwa hai.
15. Haki ya uhuru wa mtu binafsi.
16. Haki ya faragha na ya usalama wa mtu.
17. Uhuru wa mtu kwenda atakako.
Haki ya Uhuru wa Mawazo
18. Uhuru wa maoni.
19. Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo.
20. Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine.
21. Uhuru wa kushiriki shughuli za umma.
Haki ya Kufanya Kazi
22. Haki ya kufanya kazi.
23. Haki ya kumiliki mali.
24. Haki ya kupata ujira wa haki.
Wajibu wa Jamii
25. Wajibu wa kushiriki kazini.
26. Wajibu wa kutii sheria za nchi.
27. Kulinda mali ya Umma.
28. Ulinzi wa taifa.
Masharti ya Jumla
29. Haki na wajibu muhimu.
30. Mipaka kwa haki, uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu.
Madaraka ya Pekee ya Mamlaka ya Nchi
31. Ukiukaji wa Haki na uhuru.
32. Madaraka ya kutangaza hali ya hatari.
Kwa tasaburi juu ya maelekezo ya misingi ya Katiba, Elimu 2.0 inatupatia topografu rahisi ya ili kubaini topolojia ya ufikirifu kwa miktadha wa ‘matamanio’, ‘uzalendo’, ‘Utashi’ na ‘Maendeleo’; namna ambavyo hii inasadifiwa kwa mapana jumuishi ya kimashauri juu ya ‘mtu/mtanzania na ustawi’. Kwamba haya yote, katika eneo linalotambulika kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hukadirisha sura na mielekeo ya jamii/taifa yenye kuakisi tunu kuu zilizo ni ‘uhuru, haki, udugu na amani’.
Jambo hili kuifanya katiba kuwa ni msingi wa sheria zote, mahusiano yote, kujaliana na kutosumbuana ndani ya mipaka ya nchi. Lakini kumbe pia, namna hiyo hiyo kuhakikisha usumbufu wa namna yoyote ulioni nasibu ya kutokea nje ya mipaka ya nchi, wanachi wote wanasimama kama nguvu moja kulinda, kutetea na kudhihiri usovereini wa nchi-dola. Kwamba, serikali inawakilisha wanachi na basi kiuhalisia wa mambo, wenye mamlaka kamili ya nchi ni wanachi wenyewe ama/na wawakilishi wao—wawakilishi, wakati hata wakati, ni watu wenye dhamana za utumishi wa umma kupitia mifumo.
Kiuono na ufikirifu mifumo, haya ndiyo yanaleta wajibu wa wanajamii wote kuzifahamu sheria za nchi, kuwa watiifu kwa vyombo na mamlaka za nchi kwa kuwa mwongozo wa Ujamhuri ni katiba ya watu wenyewe ilivyo ni mkataba kati ya watawala na watawaliwa. Hili ndilo kwa nini hulazimu kipengele cha kuilinda na kuitetea katiba ya nchi ni kitovu kikuu cha kiapo chochote cha utumishi/uwakilishi katika chombo cha mamlaka kwa niaba ya umma.
Elimu 2.0 ndiyo inaweza kuwapatia wanajamii ‘vina sahihi vya tafsiri’ kufaa muktadha wa maingiliano ya utendaji, haki na ustawi wa jamii. Uzalendo ni kuwa na imani na Ujamhuri kupitia misingi ya katiba. Imani ni fanusi ya ‘
Nia’ ambavyo kukadirishwa na Mizania ya ‘
Kujisikia’ na ‘
Vina vya tafsiri’ katika mwanajamii kwa wakati. Katika jamhuri, kuridhika ama kutoridhika kwa mwanajamii hutafsirika kivitendo kwa ushikiriki wake kwenye ‘siasa za nchi’; na hasa hasa katika shughuli na utaasisi wa uchaguzi/upigaji kura.
Utashi ni zao la ‘Kujitambua’, ncha OX katika fremu-kazi ya uono na ufikirifu mifumo; ambavyo huu huleta dhamira ya ‘uzalendo’ kwa yule mwenye kujua ilivyobora. Kwa topolojia ya kukagua na kuyaagua matatu,
Nia-Kujisikia-Vina vya tafsiri, muktadha wa uzalendo wa mtu unaweza kubayanishwa. Uzalendo huleta ‘uwajibikaji sahihi’ katika mifumo ya tawala na ustawi wa nchi-taifa. Uwajibikaji usiyosahihi, kiufundi ni ‘Usaliti kwa Umma’; jambo ambalo huhitaji wanajamii wenyewe wawe macho sana na mifumo yao ya tawala, na wawe na Elimu 2.0 pia rizayati ya Elimu 3.0. Kwa kuwa uwajibikaji usiyosahihi una asili ya mawili: ‘kutokujua ilivyobora’ au ‘mmomonyoko wa maadili ya utumishi/dhamana ya cheo’.
Kutokujua ilivyobora, ni topografu inayobeba topolojia ya ufikirifu kuhusiana na hadhi ya aidha mtu kutokuwa na kumbukumbu ama uzoefu kiutendaji, hivyo kuwa na uwezekano wa kufanya makosa ya namna moja ama ingine bila kukusudia. Dawa ya kutokujua ilivyobora ni NIA na bidii ya kutafuta kujua ilivyobora—kutafuta Elimu na Maarifa zaidi. Ni kwa kusudi hili, mkazo wa Elimu, kujielimisha pia Haki ya kupata elimu vinanafasi ya kipekee hata kwenye maelekezo ya Katiba. Elimu ndiyo huleta ‘Kujitambua’--hasa hasa ikiwa na misingi fasaha na muafaka kwa Elimu 1.0, Elimu 2.0, na Elimu 3.0. Kiufundi, elimu ya madarasa pekee kwa mfano, si ufunguo kamili wa kumuwezesha mwanajamii kujitambua na kutekeleza ‘yote’ ya wajibu wake kwa fasaha na ukamilifu. Elimu rasmi na isiyo rasmi hutengeneza mazingira ya mtu kupata kujitambua na kuwajibika kwa kadiri ya yale aliyona uzoefu nayo. Kwenye vyombo vya utumishi na shughuli, kutokujua ilivyobora ndiyo hukabiliwa kwa mafunzo ya wakati hata wakati na ‘semina elekezi’--pia ujuzi wa tathmini za kiuendaji.
Mmomonyoko wa maadili ya utumishi/dhamana ya cheo, ni topografu inayobeba topolojia ya ufikirifu kuhusiana na hadhi ya ‘kushawishika vibaya’ na basi kujinasibu na makusudi yenye kuharibika kiutendaji na wajibu --kwenye nafasi ya mtu katika jamii. Ushawishi mbovu katika jamii ni ‘mbegu ya uovu’—uovu ni jambo lenye kuleta madhara/athari hasi katika sura na hadhi ya msimamo ama maendeleo ya jamii. Hili litukumbushe, wema au ubaya, ni tafsiri zetu sisi wanadamu; na huwa hivi kwa kuwa jambo jema hutuletea wanajamii ‘kujisikia vizuri/vema/salama’ na wakati jambo baya/bovu hutuletea ‘kujisikia ugonjwa/maradhi/kero/kadhia’. Kwa hivyo ili kuzuia yale kuweza kupelekea athari hasi kijamii, wanajamii hutaasisi vyombo kama ‘Bunge’ na ‘Serikali’ ili kuzitengeneza sheria za nchi, na tena kuzitekeleza. Kuwa kwamba, yale mambo yaliyo ‘rafiki’ kwa ustawi wa umma yanapewa ‘uhai’, na wakati yale ‘yasiyo rafiki’ yanathibitiwa/kutokomezwa ama na kuzuiwa yasijiri katika muktadha wa ‘Matukio-Wakati-Machaguo ya Kitaasisi-Jamii’. Kiufundi,
Sura na Mienendo ya Jamii, iwe hasi ama chanya, ni fanusi ya ‘maadili’; kwa kuwa mwenye kujua ilivyobora, hutenda ilivyobora…
Kwa hivyo, kiuono na ufikirifu mifumo, ‘Haki na Wajibu’ hutengenezewa ‘vina vya tafsiri’ kwenye katiba, na kumbe utendaji wa mwanadamu unahitaji muktadha fasaha wa matendo ili kukadirisha ‘utendaji kwa mizania’; chombo cha kutafsiri, ‘sura ama mwenendo wa jambo la jamii’—ikiwa unakaa ama kwenda kwa ‘sura rafiki’ ama ‘sura isiyo rafiki’ dhidi ya ‘tamko la Ujamhuri’, kwa wakati, ndiyo ‘Mahakama’.
Kwa hivi, dhana ya ‘utekelezaji wa haki’ ni fanusi ya kukinga maadili ya taifa kwa ncha moja; na ncha nyingine ni kulinda nasibu ya ‘utashi juu ya ustawi mwema’ wa kila mmoja wa mwanajamii. Hili ndilo huleta busara ya kila mmoja ni sawa mbele ya sheria; maamuzi ya Mahakama ni ya mwisho japo uhalali wa sheria hufanywa na uwakilishi wa watu kupitia shughuli za Bunge la Nchi.
Wanachi kupitia siasa za Demokrasia ya Kiuwakilishi wanaouwezo wa kujitungia sheria, kuzibadilisha ama hata pia kuzifuta kwa matakwa, maslahi ama/na mustakabali wa nchi yao. Uwakilishi wa watu ndiyo hufanyika kwa shughuli za siasa za nchi; ugombeaji nafasi za madaraka na uwakilishi kupitia uchaguzi, kushiriki katika uchaguzi na ushikaji wa hatamu za uongozi kwa vipindi maalum. Haya ndiyo hukadirsha haki ya kuchagua au kuchaguliwa, kuwajibika katika mifumo ya ustawi na maendeleo, kwa vigezo na masharti yaliyoainishwa katika Katiba—msingi wa ujamhuri kuwa ni mkataba kati ya watawala na watawaliwa kwa ridhaa ya wananchi wenyewe.
Kiuono na ufikirifu mifumo, Utashi juu ya ustawi mwema kwa jamii ni ‘vachu/siha njema’ ya raia mwema. Kwenye fremu-kazi ya uono na ufikirifu mifumo hili ndilo huja na metafizikia ya ‘vinasaba mwili’ ilivyo ni ‘utu’. Na basi ‘Utu’ ni mwendelezo wa fizikia ya mwili wa mwanadamu wenye miguu miwili, mikono miwili, kiwiliwili na kichwa chenye milango tano ya fahamu na vipawa vya akili. Haya kwenye katiba, ndiyo msingi wa kustahikia haki kwa ajili ya ‘usawa’, ‘kuishi’, ‘kufanyakazi’, na ‘uhuru wa mawazo’.
Utendaji na wajibu wa mtu katika jamii na Jamhuri, ndiyo nguzo ya ustawi na maendeleo. Yale matendo yote yaendayo kinyume na dhamira hii ni ‘madhambi’ yanayoweza kutafsiriwa hivi mbele ya vyombo vya sheria; japo kimsingi mtu ‘hana hatia’ hadi pale ‘athibitishwe makosa pasi na chembe ya mashaka’ mbele ya Mahakama.
Kiuono na ufikirifu mifumo, utendaji na wajibu wa chombo cha umma katika jamii na Jamhuri, ndiyo dhamana kwa shughuli za kulinda na kudumisha nguzo ya ustawi na maendeleo ya mtu/mwanajamii/wanajamii. Haya, katika katiba yetu ya JMT, ndiyo hukadirisha mwongozo wa ‘wajibu wa jamii’, ‘masharti ya jumla’ na ‘madaraka ya pekee ya Mamlaka ya nchi’. Haya yanatukumbusha kuzingatia umhimu wa utamaduni kuweka madarakani ile serikali ya kuundwa na taasisi imara ya wawakilishi/watendaji wenye uwezo, umakini, na upeo wa kuyabayanisha maendeleo na ustawi wa umma. Kwa katiba yetu ya sasa, hili ndilo hutajwa kuwa ni siasa za mfumo wa vyama vingi.
Sasa, hapo awali JMT ilikuwa chini ya siasa za mfumo wa ‘Chama Kimoja’; kwa namna hii bado katiba iliyopo ‘inafaa zaidi’ ule umma na siasa za mfumo wa chama kimoja. Hili linaweza kufanyiwa kisomo ama rejea, kubaini namna gani ule ‘utayari wa marekebisho ya katiba kufaa siasa za vyama vingi’ ulitokea katika historia ya nchi.
Kwa hivyo, uono na ufikirifu mifumo, unaweza kutusaidia kubaini ‘hekima yeyote’ katika kutafuta kuelewa ‘kiu ya mabadiliko’ ya katiba katika jamii yetu ikiwa ‘Utashi’ umeongezeka. ‘Rasimu ya Katiba’ iliyotokana na mchakato uliopita wa Bunge la Katiba(2012) unamaboresho yenye kuakisi ‘matakwa mapya kimifumo ya nchi’; topografu za kipekee ni pamoja kujitokeza upya kwa yale maudhui yaliyoipa hadhi na heshima kipekee chama tawala, Chama cha Mapinduzi, mambo kama vile ‘mamlaka ya wanachi’, ‘utu’,’udugu’, ‘ukombozi na umoja wa Bara la Afrika’ n.k.--maudhui haya yanakuwa sehemu ya ‘heshima ya kihistoria na mustabali wa nchi’ kikatiba. Serikali na vyombo vyake kufafanuliwa mwongozo kwa sura na pia utendaji wake mpya kwa ajili ya Maendeleo na Ustawi wa umma; Vivyo hivyo, malengo ya maendeleo na ustawi yanabayanishwa kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kimazingira; ambavyo pia muktadha wenye kukazia ‘Utafiti, Dira ya Maendeleo, Mipango na Utekelezaji wa Malengo ya Taifa’ unakuwepo kikatiba.
Rasimu hii ya Katiba(2012), kimaudhui ya uchumi na maendeleo na msuko wake, umeepa dhana za ‘siasa za ujamaa na kujitegemea’ kwa mashauri mbadala juu ‘watu/kazi/maendeleo/ustawi’; kama vile: “kuimarisha na kujenga uwezo wa vyama vya ushirika ili viwe vyombo madhubuti vya kueneza maarifa, mbinu na zana bora za kisasa katika kilimo, ufugaji na uvuvi ili kuongeza tija katika uzalishaji, kutoa mikopo, kutafuta na kuendeleza masoko ya mazao yao;” pia “kuhamasisha uwekezaji wa pamoja baina ya raia na wasio raia katika miundombinu ya uchumi, uvunaji wa rasilimali na maliasili za Taifa;”. Japo kiufundi, maendeleo ya sayansi, tekinolojia na ubunifu si tu yanaweza kubadilisha sura na mienendo ya watu/kazi/maendeleo/ustawi lakini pia yanaweza kubadili dhana za ‘fedha na mikopo’ kwenye ushirika; ama ‘mitaji ya pamoja kiuwekezaji’ kwenye shughuli za kibiashara. Hili la asili ya ‘Mawezekano ya Mapinduzi ya Kifikra katika mbinu za uzalishaji mali’ ndilo rasimu hii imeepa--imeepa misimamo jasiri juu ya ‘kupambana na ubepari/unyonyaji na ubeberu’ ndani na nje ya nchi; hata kama misimamo hii inawezekana--inawezekana pasipo ulazima wa tashtiti dhidi ya ubepari wenyewe, azma ya kujikweza kiuchumi na basi pia kudindiana kimifumo katika mseto wa jamii ya ‘wanaojua isivyobora’ na ‘wanaojua ilivyobora’.
Topografu ya kumulika kauli: “utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na kutumika kwa manufaa ya wananchi wote na kuzuia unyonyaji wa aina yoyote;’’ kwa mujibu wa rasimu hii ya katiba(2012) ni ‘utata’ kwa yote mawili—dhana za ‘utajiri/mali wa taifa’ na ‘unyonyaji’; kwa kuwa hata hivi leo na kwa katiba tuliyonayo kwa mfano, ‘unyonyaji’ haujaweza ‘kuzuiwa’. Biashara huria leo hii, 2023, kwa mujibu wa sura ya uliberali wa kileo zinaasili ya ulanguzi na pia unyonyaji wakati wote!
Uono na ufikirifu mifumo unatusaidia kubaini topografu ya kwamba ‘katiba’ si kisomo ama ‘ahadi za ushawishi kwa ajili ya kugombea nafasi ya uchaguzi’, mfano wa kuahidi ‘kuwajaza mapesa wananchi’... Japo ndiyo katiba yapasa kuwa ni ‘shauri muafaka’ miongoni mwa wanajamii wenyekujua ilivyobora. ‘Katiba kamilifu’, kiufundi ni muhari kuwepo, kwa kuwa wanajamii wanatofautiana upeo na karama za akili juu ya maisha na mifumo pamoja na vina vya tafsiri zake, basi hata utaasisi ma-mabadilisho ya katiba wakati mmoja hata mwingine bado ni kompromaizi ijayo na ‘maridhiano’ ya kijamii.
Haya yatulete kwenye Shauri la Mwalimu Nyerere kuhusu kusudi la kuanzishwa kwa Chama cha Mapinduzi, 1977. Kiufundi mengi ambayo kwenye Katiba yetu ya sasa(1977) yanayoweza kubainishwa kwamba ni ‘mapungufu’ yalikusudiwa kuja kukamilishwa na ‘shughuli’ ya Chama cha Mapinduzi. Hiki ni chombo kilichokusudiwa kuitengeneza njia kwa uhuru wa ndani wa wananchi, maendeleo ya watu na vitu, pia daraja na jukwaa madhubuti kati ya wananchi na serikali yao. Azma na dhamira ya kukitangaza Chama hiki kama ni ‘mwanzo mpya’ wa demokrasia ya siasa za ujamaa na kujitegemea kuliitangulia hata kule kutoka rasmi kwa Katiba ya nchi ya mwaka 1977.
Elimu 2.0 inatupatia topografu na topolojia za ufikirifu wenye kujua ilivyobora juu ya Utaasisi wa Chama cha Mapinduzi; rizayati ya Elimu 3.0 ndiyo inakamilisha ‘Topolojia muafaka kwa Ontolojia na Metafizikia ya Kuundwa na Kuanzishwa kwa Chama hichi --kilicho ni chombo kwa ajili ya utekelezaji wa siasa za uwakilishi katika Jamhuri ya watu wa Tanzania. Kwa kutumia fremu-kazi ya uono na ufikirifu mifumo, tunaweza kuichambua katiba ya Chama cha Mapinduzi ili kubaini elementi muhimu za kukadirisha ‘Sura na Mwenendo wa Chama cha Mapinduzi’.
Katika fraktali ya ‘
Mpango Mzima’, Chama cha Mapinduzi, kilianzishwa kwa ‘vekta
Dhamira’ ya ‘siasa za ukombozi’ zenye chimbuko la ‘vekta
Vina vya Tafsiri’ kama vilivyobayanishwa na “Azimio la Mkutano Mkuu wa Taifa wa pamoja wa TANU na ASP”; mnamo tarehe 21 Januari, 1977 mjini Dar es Salaam, chini ya uongozi wa pamoja wa Mwalimu Julius K. Nyerere Rais wa TANU na Ndugu Aboud Jumbe, Rais wa ASP. Maazimio yalifanyika kutokana na muktadha wa uono na ufikirifu mifumo juu ‘
Sura ya Nchi na Tawala ya Tanzania’ ambavyo vilipelekea msimamo wa matatu(3);
Mosi, kuvivunja vyama vya TANU na ASP ili kuunda chama kipya kilicho ni ‘Chama cha Mpinduzi’;
Pili, Kuweka ‘
Kumbukumbu-Uzoefu sawa’ juu ya mwisho vyama hivi viwili na hapo hapo kuwa ni mwanzo wa Chama cha Mapinduzi. Kwamba huku hakukuja ‘kutokana na kushindwa kimajukumu’ bali ‘ni jitihada ya kupiga mbele hatua mpya’ ya jambo lile lile la msingi:
Mapambano ya Ukombozi wa Taifa letu na wa Bara la Afrika; na
Tatu, Kuyaendeleza Mapinduzi ya Kijamaa na matakwa ya kwamba: “Chama cha Mapinduzi kiwe ni chombo madhubuti katika muundo wake na hasa katika fikra zake na vitendo vyake vya kimapinduzi vya kufutilia mbali aina zote za unyonyaji nchini, na kupambana na jaribio lolote lile la mtu kumuonea mtu au shirika au chombo cha nchi kuonea na kudhalilisha wananchi, kudhoofisha uchumi au kuzorotesha maendeleo ya Taifa”.
Katika fraktali ya ‘
Uongozeaji Njia/Mapito’, Chama cha Mapinduzi kinasibishwa na ‘Vekta
Nia’, adhimu, ilivyo ni ‘Imani ya Chama’; ambavyo ni matatu katika moja;
Mosi, “Binadamu wote ni sawa”;
Pili, “Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake”; na Tatu, “Ujamaa na Kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru”. Haya ndiyo yanasadifiwa katika ‘vekta
Mwongozo’ kama kanuni na taratibu kumi nne(14) za utekelezaji zilizotungwa kwa ajili ya kuongoza shughuli mbalimbali za Chama cha Mapinduzi. Na basi matendo ya Chama kwa kadri ya ‘vekta
Vitendo’ ndiyo yale makusudi kumi na tisa(19) yenye kukadirisha Malengo/Shabaha za Chama cha Mapinduzi.
Katika fraktali ya ‘
Utengeneaji’, Chama cha Mapinduzi kina ‘vekta
muundo’ ilivyo ni muundo wa ‘Wanachama na Viongozi’ katika ngazi na safu mbalimbali za utendaji; wenye majukwaa ya mashauriano, maamuzi, utekelezaji wa maagizo ya Kichama. Namna hiyo hiyo, hadhi ya utaasisi wa Chama cha Mapinduzi hukadirishwa na ‘vekta
Ushawishi’ ilivyo ni wajibu wa kila mwanachama ndani ya uhai wa Chama; uenezi wa itikadi ya Chama ni ‘maneno na matendo’—mtu/mwanachama kuwa mfano halisi wa maneno na matendo yake kwa kuielewa na kuitekeleza siasa ya Ujamaa na Kujitegemea; hili ndilo linakadirisha ‘vekta
Kujisikia’ miongoni mwa wanataasisi wa Chama cha Mapinduzi.
Katika fraktali ya ‘
Uthibiti Sura na Mienendo ya Chama’, Chama cha Mapinduzi kina ‘vekta
Mfumo’ ilivyo ni shughuli ya ‘kushika hatamu’ kadiri ya ilivyopambanuliwa ki-’
Dhamira-
Mwongozo’ na ‘
Vina vya tafsiri-Kujisikia|Hamasa ya Chama’ kuelezwa dhahiri katika azimio la kuanzishwa kwake:
“
Chama tunachokiunda tunataka kiwe chombo madhubuti katika muundo wake na hasa katika fikra zake na vitendo vyake vya kimapinduzi vya kufutilia mbali aina zote za unyonyaji nchini, na kupambana na jaribio lolote lile la mtu kumuonea mtu au shirika au chombo cha nchi kuonea na kudhalilisha wananchi, kudhoofisha uchumi au kuzorotesha maendeleo ya Taifa;
Chama tunachokiunda tunataka kishike barabara hatamu za uongozi wa shughuli zote za umma kwa maslahi ya Wafanyakazi na Wakulima wa Taifa letu;
Chama tunachokiunda tunataka kiwe kiungo kati ya Wanamapinduzi wa Tanzania na Wanamapinduzi wenzetu kokote waliko.”
SASA, Ni Uono na Ufikirifu Mifumo wenye ‘Njia’ ya katika sura na jitihada za kujisahihisa na kitaasisi na mifumo kwa taifa letu la Tanzania. Kuzingatia nasaha na ushauri wa Mwalimu Kambarage Nyerere, siku ya ufunguzi wa Chama cha Mapinduzi, 1977, kuanza kwa chama ilikuwa ni mwanzo wa ‘Huduma’; kwamba watu wamadaraka ni watu wa dhamana ya uwakilishi kwa makusudi ya ustawi na maendeleo wenye kuazimia ‘Uhuru wa Ndani Hasa wa Nchi’ wa nchi sovereini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ikiwa watu wenye dhamana wataonekana hawafai mbele ya macho ya umma wa Watanzania, basi ni wanachi wenyewe wanaweza kuwaondoa hawa madarakani ili kuwaweka wale wenye ‘Nia Njema’ na ‘Moyo wa Utumishi’ wa Umma.
Siasa za Ujamaa na Kujitegemea, kiuno na ufikirifu mifumo hazitengemai katika jamii kwa sababu za kuwepo kwa ‘Chama’ ama/na ‘Serikali’ yenye kujitangaza kuwa ni ‘Taifa la kimapinduzi ya Kijamaa’. Kwa Elimu 2.0 yenye rizayati ya Elimu 3.0; ‘Ujamaa’ wa kweli katika sura na mwenendo wa jamii ni mithili ya topografu ya ‘Metamofosia’ ya ‘Kiumbe Hai’. Topolojia ya ufikirifu 2.0 kwa metamofosia ndiyo kuakisi sura na mienendo ya uhai wa kiumbe ambacho, wakati mmoja, chawa hivi na mwingine kuwa vile; kwa mfano, Yai kuangua na kuwa lava; lava kukomaa na kuwa Buu; Buu; Buu kungamala hadi ‘Kipepeo’ kujitokeza kutokea kwenye gamba la Buu… Kwa taifa letu la Tanzania, Siasa za Ujamaa na Kujitegemea ni fanusi ya maisha na safari ya ‘Kipepeo’. Ujamhuri ulitaamulika, ni fahari Kipepeo iliyo ni ‘vinasaba metafanusi’ kwa ‘furaha’, ‘Uhuru’, ‘Upekee’ na ‘Uinosenti wa Utu’.
Jamii mabadilikoni, katika jicho la watu wa mwangaza, ni sawa na bustani. Watunza bustani ni wananchi wenyewe, lakini chini ya uangalizi wa ‘Malaika’; Jamii iliyotaamulika—iliyofanikiwa kuvuka kipindi cha Tumaini, hufikia fahari ya kuifahamu ‘lugha ya wanadamu na malaika’. Kwa hivi, kupitia fremu-kazi ya uono na ufikirifu mifumo mtu anaweza kufanya kisomo kwa jamii yoyote—iwe Duniani ama kwenye Sayari nyingine; na kuweza ‘kutafsiri’ elementi za ‘Sura na Mienendo’ ya jamii. Ikiwa ujuzi wa hili unakuwa na wananchi, basi uwezo unafanyika kwa wao kuwa na ‘hekima na busara’ juu ya ‘bustani zao’.
Kiufundi, ‘siasa safi’ ni muhari kuwepo ‘wakati wote’—jamii kuwa pamoja ni shughuli na harakati za kujenga muafaka juu ya sura na mwendendo wa jamii’. ‘Uongozi Bora’ si jambo la madaraka kwa kujitenga katika jamii. Kwa kuwa kiuno na ufikirifu mifumo, uongozi ni kufanya maamuzi na kuongozea njia katika kudhihiri mabadiliko ya sura na mwenendo wa jamii. Ikiwa kwa mfano, tunakwenda kufanya Elimu 2.0 na Elimu 3.0 ni fikio la wengi miongoni mwa wanajamii; sura za kisiasa, uchumi, usoshali na utamaduni zinakwenda kubadilika katika taifa na nchi. Metamofosia katika ‘Kujisikia’ ndiyo itakwenda kufanya mawezekano ya ‘panga/pangua’ ya taasisi na mifumo ya jamii. Vitu vingi vitakwenda kubadilika -- tunayoyafahamu na kuyafuatisha kivitendo leo kama ‘Sheria’ yatakoma, ama kubadilika kabisa. Hili litukumbushe, kuna hata mambo ambayo leo hii tunaweza kujinasibu nayo ‘kimkakati ama/na mikataba ya kimataifa’ kutokana kutokujua kwetu ilivyobora, kesho si tu mambo yatabatilishwa kwa raha—yanaweza kubatilishwa kwa uchungu. Uchungu huo kuwa ni ‘Ubatizo’ wa ‘Maji ama/na Moto’. Kwa hivyo, ni
raha|huzuni ‘huleta watu pamoja’ na
maumivu|Uchungu ‘husambaratisha watu’ -- ilivyo ni ‘metamofosia’ za kimaendeleo na ustawi. Hili kuwa basi, fanusi ‘Malaika’ ni usentienti wa ‘
akili-hisia-imosha’ na ‘
akili-fikara adilifu-intuji’. Hili leo hii, kwa misingi ya Elimu 1.0, tunalifahamu kwa ‘juu juu’ kama mashauri ya ‘Amani’ ama/na ‘Mshikamano’ wa kinchi. Kufikiri hili labda linaweza kuwa mikononi mwa vyombo vya nchi-dola, kama maarifa ama/ujuzi wa kukusanya taarifa za kisogoni kwa ajili ya ‘kudumisha utawala’ --kwa afisi kuu ya tawala na mikakati ya kutumia ‘mhimili wa nne’ wa nchi-dola ili ‘kuchezea akili na hisia’ za ‘umma usiyojua ilivyobora’...
Makusudi yenye kuharibika katika Mtu, katika ‘UTU’, daima ndiyo kifunguzi cha ‘Nia ovu’ katika muktadha wa maendeleo na ustawi wa umma. Wanadamu wote tu ni wepesi wa kujichanganya kwenye ‘nia ovu’--kwa kuingia katika ‘vishawishi’. Katika ulimwengu wa Uhuru, utashi ni ‘kujichagulia fungu’ la kupata ama kukosa kilichobora kulingana na upeo wa akili na mazingira rafiki/yasiyo rafiki kwa maendeleo na ustawi binafsi. Mwalimu Kambarage Nyerere alivyoasa wananchi wawe macho na chama chao, chama cha wananchi, Chama cha Mapinduzi, alikuwa katika ‘Nia njema’ ya kulijenga taifa la watu ‘wanyoofu’ wa ‘waadilifu’. Unyoofu na uadilifu ndiyo nguzo ya ‘Chama’ na ‘Serikali’ kwa sura na mienendo ya ‘tabia rafiki’ kwa ajili ya ‘Haki na Usawa’ katika Taifa. Uadilifu wa mwanachi ama/na mtumishi ni kuhakikisha yale yenye ‘enzi’ kwa ‘maendeleo na ustawi wa taifa’ yanatuzwa na kuzingatiwa wakati wote. Ikiwa, kitaifa, tumeazimia ‘Siasa za Ujamaa na Kujitegemea’ basi ni wajibu wa kila mwananchi kutekeleza haki na wajibu wenye kukadirisha muelekeo wa taifa la Kijamaa na Kujitegemea’.
Makusudi yenye kuharibika katika Mtu, katika ‘UTU, ndiyo kile tunachoweza kukikadirisha kuwa ni muktadha wa ‘Rushwa’--ilivyo ni kile tunachokitaja kwamba ni adui wa ‘Haki’. Miiko ya ‘Chama’ na ‘Serikali’ ipo kwa ajili ‘kuratibu’ mienendo ya kitabia za watumishi na pia watu wa madaraka. Kwenye fremukazi ya uono na ufikirifu mifumo, miiko ni muktadha wa ‘vinasaba-vyombo’ ambavyo huwezesha watendaji kuwa na kadiri ya sura ya uadilifu kwa ‘mipango na mapito’; basi ndiyo kusema pia, ‘utekelezaji wa mapito kwa ajili ya Maendeleo na Ustawi wa Umma’. Kila nchi dola ina ‘Miiko’ kwa asili moja ama ingine, na ikiwa miiko hii ‘haizingatiwi’ taifa la watu ni lenye kuelekea ‘kuzorota’. Kwa watu wa Mwangaza, viashirifu vya uzorotefu wa taifa, huwa bayana kwa visomo 1.0 juu ya mazingira ya ndani na nje ya nchi-dola, vinavyofuzu Elimu 2.0 na Elimu 3.0 ilivyo ni kadiri ya ni usentienti wa ‘
akili-hisia-imosha’ na ‘
akili-fikara adilifu-intuji’. Kwa hivyo, ‘ulinzi halisi kwa maendeleo na ustawi wa mataifa’ hauko na vyombo vya kawaida vya nchi-dola hasa, bali na fanusi ‘malaika’ ambavyo wakati mwingine hutenda na sambamba na wale wenye ‘nia njema’ na ‘wito’ katika ‘wakati sahihi’. Kiufundi, mtu yeyote ni ‘mdau’ wa ‘ulinzi kwa maendeleo na ustawi’ ikiwa ni muaminifu kwa ‘akili’ na ‘moyo’; na anafikiwa wakati wowote na ‘malaika’ ifaavyo kwa ‘Matukio-Wakati-Machaguo ya Kitaasisi-Jamii’.
Kuanza kwa shughuli ilivyo ni taasisi ‘Chama cha Mapinduzi’, kwa watu wa Mwangaza, Mwalimu Nyerere kuwa ni Shahidi wa haya, ilifahamika fika kuwa ni mwanzo wa ‘jamvi la wavu’ lenye kutupwa kokoroni baharini. Hili litavuwa yote, halali na haramu—fumbo la imani likabakishwa, Je, ni nani atakayekadirisha ‘manufaa’ ama ‘hasara’ ya kuutanguliza uvuvi huu tuliouita ‘siasa za ujamaa na kujitegemea’ katika Taifa changa? Hichi kilikuwa ni kitendawili ambacho ‘mji ulikwisha kutolewa’ ikiwa wanachi wanashindwa kukitegua. Majibu yake yako dhahiri kwa mtu wa ELIMU 1.0, ELIMU 2.0 na ElLIMU 3.0…
Chama cha Mapinduzi kilianzishwa kwa kupambanua muktadha wa maendeleo na ustawi kama kama chama cha wananchi—walio ni ‘Wakulima na Wafanyakazi’. Hili lilikuwa ni ingilio la ‘akitipu jamii’ kwa mujibu wa ufundi wa ‘metamofosia’ ya ‘akili-hisia-imosha’.
Kwa mtu wa Elimu 2.0 anaweza kutazama ile topografu ya Kisa cha Maisha na Huduma ya Yesu kule Mashariki ya Kati. Yeye alizaliwa katika jamii ya ‘Wakulima walio wengi’, pia ‘Wavuvi’ na ‘Wajenzi’; alikuwa ni Mtu wa Nyumba ya Seremala/Mjenzi/Mwashi. Watu wake, Wayahudi waliowengi, wanajamii ya Galilaya, walikuwa chini ya Utawala wa Kijeshi wa Dola ya Rumi; hawakuwa huru ‘kisiasa’ na ‘kiuchumi’ na tena kulikuwepo na vuguvugu la ‘ukombozi’ daima katika umma wake kukadirisha Wayahudi Watamaduni wenye milengo ya makundi kama Masadukayo, Mafarisayo, Mangangari na Wa-eseni. Kulikuwa na ‘unabii’ wa Maona wengi wa zamani kuhusu kuja/kuzaliwa kwa‘Masiha’--mtu wa ‘ukombozi’. Sasa, kilichotokea kwake Yesu, ni ‘walio wake’ kijamii kumkataa isipokuwa ‘kwa wachache’ wenye ‘Roho ya Ushindi’. Kwa hivyo, ni muhimu kuipatia jamii ‘nyenzo’ kwa ajili ya kujikwamua kiufahamu juu ya mambo ya ‘Matukio-Jamii-Machaguo ya Kitaasisi-Wakati’ kwa ajili ya ‘Utashi’ wao kujiamulia mustakabali wa maendeleo na ustawi wao—ikiwezekana, katika wakati muafaka, hili lipitilize shughuli ya ‘taasisi za kuvusha muktadha wa maendeleo na ustawi wa umma kwa mifumo ya imani za kimakundi’.
Elimu 2.0: Uono na ufikirifu mifumo unatupa Hekima na Busara juu ya akili ya kutegemea ‘Masiha’ ilivyo ni mushkeli. Mtu anapoishi katika ustawi wa kimateka ama utumwa na huku akiendekeza akili ya unyonge na kuwa muhanga wa mifumo, kumtarajia ‘mkombozi’; huyu anaweza kuteseka kwa kujipendea yeye mwenyewe, pasi kujua—ama kujua isivyobora. Mifumo yote ya maisha duniani, ni matokeo ya figisu za kibinadamu na tabia zake—pia metafizikia yake. Ikiwa wanajamii wanaomuktadha bora wa elimu na kujitambua, mifumo inayowavuna ujinga wanajamii kulingana na misingi ya
Kujisikia, kuchochea Hofu na kujihami kwa mfano, itayeyuka. Kiuono na Ufikirifu mifumo, Mifumo yote inayowafunga wanadamu na hofu hufanyika kwa ufundi na utundu wa kucheza na mifumo ya usadikifu – kuzitawala fikra za wanajamii kwa kule kutishia mustabali wao wa maisha ya dunia ama hata kupitiliza duniani—iwe kwa kheri fulani, ama vipi.
Chama cha Mapinduzi, kiliasisiwa kwa hekima, busara na tahadhari kubwa kisije kuja kuwa ‘dubwana la kusujudiwa’ na umma kwa hofu—kwa kuwa ikiwa hali ingalifikia hivi, ni ishara ya muelekeo usiofaa wa maendeleo ya watu na ustawi wao, na kukengeuka kwa maadili ya Taifa. Ukengeufu wa maadili ya Taifa si suala gumu kulibaini kwa ‘mtu wa Njano ya Dhahabu’; linafahamika kwa ‘watu wa nyakati’ pia ilivyo ni ‘Fanusi Malaika’ ya jaala na mustakabali wa Jamii Tumaini—Jamii Mabadilikoni. Kwenye nembo yetu ya Taifa, haya yote yako dhahiri kwa mtu wa Elimu 1.0, Elimu, na Elimu 3.0. Pembe za Ndovu ni uashirifu wa ‘Akili Tiba na Kinga’ kwa maendeleo na ustawi wa umma ambavyo huwa na mizizi ya miiko ya Taifa kwa ajili ya yote mawili: msimamo wa ‘Mali Akili’ na ustawi wa ‘Tunu za Utaifa Jipya’.
Chama cha Mapinduzi, kiliasisiwa kwa Hekima, Busara na tahadhari kubwa kisije kuwa ‘dubwana la udhalimu’ kwa umma wenye kulazimishwa; kuwa kana kwamba watu wa madaraka ya Chama ndiyo wajua ilivyo bora kuliko wananchi kwa yote na kila kitu. Kwa kuwa ikiwa hali kufikia hivi, lile kusudi la ‘uhuru wa ndani’ wa nchi u ni wenye kufifia na basi maendeleo ya watu na ustawi wao kuwekwa rehani kwa mifumo ya kidhalimu ‘ilivyo kwa namna za dhahiri’ ama ‘kwa namna za kujificha’, na tena basi kukengeuka kwa maadili ya Taifa. Ukengeufu wa maadili ya Taifa si suala gumu kulibaini kwa ‘mtu wa Njano ya Dhahabu’; linafahamika kwa ‘watu wa nyakati’ pia ilivyo ni ‘Fanusi Malaika’ ya jaala na mustakabali wa Jamii Tumaini—Jamii Mabadilikoni. Kwenye nembo yetu ya Taifa, haya yote yako dhahiri kwa mtu wa Elimu 1.0, Elimu, na Elimu 3.0. Pembe za Ndovu ni uashirifu wa ‘Akili Tiba na Kinga’ kwa maendeleo na ustawi wa umma ambavyo huwa na mizizi ya miiko ya Taifa kwa ajili ya yote mawili: msimamo wa ‘Mali Akili’ na ustawi wa ‘Tunu za Utaifa Jipya’.
‘Dubwana la kusujudiwa’ na ‘dubwana la udhalimu’, kwa mtu wa Elimu 2.0: Uono na ufikirifu mifumo ndiyo ‘anti-thesisia’ ya ‘Uhuru na Umoja’. Huu huja kulingana na makusudi yaliyoharibika miongoni mwa jamii wenyewe na viongozi wake, ikiwa ‘Hekima, Umoja na Amani’ yawa ni ‘kiini macho’ kwa uzorotefu wa maendeleo na ustawi wa kweli. Ambavyo, watu wa madaraka wanaweza kujivisha kiburi moto ama baridi juu ya ‘kupoteza njia/uelekeo’ wa kufanikisha ‘Jamii isiyo na unyonyaji, matabaka ya wenye nacho na wasiyo nacho, kudharauliana kwa wazi ama kificho, kubaguana, siasa za hadaa n.k’. Ambavyo, watu wasio na madaraka wanajibeza, wanashikwa na hofu na uwoga, kusahau kuwa mamlaka ya nchi ni yao pamoja na viongozi wao. Ikiwa wananchi wamejisahau wajibu wao na wajibu wa serikali yao; mzizi wa fitina ni ‘mmomonyoko wa maadili ya Utaifa’ na pia muktadha wa ‘mioyo iliyovunjika’...
Mikutadha wa ‘mmomonyoko wa maadili’ na ‘mioyo iliyovunjika’ katika nembo yetu ya Taifa ndiyo husadifiwa ‘dawa’ yake kwa ‘Mwenge wa Uhuru’ katika robo ya juu ya Vesika-Paisisi—Ngao ya Ustawi; na pia ‘Shoka na Nyengo’ katika robo ya pili kutoka chini. Mkuki wa Jaala—Imani ya Uumoja ndiyo alama ya kudumu na kudhihiri kwa ‘Fanusi Malaika’ ya ‘Jamii ya JMT’ ambavyo ‘wakati’ ni jamvi la ufahamu katika >
Nia ya Usingurali< kukadirisha mamlaka, uweza, uwepo wa ‘Sovereini Jumuifu’. Na basi, ni mtu wa Elimu 2.0 na rizayati ya Elimu 3.0 mwenye kuweza kufumbua kitendawili cha ‘Roho ya Ushindi’ kama ilivyowazi machoni pa wanajamii – kuiona kila mahala pa taasisi za maendeleo na ustawi wa umma; kuwakilisha ‘wito’ na ‘wajibu’ wa pamoja na kwa pamoja kulijenga taifa la kinara kwa ‘Uhuru na Umoja’ barani Afrika.
Chama cha Mapinduzi kimerasmishwa, si kwa kubahatisha, na alama ya ‘Jembe na Nyundo’, kwa alama X ilivyo ni uaminifu daima, pia rangi za kijani na njano, kama mwanzo wa safari ya jamii KUTOKA uchanga wa Kitaifa kiuchumi na Siasa kuelekea katika ‘Ujamhuri Uliotaamulika’. Kwa watu wa mwangaza, inafahamika wakati wote—dhahabu haiwi safi hadi ipitia tanuru la moto; Jamii ya Watanzania chini ya hatamu ya Chama cha Mapinduzi ingalijua sura ya awali ya jamii mabadilikoni kwa mawezekano yote ya jamii na watu wake wa madaraka kupatia ama/na kukosea mapito ilivyo ni muktadha wa jiometria ya utendekavyo maamuzi jamii yenye kukadirisha ‘Matukio-Wakati-Machaguo ya Kitaasisi-Jamii’. Kumbe hili linakadirisha sura na mienendo ya CCM 1.0 na CCM 2.0. Ya kwanza haina kinga dhidi ya yale yote tunayoweza kubaini ni muktadha wa vipofu kuongoza vipofu wenzao. Kwa hii tunaweza kubaini viashirifu rahisi vya mmomonyoko ama uzorotefu wa maadili ya Utaifa kwa Siasa za kinafiki, upambe, uchawa, fitina, ufisadi, uzandaki n.k. Ya Pili, daima imekuwa ni kitendawili—lakini uwepo wake ni ‘fumbo la imani’; watu wote wenye nia na mapenzi mapema, wenye kutakaswa, kujitakasa na kutakasa kimifumo na basi ndiyo muktadha wa ‘Fanusi Malaika’ ilivyo ni ‘Bibi na Bwana’ katika nembo yetu ya Taifa.
Watu wa mioyo safi, na dhamira safi—watu wa ‘moto wa utakaso’, ndiyo wadau wa ‘ngano safi’ kutoka katika shamba lenye magugu. Siasa za Ujamaa na kujitegemea haziendani na ulimwengu wa ubepari na ubeberu wa kiutamaduni. Watu wa mioyo safi na dhamira safi kwa ajili ya furaha, Amani na Mapenzi mema Duniani ni fanusi malaika ambavyo Yesu, wakati wa nyakati zake, ni ‘Wateule’-- watu waliyo na ‘Roho ya Ushindi’; kwamba ‘Wanaoitwa ni wengi na hali Wateule ni Wachache’. Kwa hivyo kiufundi, shughuli ya CCM 2.0 ni hasa kukadirisha sura ya maendeleo na ustawi wa umma utoke kwenye ‘akili mushkeli’ ya kusubiri ‘Masihi’ na basi jamii yenyewe ijiongoze na kuzaliwa upya katika UTU. Watu hawatakombolewa na ‘mtu fulani wa kipekee ama vipi kuwepo madarakani’ – wala kukombolewa na ‘chama’ chochote, kwa kuwa wao wenyewe ndiyo ‘Chama’--kila yule mwenye ujasiri wa kuushinda uwoga na hofu za ‘kimifumo mfu’ ama yenye kadiri ya kuelekea kuzorota kimakusudi yake adilifu.
Chama cha Mapinduzi 2.0, ni mbivu na mbichi za kufanikisha maazimio kama yalivyoongozea kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi. Hili linawezekana kwa Umma uliomarika kwa muktadha wa Elimu 2.0 na rizayati ya Elimu 3.0 ambavyo ‘Hamasa na
Kujisikia’ hufuzu kujua ilivyobora na tena ‘Roho ya Ushindi’ kudhihiri katika mwanajamii. Hili linakuja kwa kadiri ya mapinduzi ya kweli kifikra—‘vina vya tafsiri’ kuhusu ujamaa na kujitegemea kuakisika kwenye sura na mwenendo wa jamii/Taifa na basi kukadirisha ‘Uchumi wa Kijamaa’ na ‘Utamaduni wa Kijamaa’. 2023 na kusonga, hili linafungulia njia kubaini ukweli wa Maendeleo ya Watu na vitu kuzidia mbali ‘nasibu zetu za
kushawishika vibaya’ na ‘mambo ya nyakati’ na ‘kujua isivyobora’.
Maendeleo si kutamania Majengo Mazuri na Mabarabara na kujifunga kwa mambo ya siasa, diplomasia na uchumi mbovu wa Duniani. Badala ya muktadha wa matamanio yetu kujinasibu na njia za mkato za uchumi wa fedha/biashara, fremukazi ya uono na ufikirifu mifumo inaweza kutupatia muktadha wa topografu sahihi za maendeleo ya watu na vitu --zinazofuzu na kukadirisha ukweli wa ‘Kujitegemea’. Fedha nyingi, majengo na amari za Duniani si ‘Maendeleo’; vivyo hivyo kufikiri pesa, kwa misingi ya kipato ama/na kodi, inaweza kununua ‘mali’ na ‘maisha bora’ ni ufikirifu mushkeli. Mwalimu Kambarage Nyerere alifahamu haya fika. Simulitali ya ‘Kuijenga nchi’ na ‘kulijenga taifa’ ni jambo lenye asili ya ‘Kazi’ siyo ‘Biashara/sera malishazi za mambo ya nje/Koporetikrasia/Hijimoni za siasa maslahi-taifa n.k’. Hili litukumbushe, TUWE MACHO na mambo ya kutamanishwa na kuhadaika kidiplomasia za uchumi… Wabantu tuna msemo: ‘Siyo kila king’aacho ni dhahabu’ na pia ‘Usione vyaelea, vimeundwa’--Elimu 2.0 inaweza kutupatia maarifa ya kuunda upya muktadha wa maendeleo na ustawi wetu wa Kitaifa; pasipo kuiga njia za msafara wa ‘Mamba’.
Muktadha wa ‘Kutamani Mali ya Mtu mwingine’, kupitia fremukazi ya uono na ufikirifu mifumo kunatupatia mapelekeo ya vina vya tafsiri vinavyoweza kubayanishwa na majaribu ya ‘vishawishi/
Ushawishi’ na ‘
Nia isiyonjema kwa Ustawi wa Pamoja na kwa Pamoja’ wa Jamii. Mifumo mibovu ni chaka la watu wenye makusudi yenye kuharibika; hawa kwa upotofu wa kimaadili na kuzozingatia maadili na madaraka/nafasi zao katika jamii wanazinajisi afisi zao za utumishi wa umma kwa
tabia-vitendo zenye kupindisha misingi ya ‘Haki na Usawa’. Kwa Elimu 2.0 juu ya Ubepari tunaweza kutambua na kukadirisha topolojia ufikirifu juu ya ‘Mizizi ya tamaa ya kuwa na mali nyingi binafsi ama nguvu katika mifumo ya maendeleo na ustawi wa jamii. Juu ya Ukomunisti kwa mfano, tunaweza kutambua na kukadirisha topolojia ya ufikirifu juu ya ‘Mizizi ya Wivu kwa mali maendeleo ya wengine vyenye kuchochea ‘roho za kauzibe’’. Udhalimu kwenye dola ya kibepari ama kikomunisti huinuka kwa matendo na dhamira mbovu za wachache kutawala wengi wakitumia ‘mifumo ya siasa za hadaa’ na huku wakisukumwa na ‘roho-ya-mtaka-vitu’...
Basi ndiyo katika
Katiba yetu, utangamano kulingana na hisia za yale manufaa yajayo kwa misingi ‘mali binafsi’ na ‘mali za umma’ yana mwongozo ilivyo Sheria mama; na tena msingi wa sheria zingine zote mahsusi za nchi juu ya usalama raia na haki zake -- kisiasa, kiuchumi na utamaduni. Kwa muktadha huo shughuli za kila siku za riziki na maendeleo za wanajamii, zinahakikishiwa ‘uhuru’ na ‘haki’ katika ‘kujitafutia/kutekeleza majukumu’ na pia kulinda raia, viongozi na mali zao—kwa mujibu wake. Hili, kishughuli ya kitaasisi, lina insignia ya ‘Shoka na Nyengo’ vyenye ‘Mkuki wa jaala ya Uumoja’, muktadha wa taji la ‘Mwenge wa Uhuru’ na kauli mbiu ya ‘Usalama wa Raia’. Kiufundi, ‘Haki na Usawa’ huinua taifa lolote—dhuluma, maonezi, vitisho, upendeleo ubaguzi n.k huliangamiza taifa. ‘Vitendo-tabia’ visivyo rafiki kwa mbegu ya ‘Uhuru na Umoja’ ni viashirifu vya uzorotefu wa mifumo ya Maendeleo na Ustawi wa Taifa, kwa watu wa mwangaza – Watu Halisi wa Mwenge; kuakisi tafsiri ya unyemelezi wa kuangushwa kwa misingi ya ‘maadili’ na ‘miiko’ ya utaifa – kana usemi:
Hauwezi kupanda pilipili ukajakuvuna parachichi…
Chama cha Mapinduzi 2.0 ni dhamira ya ‘UTU MPYA’ fahari ya ‘Simba’; na si ‘kondoo’ wa matoleo ya kimifumo mibovu. Ni dhamira ya ‘kujitambua na kusimika nafasi yako’ na si kusubiri ‘kutambuliwa’ ama ‘kujitambulisha sifa za kipambe’ ili ‘ukubalike’/kustahiki upendeleo wa nafasi ya kupewa na mwingine. Hili kulisadifu kwenye topografu ya michezo na utamaduni, linashahibiana na ‘Utani wa Jadi’ kati ya Vilabu vya Kabumbu vya Yanga na Simba kutoka ‘Jangwani’ na ‘Msimbazi’--maskani mbili za kutengenishwa na mto Msimbazi. Yanga(Vijana Afrika—Young Africans) daima imewakilisha temperamenti baridi kama udongo, na hali Simba ni ‘hisia za fahari na ukali/moto’. Ikiwa Yanga ni ‘Umoja wa Mataifa’ basi Simba ni ‘Taifa Kubwa’. Tofauti ya Umoja wa Mataifa na Taifa Kubwa/Muungano wa Sovieti za Urusi ni kujipambanua ‘Kiuchumi’ na ‘Siasa’ ambavyo Merekani imepata kuwa hasimu wa Urusi kwa hijimoni za ‘Ukoporetikrasia’ dhidi ya hijimoni za ‘Mabaraza ya Wafanyakazi—Sovieti’. Sasa, siyo bahati mbaya kwamba rangi za bendera ya Yanga zinafanana ni za CCM na hali za Simba hufanana na Sovieti—tena na Nyekundu ya robo ya pili ya Vesika-Paisisi iliyo ni ‘Ngao ya Ustawi’.
‘Jembe na Nyundo’ ni ncha moja ya mkuki-- ya metamofosia ya Chama cha Mapinduzi ambavyo ncha ya pili ni kadiri ya ‘Shoka na Nyengo’. Kimetafo, Chama cha Mapinduzi 2.0 ni chenye maskoti ‘Shoka na Nyengo’ ilivyo ni muktadha wa wanajamii wenyekujua ilivyobora. Wanajamii waliofaulu kuvuka ‘Mto Msimbazi’ kutokea ‘Jangwani’ kadiri sawa na kutokea Msimbazi kufika Jangwani—kuizidi fanusi ya utengano. Chama cha Mapinduzi kilitambulishwa kwa alama ya jembe na nyundo –kwa kuwa ni chama cha wananchi walio wengi ambavyo ni Wakulima kwa Wafanyakazi. Kwenye Muungano wa Nchi za Kisovieti zilitumia alama za >
‘Mundu na Nyundo’< kama insignia kwa ‘nguvu ya umma’. Kiufundi, hizi ni alama za ‘Kimapinduzi’ japo ukweli wake hubakia fumbo kwa umma wa wengi juu ya ontolojia na metafizikia ya alama zenyewe.
Ikiwa mapinduzi ni mageuzi kamili ya kiuchumi, siasa, jamii na utamaduni, haya yatakuwa hatua ya kimetamofosia ya mifumo ya jamii na fahari yake. Mageuzi haya ndiyo yataelekea kukadirisha ‘Jamii ya Dhahabu’ ambavyo ‘Moto wa Uwepo’ – daima kuwaka mahala patakatifu pa ‘Nyumba ya Tawala na Ukuhani wa Nchi’. Raia wake wangalikuwa ni Simba wasioingiliwa nafasi zao za fahari ya Utu na Ustawi. Na basi matatu yangekadirisha muktadha wa fahari ya ‘Jamii yenye Kujua Ilivyobora’--(1) Ushujaa, (2) Uhodari na (3) Umahiri; katika Dhamiri ya Utu, Matendo na Kuheshimiana kwa Dhati.
Chama cha Mapinduzi 2.0 ni shughuli ya muktadha wa ontolojia na metafizikia ya dhamiri ya ‘Kuzaliwa upya’ Kiakili, Mwili na Roho ili kuachana na mifumo ya kinyonyaji, utwana na utumwa ndani ama nje ya nchi—hili si dhahiri katika ulimwengu wa leo; na hali kutokea hapa Afrika Mashariki, jitihada zinafanyika kulifanya hili liwe ‘Hali Halisi’. Hili linakwenda kuwezekana kupitia watu wenye utayari wa ‘kuhama’ –
KUTOKA, katika Mifumo Babiloni ili kufikia muktadha wa Maendeleo na Ustawi wa Kibindamu ulivyo ni ‘
Nchi Mpya, Mtu Mpya’. Pahala pa kuimba “Nitakwenda na Jembe langu, Nitangaze Ujamaa Tanzania Kote”, basi ndiyo kuja kuimba “Nitainuka na Shoka na Mkuki na Nyengo zangu, Nitangaze Ujamaa Tanzania, Afrika na Duniani kote”...
Wanajamii wa fahari ya Simba, ni watu wa kuwa na ile roho ya
Nia yenye Ujasiri kwa kuwa na vitendo-tabia ya kwenda kinyume na
kujisikia hofu mbele ya mifumo ama/na taratibu za kidhalimu; ni watu wa
Nia ya Uhodari kwa vitendo-tabia vyao vyenye kufuzu kutoghairighairi ama/na kutokukata tamaa na basi kukomalia lile ‘walionalo ilivyo bora’; na kuamini njia/mapito yao kuelekea fahari ya UTU katika ‘Haki na Utashi’ ilivyo ni ‘kujiamulia mustakabali wa nchi yao’. Ni watu wa
Nia ya Umahiri kwa maneno na vitendo kufungamanisha nguvu sawa kwa fraktali ya
Uono Fasaha,
Vina vya Tafsiri vilivyo maridhawa na
Dhamira ya dhahabu.
Katika muktadha wa ‘Ndoto Mama Afrika’, mtawala Haile ‘Ras Tafari’ Selassie I wa Ethiopia ndiye alikusudia Afrika Mpya iwe na msimamo unaotokana na >
‘watu wa dhamira ya dhahabu’<--kwamba panapo uhatarishi kwa amani na mshikamano wa jamii, ‘Hoja ya Nguvu’ iwe batili mbele za ‘Nguvu ya Hoja’. Afrika na Watu wake ije kuwa ni jamii ya watu wa jinsi na rangi zote--wasiotawaliwa na ‘mifumo ya imani sadikifu za kimakundi’ zilizo za kigeni; na hali wao wenyewe basi kukosa nguzo za kubaini ukweli wa ‘maisha ya kiroho’. Kwamba ‘Maisha ya Kiroho’ ni jambo la ‘kujitegemea’ katika mtu—mtu mmoja hapaswi kuhoji njia ya mwenzake kwa kuwa hakuna afahamuye kiukamilifu fumbo la ‘Moto wa Uwepo’. Basi dhamiri ya nia juu ya shauri la kutafuta ‘kujua ilivyobora’ juu ya mtu, UTU, maendeleo na Ustawi, ni ‘Safari’ ilivyo ni bidii ya Elimu 1.0, Elimu 2.0 na rizayati ya Elimu 3.0 ambavyo vyote kutegemea na mtu mwenyewe—mtu kutafuta ‘Ushirika na Roho ya Ushindi’ ili njia zake zipate ‘fahari ya dhahabu’ na ‘Ubarikika’.
Renansi Afrika inakwenda kudhihiri kwa >
‘Roho ya Ushindi’< ambavyo >
‘fahari ya Simba’< imetufikia kwa Sanaa na Michezo yenye kutuletea ‘hisia’ na ‘moto mpya’ dhidi ya >
‘Mifumo Babiloni’<. Afrika kuamka na kusimama na kushika mahala pake katika ‘jamvi la usupashi-nyakati’ ni vuguvugu lililoanza nusu ya pili ya karne ya 20—‘wimbo wetu’ kwa >‘Liberiti Afrika’=Afrika Unite< ni ujumbe wa ‘Uhuru na Umoja’. Ni ujumbe huu tutaubeba kwa ‘fahari ya Simba’ hata Angani—kwenye Nyota, ambako mapambano baina ya kiza na nuru ya nafsi yangalikuendelea. Mtu wa nadhiri kwa haya ni ‘Mtu Mtamaduni’ – ni mtu ‘Rasta’ kwa fahari yake kutokutafuta ‘utukufu’ wa fahari za kikondoo na ufikirifu pofu wa kimakundi. Si lazima mtu kuzivaa drediloki ili awe ‘mtu-Rasta’; yeyote mwenye ujasiri, uhodari na umahiri katika dhamira ya dhahabu yeye ni ‘Muafrika’ katika Moyo na Matendo; na hasa ikiwa Bara la Afrika ni mahala ambapo yeye ajichagulia kuwa ni ‘nchi yake’ ya ‘Wito wa Dhahabu’ kuifanya ‘Nchi mpya, Mtu mpya’…
Tutakapofikia ‘mfano bora’ wa jamii yenye muamko na kupiga hatua; itatupasa kuliangalia upya suala la uzalendo na uraia—kulitengenezea vina maridhawa vya tafsiri kwa ‘uhamiaji’ na ‘Ustawi wa Mwanadamu’. Siku za mbele itakuwa ni dhahiri, kuwa ‘Muafrika’ si rangi ya ngozi; ni hamasa ya watu kudhihiri ‘Nguvu ya Roho’ dhidi ya madhalimu ya kinchi na dola yatokanayo na mmomonyoko wa maadili na kutozingatia miiko ya Utaifa wa ‘Haki na Usawa’ kwa Wote--’Roho ya Ushindi’. Afrika itajengwa kwa ushikiriano wa watu kutoka kote—Kaskazini, Mashariki, Magharibi na Kusini mwa bara lenyewe na Jiografia yake.
‘Mfano bora’ ni >
harakati ama/mapambano yasiyo na ghasia<. Iwe ni kwa muziki wenye kuleta watu pamoja ama michezo yenye kuchochea nidhamu, uhodari na umakini, haya ndiyo mambo yakayojiri katika ‘Vituo vyetu vya Utamaduni’ kuelekea Ujamhuri Uliotaamulika. Muziki wa Rege ni ‘Zawadi’ na ‘Tunu’ ya kutangamanisha mapigo ya moyo, ujumi na rithimu ya dhahabu. Tutumie muziki kuleta watu pamoja na kupanda mbegu bora za UTU na wito bora kwa maendeleo ya watu na vitu Afrika na Kupita… Tutumie ‘Sanaa’ kupeleka mbele dhahania za UTU bora, Ujumi na Kujidhihiri utu bora… Tufikishe ujumbe kote, Afrika na Kupita—Ujumbe wa Furaha, Amani na Mapenzi Mema kwa Watu na Viumbe vyote Duniani na Ulimwenguni kote…
Tutambue fumbo ya kile ‘Kilicho ni Khasa’-- asili ya ‘uzima’ wetu na ‘metafizikia’ yake-- ni ‘moto unaowaka pasi kuzima daima na milele’ ndani yetu. Ni moto huu ambao hutujaza ‘Roho ya Ushindi’ kutufanya sisi wote, wenye kujinasibu na dhamira ya dhahabu, kuwa ni ‘Shoka’ lenye kuweza kukata hata mbuyu mkubwa ulioje – mbuyu wa mifumo Babiloni. Sisi kuwa ni ‘Nyengo’ yenye kuvuna manufaa ya ‘mema ama/na mabaya’ yatokanayo na wanajamii ‘
kujijazia mabatili ya nafsi’ --
katika wakati muafaka wa ‘mavuno’.
2023 na Kusonga, ni wakati wa mavuno.
Tuinuke na kusimama pamoja kuifanyakazi.
+++++++
View: https://www.youtube.com/watch?v=qaZ1oFlryeM