Nyerere Anatukuzwa Bure Kama mtu aliyetafuta uhuru Peke yake!

Namheshimu sana Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere, lakini kuna kitu watanzania wengi hawakijui hasa ambao hawajasoma au mwenye uelewa mdogo kuhusu historia ya nchi na siasa!

Ni kweli mwl Nyerere alikuwa na Mchango Mkubwa kwa Tanzania tuliyonayo sasa lakini shida inakuja pale hizo sifa anavopewa yeye Mwenyewe

Ikumbukwe Kabla hata nyerere hajaenda kudai uhuru kwa Malkia Elizabeth kuna watu wa Meru (kwa sasa Arumeru/Meru) walishawahi kwenda kudai uhuru kwa malkia wakakataliwa!

Kuna mtu anaitwa Bibi Titi Mohamed, kwangu mimi huyu ni Honorable Mention maana ni Mwanamke aliyepambania sana uhuru enzi zile!

Tunapomtukuza saana Mwl Nyerere tuwakumbuke na hawa wengine maana haikuwa one man army!

Talented Engineer

TheMason
Nyerere haheshimiwi kama mtu aliyeleta uhuru peke yake. Ila, Nyerere anaheshimiwa kwa kujali maslahi ya nchi kuunganisha makabila yote na kuwa na ideology moja kwenye mapambano ya uhuru. Wameru walienda kudai uhuru walikuwa na agenda zao kama wameru, wachagga nao walikuwa na agenda zao kama wachagga, ila Nyerere aliangalia Tanzania kama kabila moja lenye mahitaji sawa
 
Waliosifiwa sifiwa wote ndio waliowauza watu wao i.e Nyerere, Mandela....

Tena mandela ndo kaiuza nchi yake mchana kweupee mpaka wazungu wakampa tuzo.. bora nyerere aliuza kiujanja ujanja!..walimpa uhuru kisha wakampa sharti awaandalie viongozi puppets!! Kabila, museven, kagame etc etc... mugabe atabaki rais pekee mzalendo amegoma kbs kuuza nchi maisha yake yote mpaka mpaka pale akili yake ilipogoma kufanya kazi sawasawa bado alikua haamini kbs mtu mwingine
 
Namheshimu sana Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere, lakini kuna kitu watanzania wengi hawakijui hasa ambao hawajasoma au mwenye uelewa mdogo kuhusu historia ya nchi na siasa!

Ni kweli mwl Nyerere alikuwa na Mchango Mkubwa kwa Tanzania tuliyonayo sasa lakini shida inakuja pale hizo sifa anavopewa yeye Mwenyewe

Ikumbukwe Kabla hata nyerere hajaenda kudai uhuru kwa Malkia Elizabeth kuna watu wa Meru (kwa sasa Arumeru/Meru) walishawahi kwenda kudai uhuru kwa malkia wakakataliwa!

Kuna mtu anaitwa Bibi Titi Mohamed, kwangu mimi huyu ni Honorable Mention maana ni Mwanamke aliyepambania sana uhuru enzi zile!

Tunapomtukuza saana Mwl Nyerere tuwakumbuke na hawa wengine maana haikuwa one man army!

Talented Engineer

TheMason
Kila jambo lazima awepo kiunganishi,awepo mwenye uthubutu,awepo mwenye nia,awepo mwenye ujasiri wa kujitoa,mwenye malengo,hakuna jambo au kitu kinaweza kufanywa bila kiongozi kikafanikiwa na ndiyo maana kama hawapo wanachaguliwa,kwa hiyo sifa hizo alikuwa nazo Baba wa Taifa,inawezakana walikuwepo wengi kama kiongozi lakini uongozi wake ukaongeza chachu ya uhuru hasa kwa kujua hitaji(uhuru) zaidi la Watanganyika na kuwa na ujasiri wa kuliwasilisha kwa Wakoloni.Lakini kwa akili ya Nyerere hasa kwa tuliopata bahati ya kumshuhudia au kupitia clip ile akili yake ilikuwa balaa na ya upekee.
 
Kiongozi hakuna mtu alokukataza kumtukuza Titi kama mpigania uhuru Nafikiri kesi ya uhaini ya mwaka 1969 ndiyo ilimpoteza japo alikuja pata msamaha baadae.Lakini bado haikuzuii kumtukuza ukipenda.
Wapo na wakina Oscar kambona
 
Watu wengi wanapomsema Nyerere, huwa wanawakilisha wahenga wote.

Mathalani mtu anaimba wimbo unaohitaji "economy of words", anaimba.

"Naye Baba Nyerere ndiye wetu muhifadhi. Naye ndiye aliyeleta uhuru. Tanzania yetu ndiyo nchi ya Furaha".

Hapo ni wazi Nyerere anawakilisha wazee wengi sana waliopigania Uhuru.

Lakini kama mtu ana roho ya ushindani atasema mbona Sykes hajatajwa? Wengine watasema mboma Chifu Kidaha Makwaia hajatajwa?

Unayoongea ni kweli ila Gari lazima liwe na dereva mmoja hata iweje, wengine mautingo tu.
 
Tena mandela ndo kaiuza nchi yake mchana kweupee mpaka wazungu wakampa tuzo.. bora nyerere aliuza kiujanja ujanja!..walimpa uhuru kisha wakampa sharti awaandalie viongozi puppets!! Kabila, museven, kagame etc etc... mugabe atabaki rais pekee mzalendo amegoma kbs kuuza nchi maisha yake yote mpaka mpaka pale akili yake ilipogoma kufanya kazi sawasawa bado alikua haamini kbs mtu mwingine
Well noted mkuu...sauzi wameshtuka saa hizi !
 
Huyo nyerere alikuwa ni Mnafiki ambaye alikuwa anaamini mawazo yake tu ndio yako sahihi na ukija na wazo la kumshauri inakula kwako,Unaweza kupotelea pasipojulikana,Halafu nasikia alikuwa anaitwa Mr.Haambiliki
 
Hakika na mimi huwa nalisemea sana hilo, wapo wazee waliotoa mali zao, fedha na majumba yao ktk harakati za kusaka uhuru lkn hawakumbukwi na wala watoto wetu hawafundishwi juu ya hao mashujaa, kule Kariakoo wapo wazee waligawa mpaka nyumba za familia, wapo wazee waliomhifadhi Nyerere lkn wote hawatajwi kabisa it is just like kuna mtu mmoja alifanya kila kitu peke yake
 
George Washington anaitwa Baba na wamarekani wewe huna sababu nyingine zaidi ya kiimani.
hicho mnacho lazimisha kilamtu aamini kile ambacho amini nyinyi ndio hapo panaleta shida wewe waona nisawa kumuita baba namama yupo wapi? nisawa imani yako inakufundisha hata viongozi wako wadini kuita hivyo usilazimishe nakwangu pia hata mwanangu amwite baba hovyoo
 
Watu wengi wanapomsema Nyerere, huwa wanawakilisha wahenga wote.

Mathalani mtu anaimba wimbo unaohitaji "economy of words", anaimba.

"Naye Baba Nyerere ndiye wetu muhifadhi. Naye ndiye aliyeleta uhuru. Tanzania yetu ndiyo nchi ya Furaha".

Hapo ni wazi Nyerere anawakilisha wazee wengi sana waliopigania Uhuru.

Lakini kama mtu ana roho ya ushindani atasema mbona Sykes hajatajwa? Wengine watasema mboma Chifu Kidaha Makwaia hajatajwa?

Wewe ni mwalimu unajua namna ya kuwaelemisha watoto wenye matatizo ya uelewa.
 
Namheshimu sana Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere, lakini kuna kitu watanzania wengi hawakijui hasa ambao hawajasoma au mwenye uelewa mdogo kuhusu historia ya nchi na siasa!

Ni kweli mwl Nyerere alikuwa na Mchango Mkubwa kwa Tanzania tuliyonayo sasa lakini shida inakuja pale hizo sifa anavopewa yeye Mwenyewe

Ikumbukwe Kabla hata nyerere hajaenda kudai uhuru kwa Malkia Elizabeth kuna watu wa Meru (kwa sasa Arumeru/Meru) walishawahi kwenda kudai uhuru kwa malkia wakakataliwa!

Kuna mtu anaitwa Bibi Titi Mohamed, kwangu mimi huyu ni Honorable Mention maana ni Mwanamke aliyepambania sana uhuru enzi zile!

Tunapomtukuza saana Mwl Nyerere tuwakumbuke na hawa wengine maana haikuwa one man army!

Talented Engineer

TheMason
Mkuu hiyo ni kawaida wala isikubabaisha,kwa kawaida katika maswala ya uongozi anayesifiwa ni kiongozi,na sio watendaji.
Chukulia mfano timu ya mpira wa miguu,kwa kawaida anayesifiwa sana ni yule aliyefunga goli,na sio aliyetoa pass ya goli,wala golikipa ambaye alipangua magoli mengi.
Mfano mwingine tunaelezwa katika historia kwamba Adolph Hitler aliuwa Wayahudi 6,000,000.Unafikiri wote aliuwauwa yeye?
Jibu litakuwa hapana,lakini utawala wake chini ya uongoziwake ndio uliotekeleza mpango ule ovu.
Kwa hiyo,kwa mwl Nyerere hali ni hiyo hiyo,pamoja na kwamba walikuwa wengi,wakati wa harakati za uhuru,wote walikubali kuwa chini ya uongozi wa mwalimu,hivyo anabeba sifa au lawama za kwakena waliomsaidia wote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom