Nyerere alitukomoa katika Elimu watu wa Kigoma

Nyerere alitukomoa katika Elimu watu wa Kigoma

AIR MSAE

Member
Joined
Aug 23, 2016
Posts
22
Reaction score
17
Nikiwa kama mzaliwa na mkazi wa Kigoma nimekulia katika maneno yaliyopata umaarufu kila kukicha kwamba Nyerere alitunyima elimu ili tusimpindue

Katika pitapita zangu nikitafuta elimu niliibuka na haya yafuatayo,

Sio kweli Nyerere alitunyima elimu sisi Waha

Sisi Waha hatupendi elimu iliyopo bali tunatafuta mchawi tumtwike fadhaa hii

Sekta ya elimu katika mkoa wetu ni kitu cha ziada tofauti na mikoa mingine ambayo wameipa elimu umuhimu wa kwanza

Maafisa elimu,waratibu elimu tumewatenga kama wao ndio wana hati miliki ya elimu ya wanakigoma

Kila mkurugenzi ajae halipi uzito suala la elimu kama halimuhusu

Walimu tumetengwa sana ukiachilia mazingira yetu ya ufanyaji kazi

Na ninachokishangaa sasa mmetuletea madawati na kusema tusome bure lakini wanaotoa hiyo elimu wametazamwa vipi

Msipojirekebisha kwa haya sisi waha bado tutaendelea kuamini sababu ya ujinga wetu ni Nyerere na ninyi waendeleshaji mnapitia njia ileile

Nawasilisha
 
Ni kweli aliwakomoeni, kwani hata 'heading' yako hapo juu imekaa vibaya. Ulitakiwa kuandika "Nyerere Alitukomoa Watu wa Kigoma Katika Elimu" na sio "Nyerere Alitukomoa Katika Elimu Watu wa Kigoma"
 
Kigoma mna matatizo kuanzia chini hadi juu,,ninyi wenyewe watumishi pamoja na wananchi wenu hamjielewi nani amwongoze nani
Ulisemalo ni kweli maana hata katika sekta nyingine yote ni yaleyale

Watumishi wanalia na wananchi wanalia pia

Hakuna mkombozi

Ni kama awamu ya 4 kila mtu alikua analia viongozi na wananchi hakuna aliyekua na solution ya matatizo yetu

Ndalichako alikuja juzi juzi lakini pamoja na kumuuliza utatuzi wa kero zetu alionekana kumrushia mkuu kwamba haambiliki

Kilikua kikao cha ndani na walimu
 
Prof Ndalichako Simamia Elimu kwenu Kigoma.
Ukifanikiwa kutoka kigoma hata kama ni mzaliwa hukumbuki kurudi maana tunapajua wenyewe

Kwa udhibitisho angalia wabunge wa kigoma hawarudi hadi uchaguzi mwingine
 
cfa nyngne ya hawa jamaa hawapendi kujitambulisha kabila lao mara nyingi na kwa sababu hawapendanagi wao kwa wao so huepuka kujitambulisha kwa kabila ili kupunguza Mazoea baina Yao yani waha wenzao! Ila wana roho mbaya hawa jamaa Hataree always ni wabishi na wanajifanyaga wajuaji sana na wanasifika kwa roho ya kukunja na hawapendagi mtu mwngne awe nacho awe mha wenzao au hata awe kabila jingine, halafu hawa jamaa ni pretenders wazuri unaweza kuwa na mha ukajua ni rafik yako kumbe hayuko na ww kabisa ila anakuwa anakuigizia tuu
 
Kigoma mna matatizo kuanzia chini hadi juu,,ninyi wenyewe watumishi pamoja na wananchi wenu hamjielewi nani amwongoze nani
Tatizo waha wabishi sana, bora hamjasoma mnewatesa wengine..natania tu
 
Nikiwa kama mzaliwa na mkazi wa Kigoma nimekulia katika maneno yaliyopata umaarufu kila kukicha kwamba Nyerere alitunyima elimu ili tusimpindue

Katika pitapita zangu nikitafuta elimu niliibuka na haya yafuatayo,

Sio kweli Nyerere alitunyima elimu sisi Waha

Sisi Waha hatupendi elimu iliyopo bali tunatafuta mchawi tumtwike fadhaa hii

Sekta ya elimu katika mkoa wetu ni kitu cha ziada tofauti na mikoa mingine ambayo wameipa elimu umuhimu wa kwanza

Maafisa elimu,waratibu elimu tumewatenga kama wao ndio wana hati miliki ya elimu ya wanakigoma

Kila mkurugenzi ajae halipi uzito suala la elimu kama halimuhusu

Walimu tumetengwa sana ukiachilia mazingira yetu ya ufanyaji kazi

Na ninachokishangaa sasa mmetuletea madawati na kusema tusome bure lakini wanaotoa hiyo elimu wametazamwa vipi

Msipojirekebisha kwa haya sisi waha bado tutaendelea kuamini sababu ya ujinga wetu ni Nyerere na ninyi waendeleshaji mnapitia njia ileile

Nawasilisha
Mtoa mada una matatizo yako binafsi. Waha wapo waliosoma kama makabila mengine. Inawezekana wewe huwafahamu pengine kwa sababu ya ama ulimbukeni wako ama ushamba wako. Hakuna Mbunge wa mkoani kigoma ni darasa la saba. Waziri wa Elimu, Fedha ni waha. Nenda hapo UDSM angalia wako wangapi. Serikalini na kwenye makampuni binafsi waha wapo wengi na wanafanya kazi vizuri na kwa uaminifu. Unachotakiwa kuja ni muundo wa kijiografia ndiyo umechangia mambo mengi kutofanikiwa. Waha waliegemea kushughulika na Congo / Burundi kwenye shughuli za kiuchumi. Matokeo yake Tanzania hayapimiki na hayapo. Usidanganye watu hapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom