Nyerere alikuwa na tamaa ya madaraka


Asante sana kwa kumueleza vizuri.
 
 
we nawe bwabwaee.nenda mombasa kama tz hufaidiki

Jibu hoja acha viroja! Ka wewe bwabwa unafkiri kila mtu bwabwa? Kwa utawala wa huyo dikteta Watz wanaofaidika ni wachache sana wengine tunastruggle kimpango wetu au wewe kasisi nini? Afu wewe na huyo Nyerere hamna uwezo wa kunihamisha Tanzania mlivyowahamisha babu zangu eti kuwapeleka kwenye vijiji vya kijamaa inatosha Mungu amuweke Dikteta Nyerere panapostahili
 

Asante kwa kueleza Mazuri na kutokuwa mbinafsi kwa Hayati Julius.Mapungufu kila mtu anayake; huwa tunatakiwa kupima mema na, yakizidi mabaya tuna kila sababu ya kumsifu mtu huyo kwa mema yake!

Mabaya yake hawa waiomfuatia katika Urais naona kila siku twalalama kuwa wanayafanya kupita hata Julius alivyo-imagine kuwa yanaweza kufanywa!
 

Episionage;
Kuna aliyewahi kumu-UNGUsha (yaani kumpa sifa ya u-UNGU) Nyerere ndani ya jukwaa hili, labda tuseme? So you hate him, isn't it?
 

Kwenye blue, unasema alikuwa na Tamaa ya madaraka kwasababu hakuwa mkamilifu na hakuna binadamu mkamilifu. Kwa sababu hizo ulizotoa, viongozi wote pamoja na sisi na wewe (kama wewe ni binadamu) wana tamaa ya madaraka, kwa vile hakuna mkamilifu.


Kwenye red, ningependa tu kujua kutoka kwako, je Nyerere J.K mwenyewe aliwahi kukwambia kuwa alikuwa na hofu hiyo? Au ndio psychology yako uliyopata kijiweni ndio imekupa hiyo conclusion?
 
 

kwa hiyo unataka kusema kuliko nyerere dikteta bora kikwete au mwinyi aliyeruhusu mambo yafanyike namna yoyote apendavyo. na kumopa madaraka kila mtu anayeyahitaji hata kama hana sifa?
 
Heri tamaa ya Madaraka kuliko Ufisadi na uasherati kama hao unaowajua wewe

mkuu elli,
hakuna heri yoyote kati ya hizo mbili,
hata hivyo kwa wale wanaofikiri nyerere alikuwa na uchu wa madaraka wanakosea,nyerere hakuwa na tamaa ya madaraka kama watu wanavyofikiri.angekuwa nayo asingeling'atuka kwani alikuwa na uwezo wote wa kuendelea kukaa katika madaraka na dola ikamlinda. kwa busara hakutaka kufanya hivyo.
 


1.
hakuna uhusiano, mtu anaweza akawa sio makamilifu lakini hana tamaa ya madaraka
2. kumuachia kawawa madaraka bado haithibitishi kuwa alikuwa na uchu wa madaraka isipokuwa aliamini kuwa kawawa pamoja na kutokuwa na kisomo kikubwa na mapungufu mengine aliaminika, lakini bado kwa kumuachia kawawa madaraka hakuoneshi kuwa alikuwa na uchu wa madaraka kwani ansingemuachia angekaa mwenyewe uwezo huo alikuwa nao.
3. pamoja na elimu walizonazo mwal hakuwa ameridhika kuwa wana uzalendo wa kuendeleza nchi hii kwa wakati huo na mtazamo wao pasishaka haukuwa alivyoona ungelipekeleka taifa pazuri. aliamua kwa busara kwa maslai ya taifa si kwa maslai yake yeye . maana yeye mwal aliwajua haio vizuri kuliko mimi na wewe leo hii
4.maelezo ya 3 yanajibu na hapa pia
5. ni kweli hakuwa mungu alikuwa na mapungu kama wengine.lakini alijitahidi kufanya yale mazuri aliyoamini yangetufaa sote. sio leo watu wanafanya yale yanayowafaa wao tu. ona tulipo.
haya ni maoni yangu
 
hoja hapa ni kuogopa wenye uwezo wa kuongoza kuWAWEKA KARIBU

mkuu una uhakika kuwa hao uliowataja wana uwezo wa kuongoza wano huo uwezo? wamelifanyia nini taifa hadi hivi tunavyosema. je ni wazalendo? je una hakika alikataa kuwapa nafasi jkwa sababu hiyo unayoifikiri?
 

tena si bwabwa tu ni shehtwani
 
Asante sana kwa kumueleza vizuri.

kwanza mtoa mada anaongea lakini hajui HISTORY vipi uhuru ulipatikana na akina nani walikua na ushawishi mpaka uhuru ukapatikana na kama ange waacha hao madhalagani yangetokea...nyerere bila SIR G. KAHAMA..PAULO MWANI..NA AKINA BOMANI..NA CHEEF.MAREALE..UHURU TUSINGEPATA..hawa ndio walikua washawishi wakuu kwa WAKULIMA na ndio walikua wakuu wavyama vya Ushilika wakati huo...Rashidi M.Kawawa nae alikua muhim sana kwa Nyerere sababu ndio
 
Asante sana kwa kumueleza vizuri.

kwahiyo NYERERE bila Kawawa asinge fanikiwa malengo kwani Kawawa alikua ndio mwenyekiti na mwanzilishi wa Chama cha wafanyakazi TANGANYIKA na alikua haogopi Wazungu na alikua ana ushawishi mkubwa kwa wafanyakazi kama alivyokua CHILUBA..ZAMBIA...sasa mtu waaina hiyo usipo mshaka kalibu akiasi ana wafuasi wengi hilo ndio nyerere aliliona na akawa makini sana juu ya hilo ...kwahiyo Nyerere aliishi kwa kukumbuka wapi alikotokea..NYERERE
 

Ponda ametuharibia watu jamani. Anza na matatizo ya pale kwenu Nshara, nani chanzo?? Mnajazwa ujinga na nyie mnadanganyika kirahisi. Go to hell.
 

haisaidii kwa sasa, mwache apumzike kesho ni mimi na wewe.
 
toka prezidaa aitwe dhaifu na JJ Mnyika bac wapambe wake wanahangaika kutaka kudissolve kaul,huwezi kumwita nyerere dhaifu au alikuwa na uroho wa madaraka, labda utupe ushahid wa uroho wa madaraka wa nyerere
 

MKUU naomba kuuliza,Kawawa alikuwa anajua kiingilishi?
 
Na kwa nini tunakaa hapa kumjadili Nyerere na uongozi wake wa miongo mingi iliyopita, ambao hatuwezi hata kuurekebisha hivi sasa, na tunaacha kutumia hizo nguvu kujadili matatizo ya uongozi uliopo sasa ambayo tuna uwezo wa kurekebisha?

Jadili jinsi kundi letu litakavyopanda treni ambayo ipo kituoni sasa hivi, sio jinsi ambavyo tulipaswa kupanda treni ambayo tayari ilishaondoka na kutuacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…