Nyerere ajificha kwa Wassira

Nyerere ajificha kwa Wassira

mtahengerwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2011
Posts
384
Reaction score
173
Mwl nyerere aliyeipenda nchi yake Tanzania na watu wake aliipenda upeo.Mwl alikuwa mzalendo wa hali ya juu, uzalendo wake ulijidhilisha katika maisha halisi aliyoishi kiasi kwamba hata alipopewa zawadi binafsi alizileta kwa watanzania.

Mwl Nyerere alikuwa mwadilifu sana kiasi kwamba wakati alipong'atuka hakuwa na nyumba ya kuishi kijijini kwake mpaka serikali wakaona aibu wakaamua kumjengea.Mwl Nyerere hakujua kujilimbikizia mwenyewe bali alipenda kuwalimbikizia watanzania.

Mwl Nyerere alikuwa mchapa kazi.Muda wake mwingi aliutumia kuwahangaikia watanzania.Lakini moyo huo haupo kwa viongozi wetu sasa ambao hutumia rasilimali za nchi kwa manufaa yao na familia zao.

Mwl Nyerere aliichukia rushwa na kusema rushwa ni adui wa haki sitatoa wala kupokea rushwa.Viongozi wetu wamekuwa wanafiki majukwaani wanakemea rushwa maofisini wanakuwa wa kwanza kuomba rushwa.Mwl Nyerere alichukia sana viongozi wanaotumia rushwa kununua uongozi, Leo hii tumeshudia na tunaendelea kushudia viongozi wanaousaka urais wanatumia fedha nyingi kuwanunua wajumbe watakaowapendekeza kwa kuwapigia kura.

Mwl Nyerere aliweka na kuheshimu miiko ya uongozi na kusema uongozi ni dhamana lazima uwaheshimu na kuwatumikia wananchi waliokupa madaraka hayo.Mwl Nyerere alisema ukiwa kiongozi ni wewe tu na wala sio familia yako (mke wako na watoto wako) hao sio viongozi lakini wanatakiwa waishi kwa kuheshimu miiko ya uongozi.

Baada ya Mwl Nyerere kufariki viongozi wetu walioishi maisha ya kinafiki enzi za Nyerere waligeuka kuwa manyang'au na kuanza kutapanya na mambo mazuri aliyoyaweka Mwl Nyerere kwa faida ya watanzania.

WASSIRA pekee ndiye aliyebaki kuwa kielelezo cha maisha halisi aliyoishi Mwl Nyerere na kuyaamini kati ya viongozi tulionao.WASSIRA ni mwadilifu, mchapa kazi, mzalendo na ni viongozi anayeheshimu miiko ya uongozi.

WASSIRA ndio anayefaa kuwa rais ajaye baada ya kikwete kwa sababu nilizozitaja hapo juu na amekuwa kiongo mkubwa sana katika uongozi wa kikwete katika mambo mbalimbali.Hii inatokana na sifa kubwa aliyonayo ya kujiamini na uwezo mkubwa wa kupambanua mambo mbalimbali akaeleweka.

Ndo maana nasema bado tunaye Nyerere anayeishi kwa WASSIRA tumuungo mkono wassira katika mbio zake za urais arudishe hesima ya taifa hii ambayo inaenda kuwa historia na kuwekwa mwenye makumbusho ya taifa.
 
Wassira kiongozi hodari sina wasiwasi nae. hebu na tutsmuona hii 2015... ni zamu yake. muadilifu na mprnda haki. harufu ya Tanzania Makini naiona.
 
Nyerere ajificha kwa wassira .

Hata sie tunakubali ni mchapa kazi, bungeni anasifika kwa kutoa hoja za kutetea haki za wanyonge..
index.jpg invdex.jpg

Itabidi tu tumuamini hasa kwenye maswala ya huduma za afya, tuna uhakika ataleta vyombo vya kisasa, dawa na vifaa mahospitalini..

indnex.jpg
 
Hata sie tunakubali ni mchapa kazi, bungeni anasifika kwa kutoa hoja za kutetea haki za wanyonge..
View attachment 222519 View attachment 222520

Itabidi tu tumuamini hasa kwenye maswala ya huduma za afya, tuna uhakika ataleta vyombo vya kisasa, dawa na vifaa mahospitalini..

View attachment 222521

Hahaa! Hizi picha zimenichekesha sana, za miaka hiyo, lakini hiyo moja akiwa na Mhe. Greyson Lwenge anaandika sio kuwa amesinzia,

Lakini kama hizi ndizo kashfa zake basi anazo element za uanafunzi wa Nyerere( sio Nyerere, na wala hajawahi kujiita hivyo). Kwani amekuwa mtu wa siasa za watu na kiongozi wa Maisha ya Kawaida hata anaweza kushare nao kikombe kimoja.
 
Mungu ampe afya njema wewe ndiye tumaini pekee la watanzania.Mhe. Wassira sikia na uyaonee huruma machozi ya watanzania wanaokulilia, maisha yako, uwajibikaji wako na mzalendo wako umewajangea watanzania imani kwako, nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kuelekea plot no 1.
 
Ameanza kazi Wizara ya Kilimo tumpe nafasi kwanza atekeleze, mwenye update Kama Wakulima wameanza kulipwa madai yao atujulishe hapa
 
Ameanza kazi Wizara ya Kilimo tumpe nafasi kwanza atekeleze, mwenye update Kama Wakulima wameanza kulipwa madai yao atujulishe hapa

Yaani watalipwa sababu yeye kawa waziri hapo???!!
Au una maana gani???!!
 
Ameanza kazi Wizara ya Kilimo tumpe nafasi kwanza atekeleze, mwenye update Kama Wakulima wameanza kulipwa madai yao atujulishe hapa

Siku moja baada ya kuteuliwa kwenda wizara hiyo ametangaza kuwa lazima wakulima walipwe! hii ni habari njema sana kwa wakulima ambao walikuwa hawajui hatima ya malipo yao.Hongera sana mhe. Wassira juhudi zako tunaziona.
 
Umepewa kiasi gani kupiga promo hii? Naona korabo iko Vyema na wapambe wengine wanashusha mistari.. Hii si zamu ya wassira wala sisiem tupishe wengine wapya kabisa kwenye utawala wabadili upepo.
 
Yaani watalipwa sababu yeye kawa waziri hapo???!!
Au una maana gani???!!

Mie nimetaka update tu Mkuu maana ametangaza wataanza kulipwa jana, mengine hayo ni majungu tu.

Kama hawajaanza kulipwa tujue kwanini amewahadaa wakulima.
Kama wanalipwa stahiki ya jasho lao tumpongeze kwa kusimamia haki za Wanyonge kuliko viongozi wengi walioko serikalini.
 
tangu nae aungane na manyang'au wenzake kuiwtetea katiba yao sina imani naye kwakua nae ni sukule wa limumba
 
Umepewa kiasi gani kupiga promo hii? Naona korabo iko Vyema na wapambe wengine wanashusha mistari.. Hii si zamu ya wassira wala sisiem tupishe wengine wapya kabisa kwenye utawala wabadili upepo.

Mimi sijapewa kitu chochote wewe mwenyewe unawajua wagombea wanatumia fedha ningezitaka ningeenda huko kuzitafuna ! Mimi napigania heshima ya taifa hii.Nawapigania wazalendo wanaolipenda taifa hili kwa moyo wa dhati ambao maisha yao na matendo yao yanatupa picha kamili ya uzalendo wao.Nawapigania wazalendo watakaoguswa na maisha duni ya mama zetu na baba zetu huko vijijini ambao hawajui kesho yao itakuwaje.Wassira ni kielelezo cha viongozi tunaowahitaji ndio maana watanzania wameweka matumaini yao ya mwisho kwa Wassira.
 
Mie nimetaka update tu Mkuu maana ametangaza wataanza kulipwa jana, mengine hayo ni majungu tu.

Kama hawajaanza kulipwa tujue kwanini amewahadaa wakulima.
Kama wanalipwa stahiki ya jasho lao tumpongeze kwa kusimamia haki za Wanyonge kuliko viongozi wengi walioko serikalini.

Kama wameanza kulipwa ni sababu pesa imepatikana sio sababu yeye ni waziri, na kama imeanza kulipwa basi ni mipango ya aliyeondoka!!!

Kila mtu apae kwa mbawa zake! !!!
 
Kama wameanza kulipwa ni sababu pesa imepatikana sio sababu yeye ni waziri, na kama imeanza kulipwa basi ni mipango ya aliyeondoka!!!

Kila mtu apae kwa mbawa zake! !!!

Wako mwenye kuandaa na kuhakiki kwa Mara ya mwisho malipo na wiki hii hii wananza kulipwa! Na si kweli kwamba mpango huo ulioandaliwa na waziri aliyepita! Kila mtu anamfahamu chiza kuwa ni waziri asiye na mwelekeo wapi alipo na wapi anapoenda.
 
WASSIRA ni mzalendo, muadilifu, msafi, mchapakazi, ana uwezo mkubwa wa kubambanua mambo na ana msimamo Mkali kuhusu masuala mhimu ya taifa hili! huyu ndiye rais anayependwa na watanzania wote kwenye kiu ya kuona maendeleo na kuona rasilimali zao zinasimamiwa vizuri ili ziwanufaishe watanzania wote!
 
Back
Top Bottom