Nyani haoni kundule

Hassan Mambosasa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2014
Posts
3,988
Reaction score
5,809
Habari zenu wanajamii, natumai nyote ni wenye siha njema. Kwa wale waliyo na shaka kwenye afya zao, Mungu awajalie soha njema na awaondoshee maradhi.
Naomba niwasilishe hili

Mtanzania akibaguliwa, basi sisi huwa wa kwanza kulalamika jamii fulani inawabagua wenzetu huko kwao. Tunaweza kuandaa na kushikilia mabango mitandaoni kukemea jambo baya, hata ulimwengu mzima ukaamini ya kwamba mwenzetu kaonewa kule.

Sisi ni wa kwanza katika kueneza ule ujumbe usemao 'Say no to racism' pale inapotokea mwenzetu kabaguliwa na kikundi cha watu fulani. Yaani mtu kutoka nje akiona harakati hizo, anaweza kusema sisi ni wamoja na wenye kujali mno. Watu wenye kupinga vita ubaguzi kuliko kitu chochote, hata mishipa ya shingo itatusimama mtanzania kabaguliwa huko.

Sasa njoo huku tunapoishi wenyewe, ndiyo utaona sisi ni wabaguzi wakubwa, tunabagua wageni muda mwingine na hata kubaguana wenyewe kwa wenyewe. Najua wengi watakataa hili, ila wacha nikupe walau dondoo chache uelewe sisi ni wabaguzi wa kiwango gani.
Naanza ifuatavyo;

Mosi, utanzania huangalia mtu aliyeupata uraia kutokana na kuzaliwa nchini au kuchukua uraia wa nchi ifuatayo. Mtu yeyote atakayezaliwa hapa na kuishi hapa, akawa hana uraia wa sehemu nyingine yeyote ana haki ya kuitwa mtanzania. Lakuni sisi tutawaita majina kutokana na ngozi zao mara yule mhindi, huyu mwarabu mara yule msomali.
Yaani tunasahau hata wenye ngozi nyeusi waliyopo huko Ulaya haswa Ufaransa pamoja na kubaguliwa sana, hawajawahi kuitwa waafrika wale zaidi ya sisi kujipendekeza kuwaita.
Kwanini msiwaite watanzania kama wamezaliwa hapa na kukulia hapa, hawana uraia wa nchi nyingine yeyote ile. Kama si ubaguzi huu ni nini?

Pili, kihistoria wapo watanzania waliyofanya makubwa kwenye nchi yetu serikalini na kwingineko lakini hawagusiwi hata kutajwa. Yupo brigadia jenerali mwenye asili ya asia kutoka ndani ya jeshi letu wa tangu awamu ya kwanza(naomba nisimgusie sana). Kuna spika Yusufal Karimjee, huyu eti spika wa kwanza wa bunge hata shuleni watoto hawamjui. Mtu anamaliza elimu ya sekondari kuna masomo ya uraia na historia, mtu kama huyo hamtambui. Ila wazawa wenye asili ya hapa, hadi nyimbo wanaimbiwa mashuleni kwa jambo walilolifanya hata kama si kubwa kuliko la yulee!

Tatu, wenyewe kwa wenyewe tunabaguana kwa kabila. Ajira kupata imekuwa tunaangalia kabila na ukanda baadhi ya sehemu kama bosi ni mwenye kutoka sehemu fulani. Ofisini tunajazana mandugu wa kabila moja, na hata ukoo mmoja ilihali watu wenye sifa stahiki kutoka sehemu zingine wapo. Kama huu si ubaguzi ni nini haswa?
Kuoana imekuwa tukijali fulani kutoka kabila fulani, hata tunafikia kupiga marufuku watoto wasiolewe na kabila fulani. Yaani mzazi hata ndugu wapo radhi kumpa laana kijana wao, kisa kaoa kabila fulani. Kama huu si ubaguzi ni nini haswa?
Maendeleo na nafasi za uongozi kuteuliwa kuendana na ukabila hata ukanda, haswa nafasi za juu kwenye taasisi na hata sehemu zingine ndani ya nchi hii. Akifanikiwa kuipata mtu mwingine nafasi adhimu, utasikia mara kapewa kabila fulani na si kusema mtanzania mwenzetu kapewa.
Hivi kutaja msukuma, mhaya, mchaga, mngoni, mzaramo ndo kapewa uongozi, ukioneshwa kuchukizwa na kitu hicho. Nikisema ni ubaguzi nakosea? Achilia mbali utani huu wa makabila ni sehemu ya kudumisha umoja ikiwa utatumiwa vyema. Maana utani huondoa chuki, ikiwa utatumika kiustahiki
Achilia hayo, tumekuwa tukielezana sifa mbaya za kutoka kabila fulani au ukanda fulani. Mara wanawake wa kabila lile wapo hivi, wa ukanda ule wana sifa chafu kadha wa kadha. Yaani kila kabila linatoa kasoro za wenzake, kama vile hawana tatizo lolote.

Sasa nikisema sisi watanzania ni wabaguzi ninakosea? Kwa vitu vichache hivyo nilivyoviorodhesha. Humu nchjni ndo tulivyo, ila likitokea la nje ni wa kwanza kuropoka kuchachamaa kama vile tunatolewa meno yanayouma bila ganzi.
Ama kweli nyani haoni kundule

HEBU KABLA YA KUONDOA VIBANZI KWENYE MACHO YA WENZETU, TUTOE BORITI MACHONI MWETU.

HUWEZI KUUPINGA UBAGUZI NJE YA MIPAKA, WAKATI NDANI UNAISHI NAO. ANZA KUKOMESHA KWANZA ULIYOPO NCHINI NDIYO UFUATE WA UGENINI.


wassalam.



Hassan O Mambosasa,
juniormambosasa@gmail.com
Mwakidila, Tanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ubaguzi upo hata katika familia ya baba mmoja na mama mmoja, hata hao kabila moja au kanda moja unaosema wamejazana ofisini utakuta humo ndani wamegawanyika makundi kadha wa kadha. Kifupi binadamu ni kiumbe mbinafsi sana, na akikosa wakumbagua anaweza jibagua mwenyewe.

Hao unaosema wamezaliwa Tanzania lakini wana asili ya bara fulani wao ndo huwa wa kwanza kuonesha ubaguzi maana hata shule hujenga za kwao, wao wanao dada zetu halafu hawataki sisi tuoe dada zao, na kwenye mambo mbalili mbali ya kijamii hawashiriki labda siasa tu tena huwezi kuwaona wakipiga kura wanataka sisi tuwachague.
 
Ni kweli uyasemayo, ila hebu fikiria kama wenyewe tuna ubaguzi. Tutaanza vipi kupambana nao ili wasiweke ubaguzi ilihali sisi ni wabaguzi pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…