DOKEZO Nyamanoro - Mwanza wanalazimisha tulipe Service Levy kwa cash, kwanini wasitupe Control Number?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kata ya Nyamanoro Mkoani Mwanza wamekuwa wakiendesha kampeni ya kufunga maduka na kuchukua waliopo Madukani, hilo linafanyika kama unakuwa hujalipa Service Levy.

Hili suala sijui limetoka wapi na mimi kama Mfanyabiashara ni mara ya kwanza kusikia natakiwa kulipia Service Levy ya Shilingi 50,000.

Mfano mimi wamechukua Mfanyakazi wangu wanataka tulipe Shilingi 50,000 pamoja na Shilingi 100,000 ya faini na zilipwe cash, wanakusanya Watu wengi wakitumia Mgambo.

Sisi Wafanyabiashara tunaona huu ni uonevu kwani tungeelimishwa kwanza..na pia tupewe Control Number tulipe na sio kutakiwa kulipa Cash.
 
Hii ni harufu ya wizi, gov ina require cn number in almost kila nyanja. Cash inarudisha urasim. Mamlaka ziingilie
 
Back
Top Bottom