Napenda Nichukue Nafasi hii Kumpongeza sana, sana Mh. Lazaro Nyalandu kwa Kuhama CCM! Ila kuna Mambo mawili ningemtaka Ayafanye.
1) Wakati wa Kupitishwa Kwa sheria za Habari, Ilidaiwa na Ushahidi wa Picha na Video Ukatolewa kwa waandishi, Swali la Kiongozi wa Upinzani Bungeni Likakataliwa na Naibu Speaker ati Lisijibiwe. Ishu ilikuwa hivi?
Nd. Magufuli alikwapua 2.7 Bilioni hazina na Kuwapa CCM. Wagawane, wote wakapewa Milioni 10 kila mmoja! Wewe Utusaidie Je Ulipewa Milioni 10 na wewe? Maana Ulikuwa ni CCM Yes or No! Kama Jibu ni Yes Basi Naomba Uite Mkutano wa waandishi, Uzirudishe Kama Ngeleja alivyofanya Zile za Escrow Mil 40.4 Kisiasa Utatisha sana! Kama Jibu Ni No Pia Ita Waandishi wa Habari Utuambie kuwa sio Kweli ili tuliojenga Kinyongo na Rais Magufuli kwa Hili Tuombe Msamaha. Nawahakikishia Watanzania Wote Nitapiga Magoti na Kumwomba Rais Magufuli Msamaha kwa Kumkomalia kwa issue ya Uwongo, Ikiwa utasema hakuna Milioni 10 walizopewa wabunge wote wa CCM.
Lingine Nalotaka Nikuombe, Je Ulipokwenda Kumtazama Lissu ICU, na Ukarudi, Baada ya Muda Ukatoa utetezi wa kwanini wewe ulienda Kumtazama! Je kuna Namma yoyote ambayo kuna watu au mtu alikunyanyapaa kwa kumjulia hali Lissu?
Haya Mambo Niliyokuomba na Kukushauri Ni Jiwe la Msingi wa Safari yako Mpya ya Siasa! Its now or never Usidharau!