Nyalandu anatafuta nini kwa Lowassa, Sitta na Membe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyalandu anatafuta nini kwa Lowassa, Sitta na Membe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Independent Voter, Feb 1, 2012.

 1. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbunge kijana Lazaro Nyalandu anasema kwa namna yoyote ile, yeye si mgombea wa urais wa Tanzania . Alipiga hatua moja mbele na kusema hayuko chini ya kundi lolote kati ya yanayotajwatajwa kujipanga kugombea urais wa Tanzania mwaka 2015.

  Lakini Mh.Nyalandu pamoja na kujaribu kukimbiza ubawa wake katika rafu na mpambano usio na huruma wa kuwania urais, bado alionyesha jinsi alivyo na mahusiano mazuri na hao aliojitenga nao(Lowassa,sitta na membe).

  Akimzungumzia Lowassa alisema: "…ninamheshimu, ninamheshimu sana (Lowassa) na ni mara nyingi niseme tukiwa Dodoma nakunywa naye chai. Mi naendaga (naenda) nyumbani kwake. Na kuna kipindi nimeshawahi kuambiwa na baadhi ya watu tulionekana Monduli, kwa hiyo, moja kwa moja uko kwenye hilo kundi la mzee wa Monduli. Nilicheka sana ."

  Kuhusu Sitta alisema, "Huyu ni ‘mentor' (mwalimu). Ni mtu, ambaye kwanza ananishauri vitu vingi. Ni rafiki yangu hata kama akinisikia. Sidhani kama kuna siku itapita sijaenda kumwona mzee Sitta. Kama hatujaonana kesho yake tutaonana, tutazungumza, tunaenda kwenye maeneo mengi pamoja, jambo lipo tunashauriana."

  Kwa upande wa Membe alikuwa na haya: "Sasa turudi kwa marafiki zangu wanaojulikana wa kawaida, Bernard Membe. Ni rafiki yangu mzuri sana . Tumeanza naye Bunge mwaka 2000. Unajua siamini kwamba mwaka 2000 ni karibu miaka 12 iliyopita. Maana yake ni kama jana tu. Tukiwa 'ma-back bencher', Kamati ya Mambo ya Nje wote. Sisi ni marafiki, yaani ni marafiki. Kwanza nyumbani tunakaa jirani. Jioni lazima tuzungumze. Kwa simu lazima tuongee. Nikitaka 'kubipu' ugali nyumbani kwake sipigi hodi. Ni marafiki wa kiasi hicho. Kwa hiyo, mtu anayejisikia kunihusisha na lile kundi kama lipo, off course wamesema sana ."

  Nyalandu ana haki ya kusema hicho alichosema. Ni haki yake. Lakini katika ulimwengu wa siasa hakuna kitu chochote kinachotokea kwa bahati mbaya kwa wanasiasa aina ya Nyalandu. Kila kitu kinapangwa, kwa nini aseme sasa na aseme nini.Kwa kuzingatia mbinu za kisiasa hasa katika ulimwengu wa sasa ambao habari nyingi hutengenezwa na ‘ma-spin doctors', Nyalandu naye amejitengenezea habari yake kwa nia ya kupata manufaa makubwa ya kisiasa pia.

  Kinachoonekana haraka haraka ni kwamba Nyalandu anawakana akina Lowassa, Membe na Sitta, lakini anathibitisha kuwa yeye na wote hao ni damu damu. Hapa anajifungamanisha zaidi nao; maanake ni kwamba anawataka wote kwa kuwa hana hakika ajiegemeze wapi. Hii inaweza kuwa ni strategy nzuri hasa kwa mwanasiasa kijana wa aina yake, Nyalandu anajijua kuwa yeye si jabali ndani ya CCM, si jabali ndani ya mkoa wa Singida, wala si jabali kwa maana ya mwanasiasa mwenye mikakati na mbinu ya kuunganisha makundi na hivyo kusaidia kukusanya kura kama suala ni kupiga kampeni kwa wajumbe wa vikao vya maamuzi vya CCM.Analijua hili vizuri, lakini kama mwanasiasa yeyote yule angetamani sana awe na nguvu hizo. Kwa maana hiyo, anachojaribu kufanya kwa sasa ni kujaribu kujijenga kisiasa ili kuwa na nguvu za kukusanya kura na pengine kuwa nguzo ya kisiasa siku za usoni.

  Je kwa kumtazama hapa Nyalandu tunaweza kusema ni mwanasiasa kijana mwenye kufanya siasa zake kisayansi kwa ajili kujijenga kisiasa na kutengeneza mtandao wenye nguvu siku za usoni utakaomuwezesha pengine kutekeleza malengo yake makubwa ya kisiasa aliyonayo ama ni mchumia tumbo ambae mkakati wake katika kuuma na kupuliza; anatamani kula keki yake lakini bado ibaki mkononi..isiishe?
   
 2. D

  DOMA JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Anagombea kupitia cck au?
   
 3. K

  KIFILI Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huyu dogo kuna karata inaonekana anaicheza,si wa kumbeza hata kidogo,kuna kitu anafanya! tusubiri tuone ataishia wapi
   
 4. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  du kazi ipo mwaka huu lakini yote kheri!
   
 5. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  mnafiki kama walivyo wanyaturu wengi ninao wafahamu
   
 6. k

  kuzou JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kama urais ni urembo tutamchagua ben kiny.'eee
   
 7. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Au anataka kuifufua tena Fursa Sawa kwa Wote
   
 8. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  mnafiki kama walivyo wana magamba wengi!
   
 9. K

  KIFILI Member

  #9
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama ataibeba dhana hiyo kwa vitendo na kuichukua kuwa sera yake nitamuunga mkono,imekaa vizuri kwa sisi tunaotazama sera!
   
 10. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  mambo mawili namkubali Nyalandu. Ana akili na mchapakazi. Namfahamu. Kinachomharibu ni pesa alopata inayomfanya afikiri its a time to be high in Tanzanian politics. Its true that he is not thinking for presidency. But he is for something closer, something which at end of the day it may bring him in! Only the system corrupts him
   
 11. hollo

  hollo JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 781
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Nyuki hufuata nini kwenye maua?
   
 12. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mimi binafsi japo mwanzo nillianza kumbeza lakini ameanza kunitisha,kuna mchezo wa kisayansi anaucheza ukimfuatilia nyendo zake utagundua kila analolifanya zikiwemo hizo chai zake anazosema kunywa na kina lowassa zina malengo mazito,naamini sio urais 2015 ila kuna kitu anakifanya na yuko serious nacho.....let us wait na c
   
Loading...