Nyalandu amaliza utata wa tozo

Nyalandu amaliza utata wa tozo

Jodeny

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2012
Posts
201
Reaction score
25
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ametia saini Tangazo la Serikali (GN) kuhusiana na utozaji toza kwa hoteli za kitalii zilizopo katika Hifadhi za Taifa.

Pia amewaonya wawekezaji wanaokwepa kulipa kodi halali za serikali kuwa, hatasita kuchukua hatua kali na kwamba, ni lazima mapato ya serikali yakusanywe kikamilifu.

Akizungumza ofisini kwake jana, wakati wa kutia saini tangazo hilo, Nyalandu alisema amechukua uamuzi huo baada ya watalaamu wa wizara pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuridhia baada ya kulipitia kwa umakini.

Hata hivyo, alisema mfumo wa utozaji tozo hizo utaendelea kufuatiliwa na kufanyiwa marekebisho kwa kadri itakavyoonekana inafaa ili kuhakikisha taifa linakusanya mapato yake kikamilifu.

Alisema hatua hiyo utekelezaji wa Azimio la Bunge na Mahakama Kuu na kwamba, hoteli zote zinazopaswa kulipa tozo hiyo zitafikiwa ili kulinda mapato ya serikali.

“Nafurahi kueleza umma kuwa leo (jana) ninasaini Tangaza la Serikali kuhusiana na tozo za hoteli za kitalii ndani ya hifadhi zetu. Ni jambo ambalo lilizua mjadala, lakini kwa kawaida serikali hufanya kazi zake baada ya kupata ushauri wa kitalaamu na kujiridhisha na kila kinachofanyika.

“Watalaamu wa Wizara yangu na wale wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali…hatua zingine za utekelezaji zinaweza kuendelea,” alisema Nyalandu.

Awali, Nyalandu aliagiza kufanyika kwa uhakiki wa kina kutokana na hoteli zaidi ya 25 kutokuwemo kwenye orodha ya zinazotakiwa kulipa tozo hiyo.

Alisema kamwe asingeweza kukurupuka kwa kuwa hoteli zilizoidhinishwa ndani ya hifadhi za taifa ni 57, lakini zilizoorodheshwa ni 30 tu.

Kutokana na hilo aliagiza ukokotoaji wa tozo hiyo uzingatie haki kwa kuwa ni mojawapo ya masuala ya msingi yaliyomfanya kuchelewa kusaini tangazo hilo.

“Nilitaka kujiridhisha kwanza kabla ya kufanya uamuzi kwa kushirikiana na wataalamu wangu wizara, ninasaini lakini tutafanya maboresho kwa sababu kuna hoteli kubwa zimeachwa jambo ambalo halikubaliki kwa maendeleo ya nchi,” alisema Nyalandu na kuongeza:

"Naipenda nchi yangu na nina uchungu nayo… iwapo ningekubali kusaini hii bila kujiridhisha kusingekuwa na usawa kwani, kuna hoteli za viwango tofauti.”

Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) ilitaka kulipwa tozo kamili na kutangaza tozo mpya 2007, jambo lililosababishwa kuwepo kwa kesi hiyo, ambayo ndio kitendawili chake kimeteguliwa rasmi.

Katika hatua nyingine, Nyalandu alisema wizara yake itaendelea kuwa kinara katika ukuaji wa uchumi wa taifa na kwamba, itaongeza juhudi zaidi za kukusanya maduhuli ya serikali.

Amesema sekta ya utalii nchini itaendelea kuboreshwa na kupewa kipaumbele na kwamba, watumishi na watendaji wote wataendelea kujipanga ili kuhakikisha ufanisi kazini unaongezeka maradufu.


IMG_0630.jpg
Nyalandu akisaini Tangazo la Serikali ofisini kwake jana.
IMG_0646.jpg
Nyalandu akikabidhi GN kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Celestine Gisimba, kwa hatua za utekelezaji
 
Sasa hapa bei inapanda kwa Watalii wasipokuja Mnadai kwasababu ya Lema Arusha serekali yakikanjanja kanjanja
 
Back
Top Bottom